Saturday, 28 September 2013

MAGAZETI YA MWANANCHI NA MTANZANIA YAFUNGIWA-Yadaiwa kuchochea amani ya nchi


Septemba 28,2013.
SERIKALI imeyafungia kuchapisha magazeti ya MWANACHI na MTANZANIA kuanzia tarehe 27i Septemba,2013 kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika  habari na makala za uchochezi kwa nia ya kusababisha uhasama na kusababisha wananchi wakose imani na vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini.

Gazeti la Mwananchi limefungiwa kuchapisha kwa siku kumi na nne(14), kuanzia 27,Sepemba 2013.Adhabu hii imetangazwa na tangazo la serikali hapo jana (Government notice)namba 333 la tarehe 27 Septemba, 2013.

Gazeti la Mwananchi limepewa adhabu hiyo hivi karibuni kwa madai kuwa limechapisha habari zenye uchochezi na uelekeo wa uvunjifu wa amani, Limetolea mfano tarehe 17,July 2013 katika  toleo namba 4772 lilichapisha habari kuwa "MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013" kwa kuchapisha walaka uliozuiliwa kwa kutumika na vyombo vya habari,walaka huo ulikuwa wa siri haukupaswa kuchapishwa na vyombo vya magazetini.

 Aidha katika toleo la Jumamosi tarehe 17,Agosti 2013 lilichapisha habari yenye kichwa cha habari kisemacho "WAISLAM WASALI NCHINI KWA ULINZI MKALI" habari hiyo ilikolezwa na picha ya mbwa aliyeonekana na hasira kali,habari hiyo ilipeleka tafsiri kuwa jeshi la polisi lilipeleka mbwa katika maeneo ya ibada la waumini wa kiislam jambo ambalo si la kweli.

Jeshi la polisi katika diria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya misikiti. Serikali na jeshi la polisi linaheshimu na kuzingatia maadaili ya dini hiyo hivyo vinadai kuwa hawawezi kupeleka mbwa katika maeneo hayo.

Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kuchapisha habari na matangazo yake kwa siku tisini(90)kuanzaia jana tarehe 27 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi, imedaiwa kuwa gazeti hili limeonywa mara nyingi kuacha kuchapisha habari zenye uchochezi na zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani na kuwa lizingatie maadili ya fani ya habari.

Pamoja na kuonywa gazeti hili halisikia onyo la msajili wa magazeti mfano toleo lililochapishwa tarehe 20 Machi 2013 toleo namba 7262 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho "URAIS WA DAMU" na chapisho linguine la terehe 12 Juni 2013 lenye chapisho lenye toleo namba 7344 lilichapisha makala isemayo "MAPINDUZI HAYAEPUKIKI".

Aidha siku ya Jumatano tarehe 18 Septemba,2013 toleo namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha habari isemayo  ""SERIKALI YANUKA DAMU" taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizounganishwa kwa ustadi mkubwa kupitia teknolojia ya kompyuta huku picha hizo zikiwa zimetapakaa damu nyingi  mithili ya damu nyingi kumwagika. Katika taarifa hiyo gazeti hilo lilidai bila uthibitisho  kuwa jeshi la polisi linahusika na waathirika waliomumizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na wengine kuvamiwa na kuumizwa vibaya.

Vilevile gazeti hilo limeishutumu serikali kwa kuwa goigoi katika kushughulikia masuala ya kigaidi yanayotokea nchini.