Sunday, 15 September 2013

AUC hosts a Gala Dinner and Award Ceremony for staff members.

Description: IMG_6744 copyAddis Ababa, Ethiopia – 14th September, 2013: The African Union Commission (AUC) staff and their families marked the 50th Anniversary of the OAU/AU today 14th September 2013, with day long celebrations that culminated in a Gala Dinner and award ceremony hosted at the Headquarters.

Through this initiative and in line with the year-long celebrations of the 50th Anniversary, the Commission celebrated the dedication, commitment and achievements of all staff members who are seen as key stakeholders in the implementation of the vision and mission of the organization.

“The AU Commission staff ensures that the wheels of our Union keep turning” said the Chairperson of the Commission Dr. Dlamini Zuma during her welcome speech.

After congratulating all participants, the Commissioner for Social Affairs Dr Moustapha Kaloko announced the names of long serving staff members who received their award from the Chairperson and Deputy Chairperson Mr Erastus Mwencha. Testimonies highlighting personal experiences, sharing memories and high moments within the continent and the organisation were heard from four of the long serving staff members. 

Description: IMG_6734-001 copyTrophies were also awarded to the winners of the various sporting activities and matches that took place during the celebratory day, such as: Football, Tennis, Table Tennis, and Basketball.

The event, moderated by the Director of Social Affairs of the AUC, further entertained the invitees with a cultural fashion show and various vocal and dance performances notably from the AUC Choir and children among others.
MFM/

SERIKALI KUUNDA UPYA SHERIA YA KUDHIBITI DAWA ZA KULEVYA-Yasema sheria iliyopo sasa inamapungufu makubwa,tatizo linalazimu marekebisho ya haraka.


 

Septemba 14, 2013- Jumamosi.
SERIKALI inakusudia kuifanyia marekebisho sheria ya kudhibiti dawa za kulevya ya mwaka 1995, ili kuongeza kasi ya kukabiliana na tatizo hilo. Hatua hiyo inakuja baada ya Serikali kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kuweza kuifuta sheria hiyo na kutunga sheria mpya, itakayosaidia kuzuia mianya yote inayochochea tatizo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alisema sheria iliyopo sasa ina upungufu mkubwa hivyo inalazimu marekebisho ya haraka.

Lukuvi, ambaye pia ni Mbunge wa Isimani, alisema upungufu huo unakwamisha jitihada za udhibiti na wakati mwingine watuhumiwa wanaojihusisha na biashara hiyo haramu wamekuwa wakishinda kesi zao mahakamani na kuleta hisia mbaya kwa jamii.

“Tunataka kutunga sheria mpya ya kupambana na madawa ya kulevya, ambayo inayotumika sasa ina mapungufu, pia tunataka kuanzisha chombo maalumu ambacho kitakuwa na mamlaka ya kisheria ya uchunguzi, kukamata na kupekua, ambacho kitakuwa na uwezo huo kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) isiyoingiliwa na chombo kingine.”


Alisema sheria hiyo imekuwa ikitoa adhabu isiyoendana na ukubwa wa makosa husika, jambo linalochochea kuendelea kushamiri kwa biashara ya dawa za kulevya.

“Mfano kifungu cha 21 kinachowahusu wafadhili wa biashara haramu ya dawa za kulevya, kinatoa adhabu ndogo ambayo wanaomiliki biashara hii wanakuwa na uwezo wa kulipa faini.

“Adhabu iliyopo ni faini ya shilingi milioni kumi au kifungo cha maisha, lakini adhabu hizi haziendi pamoja, inampa uhuru jaji au hakimu kutoa maamuzi ya kifungo au faini,” alisema.

Naye Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa, alisema watuhumiwa wa makosa hayo wamekuwa wakifikishwa mahakamani bila ushahidi na baadaye kuachiwa.

“Kama tukimkamata mtu anafanya biashara ya dawa za kulevya na kukosa kidhibiti, tunampeleka mahakamani anakuwa chini ya uangalizi wa polisi na mahakama kwa miaka mitatu au mitano, kutegemeana na mahakama itakavyoona,” alisema.


Mwandishi: Margreth Itala