Saturday, 31 October 2015

Received by Interior CS, Joseph Nkaissery, at JKIA on arrival from India where I attended the 3rd India-Africa Forum Summit.
User comments
Baadhi ya vijana hao wakiwa darasani wakifurahia masomo wanayopatiwa ya kujiandaa na elimu ya sekondari katika kituo hicho cha Furahini mkoani Kilimanjaro.
Na Mwandishi wetu
TAASISI ya misaada ya Mo Dewji Foundation imekubali kufadhili  mradi wa kituo cha mafunzo cha vijana cha Furahini (FYLC) wenye lengo la kuboresha upatikanaji wa elimu katika kijiji cha Kisangara mkoani Kilimanjaro.
Imeelezwa kuwa taasisi hiyo ya bilionea Mo Dewji imetoa shilingi milioni 7 kusaidia ujenzi wa miundombinu inayotakiwa na kituo hicho chenye lengo la kuboresha elimu kwa watoto wa kijiji hicho.
Baadhi ya watoto hao ni wawafanyakazi wa mashamba ya Mkonge ya MeTL yaliyopo jirani  na kijiji hicho.
Ufadhili huo unaenda sambamba na sera za MeTL za urejeshaji wa faida yake kwa wananchi kama sehemu ya wajibu wake kwa jamii, wenye lengo la kuimarisha ustawi wa jamii inayochangia biashara za kampuni hiyo.
Taasisi ya Mo Dewji ambayo ndiyo inatekeleza wajibu wa kundi la makampuni ya MeTL la kurejesha faida kwa umma, kwa ufadhili huo kwa kikundi cha Furahini wametanua wigo kutoka katika shughuli mbalimbaliw alizokuwa wakufadhili mkoani Singida.
Lengo la ufadhili huo ni kuwezesha jamii yenye kipato cha chini kabisa kuweza kumudu mikiki ya elimu ili kukabili umaskini.
Toka mwaka 2000 kundi la makampuni ya MeTL imekuwa ikitanua mazingira ya urejeshaji wa faida kwa umma kutokana na shughuli zake mbalimbali. Katika kipindi cha miaka mitano taasisi ya Mo Dewji imetumia zaidi ya dola za Marekani milioni 3 kusaidia miradi mbalimbali ya jamii.
User comments
Baadhi ya vijana hao wakiwa darasani wakiendelea na masomo katika jengo la kituo hicho cha Furahini ambacho kinatarajiwa kukabaratiwa na kwa msaada wa Mo Dewji Foundation.
Tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo, shughuli mbalimbali zimedhaminiwa na kufadhiliwa. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule, uchimbaji wa visima, ugawaji wa vyandarua, usambazaji wa unga wa mahindi kwa wananchi waliokumbwa na baa la ukame kwa mwaka 2005-2006,ufadhili kwa wanafunzi wa sekondari,afya kw awale waliozidiwa kiafya, kujenga kitengo cha macho katika hospitali za mkoa,kuweka taa katika mitaa, msaada wa chakula kwa waliokumbwa na ugonjwa wa ukimwi, ununuzi wa vifaa vya michezo na vifaa vya wakulima.
Kwa mujibu wa mratibu wa kituo hicho cha Furahini (FYLC) Bw. Msuya Isiaka, wazo la kuanzishwa kwa kituo lilitokana na uzoefu wa muda mrefu wa ufundishaji katika eneo hilo la mahusiano ya jamii.
Alisema wazo la kuanzishwa kwa  kituo limetokana hasa na matokeo mabaya ya mitihani kwa wanafunzi wanoasoma shule za umma katika kijiji hicho.
 “Elimu imekuwa tatizo kubwa katika jamii yetu hasa katika shule za serikali ambazo mara nyingi zimejikuta hazina walimu, na kama wakiwa wamebahatika wanakuwa na mwalimu mmoja wa somo la hisabati kwa shule nzima, bila kutaja masomo mengine kama fizikia, kemia na  bayolojia,” alisema Isiaka na kuongeza kwamba kuna shida kubwa ya uwajibikaji kwa wlaimu na hivyo kluleta athari mbaya kwa wanafunzi.
“Tunaamini kwamba silaha yetu kubwa ya kukabili umaskini unaozunguka katika vizazi vyetu hapa Kisangara ni kuwa na elimu bora” alisema.
User comments
Kwa mujibu wa Isiaka kituo hicho kinatakiwa kuwa na maktaba kamili na chumba cha tehama.
 “Kwa kuwa na miundombinu hiyo ya kujifunzia  ya maktaba na tehama, wanafunzi wanakuwa katika nafasi ya kujifunza vyema na kuwa katika hali ya kukabili umaskini unaozunguka janmii yetu.” alisema.
Mratibu huyo alisema kwamba mafunzo katika kituo hicho katika masomo ya kemia,fizikia,bayolojia na hisabati yalianza Juni 2015.
Kituo cha Furahini ambacho kimejengwa katika ardhi yenye ukubwa wa nusu eka katika kijiji cha Kisangara kata ya Mtuva katika wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjarokipo umbali wa kilometa 2.5 kutoka kituo cha mabasi cha Kisangara.
Kijiji cha Kisangara  ambacho kipo katika eneo kame wastani kina wakazi wa kutoka makabila mbalimbali ambayo yalifika hapo kufanyakazi katika mashamba ya mkonge.
Mkonge ndio zao kubwa la biashara ambalo linalimwa na kampuni ya MeTL ikiajiri idadi kubwa ya watu kutoka katika kijiji hicho.
1 (11)
Eneo la jengo hilo la kituo linavyoonekana kwa nje.
Ukame uliitafuta Kisangara kwa muda mrefu umesababisha kasi kubwa ya umaskini. Kutokana na hali hiyo watoto wameathirika zaidi kutokana na familia zao kushindwa kuwapeleka shule binafsi  na kuwaacha katika shule za umma ambazo hazina ubora.
Kutokana na hali hiyo FYLC inajipanga kuhakikisha kwamba inarejesha matumaini kwa kuwawezesha wanafunzi hao kupunguza tofauti kati ya wanafunziw aosoma shule binafsi na shule za umma katika masomo.
Kituo kikiwa na wanafunzi 86 wa umri kati ya miaka 13 hadi 14 wanafundishwa kujiandaa kuingia kidtao cha kwanza kwa kufunzwa Fizikia, kemia,bayolojia,jiografia na Kiingereza.
Lengo kuu la kituo ni kuhakikisha kwamba wanawawezesha wanafunzi wanaosoma shule za umma wanakuwa na uwezo mkubwa kwa kuwapa nafasi ya kutumia maktaba na chumba cha Tehama na kuwapelekea walimu waliobobea kuwanoa wanafunzi hao na kuleta mabadiliko.
Aidha kituo kitatoa elimu ya maarifa ya afya ya uzazi kwa vijana ili kuweza kubadili maisha yao na kuondokana na tabia mbaya.
User comments
Ukarabati wa kituo hicho ukianza baada ya Mo Dewji Foundation kukipiga tafu.
20151023_122610
User comments
Mratibu wa Furahini Youth Learning Centre, Isiaka Msuya katika zoezi la kupakia matofali kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho kwa msaada wa Mo Dewji Foundation.
WALIOSAMBAZA MATOKEO YA URAIS KINYUME CHA SHERIA WAPANDISHWA KIZIMBANI MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (katikati), akizungumza na mmoja kati ya vijana nane waliofikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo, kwa tuhuma za kusambaza matokeo ya kura za mgombea nafasi ya urais wa chama hicho katika mitandao ya kijamii kinyume na utaratibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Imedaiwa vijana zaidi ya 190 walikamatwa kwa kosa hilo.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam leo.
Askari wa FFU wakiimarisha ulinzi mahakamani hapo.
Wafuasi wa Chadema wakionesha alama ya vidole viwili wanayoitumia.

Viongozi wa Chadema wakitoka katika mahakama hiyo baada ya kusikiliza kesi hiyo. 


Vijana waliokamatwa wakiwa katika mahakama hiyo.Na Dotto Mwaibale

WATU wanane akiwemo Raia mmoja wa Korea na raia mmoja wa Kenya wamepandishwa kizimbani kwa kusambaza taarifa za matokeo ya urais katika Mtandao wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi yakiwa na kichwa 'M4C election result management system' bila kuthibitishwa kwa lengo la kupotosha umma. 

Sanjari na hilo, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), amewasilisha mahakamani hati ya kuzuia dhamana ya washtakiwa kwa kile alichadai kuwa ni kwa sababu ya usalama na kwa maslahi ya Taifa.

Washtakiwa hao ni Mashinda Mtei (49) mkazi wa Tengeru Arusha, Julius Mwita (40) mwanasiasa na ni mkazi wa Magomeni, Frederick Fussi (25) IT, mkazi wa Mbezi, Julius Matei (45) raia wa Kenya, Meshack Mlawa (25) mchungaji na ni mkazi wa Keko, Anisa Rulanyan (41) Mhandisi, mkazi wa Kawe, Jose Nimi (51) mkazi wa Uingereza na Kim Hyunwook (42) raia wa Korea.

Wakili wa Serikali Mkuu Edwin Kakolaki alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Respicius Mwaijage wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa washtakiwa wanashtakiwa kwa mashtaka matatu.

Ilidaiwa kuwa katika shtaka la kwanza linawakabili washtakiwa wote, ambapo inadawa kati ya Oktoba 25 na 26 mwaka huu, wakiwa katika vituo tofauti tofauti ndani ya jiji la Dar es Salaam walitoa taarifa za uongo kwenye mitandao wakati wakijua hazijadhibitishwa.

Kakolaki alidai washtakiwa hao walisambaza taarifa hizo kwenye mtandao huo na katika mitandao mingine ya kijamii ambayo ni  Facebook na Twitter kutangaza matokeo ya urais ya mwaka huku kwa lengo la kuposha umma huku wakijua hayajadhibitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Katika shtaka la pili linamkabili Matei, Nimi na Hyunwook, ambapo wanashtakiwa kuwa Oktoba 26 mwaka huu wakiwa katika hoteli ya King iliyopo Kinondoni , Dar es Salaam wakiwa na hati za kusafirilia zenye namba A1532119, 930879 na M 27687807 walijiingiza katika ajira ya kukusanya na kusambaza matokeo ya urais ya uchaguzi wa mwaka huu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) bila kibali.

Pia, alidai katika shtaka la tatu lina mkabili Matei peke yake ambaye akiwa raia wa Kenya mwenye hati ya kusafirilia namba A1532119 akiwa ndani ya jiji  la Dar es Salaam alijihusisha na biashara katika Saccos ya Wanama bila kibali.

Baada ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka hayo, walikana kuhusika na tuhuma hizo, ambapo Kakolaki alidai upelelezi bado haujakamilika na pia alidai DPP amewasilisha hati ya kuzuia dhamana kwa sababu ya usalama na maslahi ya Serikali.

Wakili wa washtakiwa hao Peter Kibatala, alidai kuwa mashtaka yanayowakabili wateja wake yanadhaminika, kwa hiyo aliiomba mahakama iwapatie dhamana.

Pia, alidai hati hiyo ya DPP haiko mahakamani hapo kihali na kuiomba Mahakama itupilie mbali hati hiyo kwa sababu haina mashiko kisheria.

Kibatala alidai kuwa hati ya mashtaka iko tofauti na hati ya DPP kutokana na kifungu kilichokuwepo kuwa si sahihi, kwa hiyo kama ni hivyo hati hizo zote hazifai, kutokana na mapungufu hayo.

Baada ya Kibatala kudai hivyo, wakili Kakolaki alidai kuwa hati ya DPP ipo kihalali mahakamani na anayuetakiwa kuthibitisha hilo na mahakama kwa hiyo waiyachie mahakama.

Alidai kuhusu kifungu kilichotumika ni sahihi, akaiomba mahakama itupilie mbali hoja za Kibatala na washtakiwa wanyimwe dhamana kwa mujibu wa sheria, baada ya DPP kuwasilisha hati hiyo.

Hakimu Mwaijage alisema uamuzi wa hoja hizo atazitoa Oktoba 30 mwaka huu na washtakiwa aliamuru warudishwe rumande.

Nje ya mahakama

Washtakiwa hao waliondoka katika eneo hilo la mahakama wakiwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi ambapo wakiwa ndani ya magari ya polisi walikuwa wakionesha alama za vidole viwili.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salim Mwalimu, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sauti, Profesa Mwasiga Baregu na viongozi wengine wa Chadema walijitokeza mahakamani hapo kufuatilia shauri hilo.(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

TACCEO YALAANI KITENDO CHA POLISI KUVAMIA OFISI YAO NA KUWAKAMATA WAANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU
Mmoja wa Wakurugenzi wa Mtandao wa Asasi za Kiraia za Uangalizi wa Chaguzi (TACCEO), Hebron Mwakagenda (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dar es Salaam leo mchana, kuhusu Polisi kudaiwa kufanya uvamizi na kuwakamata waangalizi, vifaa binafsi na vifaa vya Kituo cha Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 katika kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Mbezi jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Imelda Urrio na Kaimu Mkurugenzi wa Utetezi wa LHRC, Anna Henga

Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Imelda Urrio (wa tatu kutoka kushoto), akisisitiza jambo katika mkutano huo. Kutoka kulia na Mwanasheria wa LHRC, Halord Sungusia, Mwakilishi wa Taasisi ya YPC, Maria Kayombo na Mwakiliashi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),Melikizedeck Karol.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.

TACCEO yalaani kukamatwa waangalizi wa uchaguzi


Na Dotto Mwaibale

ASASI za Kiraia za Uangalizi wa Uchaguzi (TACCEO), pamoja na Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), wamelaani kitendo cha kuvamiwa na Jeshi la Polisi, Oktoba 29, mwaka huu na lile la kukamata vitendea kazi na waangalizi wa uchaguzi  36.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo mchana, Kaimu Mwenyekiti wa TACCEO, Hebron Mwakagenda, alisema Jeshi la Polisi lilivamia kituo cha LHRC, kilichopo Mbezi na kudai kuwa, waliagizwa na mamlaka husika kuwakamata waangalizi  na vifaa vya kieletroniki vilivyokuwa vikitumika katika mchakato huo.

Mwakagenda alisema polisi hao waliongozwa na Mkuu wa Upelelezi Wilaya  ya kipolisi Kawe, ASP Mgonja, ambapo  maofisa wa uangalizi walieleza kuwa, walipata taarifa kituo hicho kinakusanya na kunasambaza taarifa za matokeo zisizo rasmi.

"Katika mchakato huo, polisi walikusanya vifaa vyetu na kukamata kompyuta za mezani 24, mpakato tatu na simu za mkononi za waangalizi 25," alisema Mwakagenda.

Alisema baada ya tukio hilo, vifaa hivyo vilichukuliwa na kukabidhiwa kituo cha kati na baadaye kupelekwa makao makuu ya jeshi la polisi huku, baadhi ya waangalizi wakichukuliwa kwa ajili ya kutoa maelezo na baadaye kupata dhamani.

Watu hao wametakiwa kurudi kituoni hapo Oktoba 30, mwaka huu kwa ajili ya kumalizia maelezo yao.

"Mchakato huo la kurudi Oktoba 30, mwaka huu lilifanikiwa na kwa sasa waliambiwa warudi leo, kwa taratibu nyingine za kipolisi," alisema Mwakagenda.

Mwakagenda alisema uvamizi huo uliofanywa na jeshi la polisi ni wa kudhoofisha ustawi wa demokrasia nchini kwani, wasababisha kuwatishia wananchi kushiriki katika mambo yanayohusu mchakato wa chaguzi nchini.

"Katika hili ni kama wameondoa dhana nzima ya ushiriki kikamilifu wa sekta ya umma na binafsi   katika kutoa maoni ya kuboresha demokrasia na uchaguzi," alisema Mwakagenda.

Aidha, Mwakagenda alisema uvamizi huo uliathiri  na kuwafanya wakashindwa kukusanya taarifa za mwisho za uangalizi wa matokeo na ukusanyaji wa maoni ya wananchi.

"Uangalizi kwa kutumia tehama haujaanza mwaka huu kwani, tangu mwaka 2010 kulikuwa na utaratibu huu, mambo yaliyofanyika hivi sasa tunashindwa kuelewa tatizo ni nini," alisema.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Moshi mjini,mfanyabiashara Davis Mosha akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Penfold kwa lengo la kuwashukuru wana CCM waliompigia kura.
Baadhi ya wana CCM waliohudhuria mkutano huo.
Mfanyabiashara Davis Mosha akitangaza uamuzi wake wa kutojihusisha tena na siasa,uamuzi uliosababisha wanaccm kushindwa kujizuia na kuanza kuangua vilio.
Baadhi ya wana CCM wakilia kwa uchungu mara baada ya Davis Mosha kutangaza kutogombea tena Ubunge .
Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro,Michael Mwita alilazimika kwenda kumuomba kubadili uamuzi wake huo.
Vilio havikuwa kwa wanawake peke yao hata wanaume walishindwa kuvumilia.
Wengine walitishia kujinyonga mbele yake.
Uamuzi wa Davis Mosha kuamua kutogombea tena Ubunge unatokana na kile alichodai kuwa baadhi ya viongozi wa CCM kushiriki kumuhujumu katika harakati za kuwania ubunge.
Wengine sura zao zilibadilika zikawa tofauti na zile tulizozizoea.
Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Moshi,Elzabeth Minde aliingilia kati kujaribu kuomba Mosha kubadili uamuzi wake huo bila ya mafanikio.
Wanaccm wengine walilazimika kupanda jukwaani bado walizuiliwa.
Wengine walizimia  na kupatiwa msaada wa huduma ya kwanza.
Mosha aliondolewa uwanjani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi kutokana na wanachi walioonekana kutofurahishwa na uamuzi wake huo.
Msafara wake ulisindikizwa na askari Polisi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.