Wednesday, 16 March 2016

SUBASH PATEL WA M.M.I STEEL AMKABIDHI MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, MABATI YENYE THAMANI YA SH.MILIONI 200 KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE
 Mkurugenzi Mtendaji wa M.M.I Steel, Subash Patel (wa pili kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (wa kwanza kushoto), mabati yenye thamni ya sh.milioni 200 Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa shule mbalimbali jijini Dar es Salaam. Wengine wanaoshuhudia makabidhiano hayo kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa M.M.I Steel, S.K. Modi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Issaya, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymund Mushi na kushoto ni Msaidizi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, 
 Mkurugenzi Mtendaji wa M.M.I Steel, Subash Patel (kulia), akizungumza katika makabidhiano hayo.
Wanahabari na wadau wa maendeleo wakiwa kwenye hafla hiyo ya makabidhiano.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (katikati), akitoa shukurani kwa msaada huo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akizungumuzia changamoto ya madarasa katika wilaya yake.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akitoa shukurani baada ya kupokea msaada huo.
Mwanahabri Renatus Mutabuzi wa Kituo cha Televisheni cha ITV akiwa kazini kuchukua taarifa hiyo.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano.

Na Dotto Mwaibale

UMOJA wa Viwanda vinavyoshughulika na utengenezaji wa vifaa vya ujenzi nchini umemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mabati yenye thamani ya sh.milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi msaada huo Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa M.M.I Steel, Subash Patel alisema waliguswa mno na changamoto hiyo inayowakabili wanafunzi ndio maana akawaomba wenzake wasaidie.

"Kampuni yangu imetoa vifaa vyenye thamani ya sh. milioni 100 na Kampuni ya Ujenzi ya Estim imetoa sh.milioni 50 wakati Export Trading imetoa sh. milioni 50" alisema Patel.

Patel alitumia fursa hiyo kuyaomba makampuni mengine kujitoa kusaidia shughuli za maendeleo nchini hasa katika sekta ya elimu yenye changamoto za uhaba wa madarasa na madawati.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadik amesema kumekuwa na changamoto kubwa ya vyumba vya madarasa jijini Dar es Salaam hasa katika Wilaya ya Temeke na Ilala ambapo katika shule moja kuna zaidi ya wanafunzi kuanzia 3000 hadi 5000.

Sadiki alisema msaada huo utasaidia kupunguza changamoto hiyo katika jiji la Dar es Salaam.

Hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo ilihudhuriwa na Wakuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema,  Ilala, Raymond Mushi na Mkurugenzi wake.

Tuesday, 15 March 2016

DC MAKONDA, GSM FOUNDATION WAZINDUA UJENZI WA JENGO LA UPASUAJI HOSPITALI YA RUFAA YA MWANANYAMALA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), ambaye mchana huu Rais Dk.John Magufuli amemteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa jengo la upasuaji katika Hospitali ya Mwananyamala Dar es Salaam leo, ambalo litakuwa maalumu kwa ajili ya utoaji wa huduma za upasuaji kwa wajawazito na wagonjwa wengine wadharura. Kutoka kulia ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Azizi Msuya, Mwakilishi wa Kampuni ya GSM, Deogratias Ndejembi ambao watajenga jengo hilo na kushoto ni Mhandisi, Hersi Said kutoka GSM ambaye atasimamia ujenzi wa jengo hilo.
 Ukataji utepe ukiendelea.
 DC Makonda akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa ujenzi huo.
 DC Makonda akiwa na viongozi wa Kampuni ya GSM Foundation. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Azizi Msuya.
 DC Makonda akizungumza na wanahabari kuhusu ujenzi huo.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Azizi Msuya akizungumza na wanahabari.
 Wanahabari wakichukua taarifa za ujenzi huo.
 Mwakilishi wa Kampuni ya GSM Foundation, Deogratias Ndejembi akizungumza na wanahabari kuhusu ufadhili wao wa ujenzi wa jengo hilo.
 Msingi wa jengo hilo.
  Mwakilishi wa Kampuni ya GSM Foundation, Deogratias Ndejembi (katikati), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda na Mhandisi atakaye simamia ujenzi huo kutoka GSM, Hersi Said wakionesha picha ya jengo hilo litakavyoonekana  baada ya kukamilika.
Taswira ya jiwe la msingi baada ya kuzinduliwa.DC Makonda akiwa na viongozi wa Kampuni ya GSM mbele ya msingi litakapo jengwa jengo hilo.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amezindua ujenzi wa jengo la upasuaji katika Hospitali ya Mwananyamala ambalo litakuwa maalumu kwa ajili ya utoaji wa huduma za upasuaji kwa wajawazito na wagonjwa wengine wadharura.

Jengo hilo ambalo ujenzi wake utaanza rasmi kesho, litakuwa na vyumba maalumu kwa ajili ya upasuaji, uangalizi maalumu kwa ajili ya wagonjwa wadharura (ICU) na uangalizi baada ya upasuaji na vingine kwa ajili ya utawala na huduma nyinginezo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Dar es Salaam leo mchana  DC Makonda alisema kuwa jengo hilo litakuwa mahususi kwa ajili ya kupunguza idadi ya wagonjwa ambao wanahitaji kufanyiwa upasuaji kwenda Hospitali yaTaifa ya Rufaa yaMuhimbili.

“Kupitia jengo hili wajawazito wote na wagonjwa wengine ambao wanahitaji upasuaji watapatiwa huduma hiyo hapa hapa Mwananyamala. 

Alisema jengo hilo litakuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa wagonjwa 350-360 hivyo kwa kiasi kikubwa tutakuwa tumepunguza msongamano Muhimbili. 

Pia utakuwa tumefanikiwa kuokoa maisha ya wajawazito ambayo yameku wa yakipotea kutokana na kuchelewa kupata tiba,” alisemaMakonda.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa yaKinondoni, Dk. Azizi Msuya alisema jengo hilo litasaidia  kuokoa maisha ya wajawazito na wagonjwa wengine ambao  wamekuwa wakifariki kutokana na kucheleweshewa kupata huduma hizo.

“Katika wajawazito 100,000 wanaojifungua, 447 wanapoteza maisha. Sasa kupitia uwepo wa huduma ya upasuaji katika hospitali hii ya Mwananyamala tutajitahidi kwa kadri ya uwezo wetu kuokoa maisha  ya wajawazito hao wanaofariki” alisemaDkAzizi.

Mwakilishi wa Kampuni ya GSM Foundation ambao ndiyo wafadhili wa ujenzi wa jengo hilo, Deogratias Ndejembi  alisema kuwa kampuni  hiyo imeamua kufadhili ujenzi huo ili kuokoa maisha ya watanzania ambao wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa huduma ya upasuaji na pia kutokana nakuguswa na juhudi za DC Makonda.

“Kama GSM tumeamua kugharamia ujenzi wa jengo hili la upasuaji ili kuokoa maisha ya wanawake, watoto  na jamii nyingine ambayo imekuwa ikipoteza maisha kwa kukosa upasuaji. Pia juhudi na uchapaji kazi wa DC Makonda. 

Amekuwaakifanyakazikwajuhudikubwa, hivyo tukaona ni vyema tuka muunga mkono” alisema Deogratias Ndejembi.Friday, 19 February 2016

KITUO CHA MABASI MASASI SASA SAFI, WAHUSIKA WAAMKA BAADA YA KUMULIKWA (+VIDEO)
Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo Mikoani Wilayani Masasi yaendelea Kuboreshwa kwa kufanyiwa Usafi wa Hali yajuu.

Leo hii Baada ya Kamera ya Lindiyetu.com kupita majira ya asubuhi ilikuta eneo hilo ambalo hapo jana lilikuwa limetapakaa Uchafu wa Kila aina likiwa Safi Kabisa.

KAMA ULIPITWA NA POST HIYO BOFYA HAPA KUANGALIA UCHAFU ULIOKUWEPO Hii inaonesha kabisa Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Masasi amedhamiria kuepuka aibu ambayo ilikuwa inakuja siku za usoni kwani eneo hilo lipo katikati ya Mji huo hivyo kuonekana kirahisi na Kuleta Picha mbaya.


Tunaipongeza Halmashauri ya Mji ambayo imelichukua jambo hili kwa Umakini mkubwa hadi kufikia Kuweka Greda ambalo lilikutwa likifanya kazi ya kuendelea kuweka Mazingira sawia katika Stend kuu hiyo.

UNAWEZA BOFYA PLAY KUTAZAMA VIDEO HAPO CHINI
HONGERENI SANA...!!!

Thursday, 18 February 2016

JUKWAA LA BIOTEKNOLOJIA LATOA MAFUNZO KWA WALIMU WANAFUNZI WA CHUO CHA BUNDA KUHUSU BIOTEKNOLOJIA
Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania na Mkufunzi wa Mafunzo ya Bioteknolojia , Dk.Emmarold Mneney (kulia), akiwafundisha wanachuo wa Chuo cha Ualimu cha Bunda (BUNDA TTC), kuhusu matumizi ya bioteknolojia na uhandisi jeni Wilaya ya Bunda mkoani Mara leo asubuhi.
Mtafiti Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akizungumza na wanachuo hao katika mafunzo hayo.
Wanachuo hao wakifuatilia mafunzo hayo. 


Mtafiti Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho, Rweyemamu wakiwa katika mafunzo hayo.
Walimu wa chuo hicho wakifuatilia mafunzo hayo.
Wanafunzi wakiwa katika mafunzo

Wanachuo hao wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo
Mwanachuo, Noshad Bryson akiuliza swali katika mafunzo hayo.
Mwanachuo, Mahana Mahana akiuliza swali.
Mwanachuo, Elias Yohana akiuliza swali.
Hapa baada ya mafunzo ni msosi kwa kwenda mbele.

Na Dotto Mwaibale

JUKWAA la Bioteknolojia Tanzania limetoa mafunzo ya matumizi ya bioteknolojia na Uhandisi Jeni kwa wanachuo cha ualimu Bunda kilichopo mkoani Mara ili kuwa jengea uwezo wa kuielewa teknolojia ya bioteknolojia  kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na changamoto za kilimo.

Akizungumza na wanafunzi hao jana Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Dk. Emmalord Mneney alisema kuwa teknolojia hiyo mpya ni muhimu kusambaa nchini ili kumkomboa mkulima.

"Tumeamua kuleta mafunzo haya kwa wanachuo hiki tukiamini kuwa baada ya kuhitimu mafunzo yao watakwenda kuwaelimisha wakulima katika maeneo yao"alisema Dk. Mneney.


Dk.mneney aliongeza kuwa kutokana na kuwepo kwa changamoto ya tabianchi kumesababisha ukame na uharibifu wa mazingira ambayo yameathiri shughuli za kilimo hasa mazao.

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo serikali imekuwa ikiiwezesha Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) kwa ajili ya kuwaongezea uwezo wa kufanya tafiti za kilimo nchini.

Dk.Mneney alisema kuwa changamoto kubwa ya wakulima ni kukosa mbegu bora za mazao ya pamba na mahindi hali iliyosababisha wakulima wengi kukata tamaa ya kilimo hicho na kuamua kulima mazao mengine.

"Kutokana na changamoto hiyo Costech imekuwa ikifanya utafiti ndani ya maabara ya kisasa iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam ili kupata mbegu bora ambazo zikionekana kuwa zinafaa zitasambazwa katika mashamaba makubwa na nchi nzima kwa ujumla" alisema Dk.Mneney.


Mwanachuo hicho Mahana Mahana alisema mkoa wa Mara unachangamoto kubwa ya kilimo kutokana na ardhi kuchoka hivyo ni wakati wa watafiti kuliangalia hilo ili kuwasaidia wakulima kupata mbegu bora zitakazo waletea mafanikio ya kilimo ya kupata mazao mengi.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Dar es Salaam, Februari 17, 2016 - Fastjet imepunguza mtiririko wa safari zake  kwenye njia ya Kilimanjaro Tanzania na Nairobi Kenya kuanzia Jumatatu Februari 15, 2016.
Fastjet ambao awali walikuwa wanatoa safari za kila siku kwenye njia hii hivi sasa watakuwa wanafanya  safari kutoka Uwanja Ndege wa  Kimataifa wa Jomo Kenyatta hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mara mbili kwa wiki  siku za Ijumaa na Jumapili tu.
Mabadiliko ya  mtiririko wa safari utazifanya ndege za fastjet kuondoka Nairobi kila Ijumaa na Jumapili saa 5.40 na kutua Kilimanajaro saa 6.40 na safari ya kurudi ndege itaondoka Kilimanjaro saa 7.10 na kutua Nairobi saa 8.10.

Kupunguzwa kwa safari hizo kumetokana na kuwepo kwa mahitaji kidogo miongoni mwa wateja nyakati za wiki kutoka masoko yote mawili ya Kilimanjaro na Nairobi na hivyo kufanya safari za ndege za kila siku kutokuwa nzuri kibiashara  kwenye siku hizo.
Shirika hilo limesema kuwa lengo lake ni kurejesha safari hizo kwenye njia ya Kilimanjaro –Nairobi pindi tu wateja wake watakapohitaji.


Safari za kila siku za  kutoka Dar es Salaam na Kilimanjaro hadi Nairobi zilianza Januari 11, 2016.
Mahitaji ya abiria kwa safari za ndege kwenye njia kubwa ya kibiashara kati ya majiji ya Dar es Salaam na Nairobi   ambayo kwa pamoja  yana idadi ya watu zaidi ya milioni nane yamekuwa ni ya kuridhisha na fastjet iko kwenye mawazo kuwa  ndege moja ni lazima iongezeke kwenye safari kati ya majiji haya miwili katika siku za usoni.

Matokeo ya safari za fastjet kwenda Nairobi kutoka Dar es Salaam yamekuwa ni makubwa ambako kunaelezwa na ukweli kuwa nauli zinazotolewa na mashirika ya ushindani kati ya  nchi hizo mbili zimeshuka kwa  kiwango cha hadi asilimia 40 tangu fastjet waanze safari zake.
Nauli za fastjet kwa kiwango kikubwa zipo chini kuliko zile zinazotozwa na mashirika mengine  kwa safari za moja kwa moja kati ya Nairobi/Dar es Salaam  ambapo nauli zinaanzia dola 80 kwa safari moja.

Nauli hizo hazijumuishi kodi ya serikali ambayo ni dola 49 kuondokea Tanzania na dola 40 kuondokea Kenya na hivyo fastjet kupendekeza wateja wake kufanya maandalizi mapema ili kutumia fursa hiyo ya tozo la nauli nafuu.Hata hivyo fastjet inasisitiza kuwa  kupunguza safari kwenye njia kati ya Nairobi na Kilimanjaro kunafungua fursa ya kuongeza uwezo kwenye njia za kikanda zilizopo na hali kadhalika uwezekano wa kuzindua  njia nyingine mpya ya kikanda katika siku za karibuni.

Wednesday, 17 February 2016

AU Commission urges African governments to use commodity downturn to strengthen their laws and institutions

Cape Town, South Africa, 7 February 2016 (ECA) – A keynote speech delivered on behalf of Her Excellency Mrs Fatima Acyl, African Union Commissioner for Trade and Industry at Cape Town’s annual Mining Indaba acknowledged the reality of the commodity price slump, but also identified the opportunity for African governments to create the right legal and institutional framework to drive change in their economies.

“Now that the boom is over, it is even more imperative for all stakeholders to get down to the hard work of implementing the development agenda embodied in the African Mining Vision, for sustainable structural transformation of African economies,” urged Her Excellency in the speech.

Stressing that the Africa Mining Vision (AMV) went well beyond simply questions of taxes and revenue collection, the Commissioner’s speech stressed mining’s role in linkages and infrastructure development.

“A typical mining company spends over 61 percent of its total investment on infrastructure and procurement – more than three times what is paid in taxes,” noted the Commissioner’s speech. “Investment through linkages presents opportunities for governments to align their development policies in ways that capture greater value from mining,”

The speech was delivered at the annual Ministerial Symposium, held the Sunday before Mining Indaba commences. The Symposium provides a platform for ministers responsible for mineral resources to discuss common risks and opportunities associated with the implementation of the Africa Mining Vision. 
CODES NA LINK: LINK: https://soundcloud.com/issamichuzi/balozi-ombeni-sefue-siku-100-za-rais-magufuli-feb-122016

Mkuu wa  Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano wa TigoDavid Zakaria akielezea athari  za matumizi ya  simu bandia kwa waandishi wa habari  (Hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika mapema leo katika makao makuu ya Tigo Kijitonyama Dar es salaam., kushoto kwake ni Meneja wa Mawasiliano, John Wanyancha


Dar es Salaam, Februari 16 2016 - Watumiaji wa simu za mkononi wameonywa dhidi ya matumizi ya simu bandia na zisisokidhi viwango vya ubora ambazo tayari zimetangwa kupigwa marufuku na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Kutokana na sababu hiyo, Tigo, ambayo ni kampuni ya kidijitali, imeanza kuendesha kampeni ya kuhamasisisha wateja wake na umma kwa jumla kupitia vyombo vya Habari inayolenga kuwaepusha na athari za matumizi ya simu bandia.

 ``Kwa mujibu wa maelekezo ya TCRA matumizi ya simu za mkononi ambazo namba zake za utambulisho wa kimataifa (IMEI) ni bandia yatapigwa marufuku kutumika kwa mitandao yote ya simu nchini Tanzania kuanzia Juni 16 mwaka huu. Ili kujiepusha na usumbufu wowote utakaotokana na hatua hii tunawashauri wateja wetu kujipatia simu halisi na bora kutoka maduka ya Tigo yaliyo karibu nao,`` alisema Mkuu wa  Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano wa Tigo, David Zakaria.
Ripoti ya utafiti ulichapishwa katika tovuti ya GSMA ("http://www.gsma.com" www.gsma.com ) inasema kwamba tofauti na ilivyo kwa simu halali ambazo hupitia mamia ya hatua mbalimbali za kuhakiki ubora wake kabla ya kupelekwa sokoni, simu bandia hazifanyiwi majarbio ya ubora na kuna taarifa za kitafiti zinazoonyesha kuwa baadhi ya simu bandia zina kiwango kikubwa cha madini ya risasi na vitu vingine ambavyo ni hatari kwa mazingira na afya ya binadamu.
Ripoti hiyo inaendelea kusema kuwa simu feki zinatengenezwa na malighafi dhaifu zisizokidhi viwango na zimeshaonesha kuwa kiwango cha hatari cha vyuma na kemikali kama risasi hadi kufikia kiwango cha mara 40 zaidi kuliko kiwango kilichoidhinishwa na sekta ya mawasiliano duniani kwa mujibu wa na Jukwaa la Watengenezaji wa Simu za Mkononi (MMF).
Akizungumza kuhusu hatua ya Tigo kutoa tahadhari kwa wateja wake Zakaria alisema, ``Wanunuzi wanatakiwa kuwa waangalifu wakati wanaponunua simu mpya au vifaa vya mawasiliano madukani au katika intaneti kwa sababu bidhaa nyingi feki zinatengenezwa kwa kuigaa muundo na nembo za kibiashara za bidhaa halisi kwa makusudi ili kuwalaghai wateja.
``Ili kuweza kuelewa iwapo simu yako ni feki au ni halisi unatakiwa kupiga namba namba *#06# ambapo atapokea  namba ya IMEI ya simu hiyo na kisha kutima kwa njia ya jumbe mfupi kwenda namba 15090 ambapo utapata jibu iwapo simu hiyo ya mkononi ni halisi au ni bandia,” alisema Zacharia. Mwisho 
Mkuu wa  Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano wa TigoDavid Zakaria akielezea athari  za matumizi ya  simu bandia kwa waandishi wa habari  (Hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika mapema leo katika makao makuu ya Tigo Kijitonyama Dar es salaam., kushoto kwake ni Meneja wa Mawasiliano, John Wanyancha


Dar es Salaam, Februari 16 2016 - Watumiaji wa simu za mkononi wameonywa dhidi ya matumizi ya simu bandia na zisisokidhi viwango vya ubora ambazo tayari zimetangwa kupigwa marufuku na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Kutokana na sababu hiyo, Tigo, ambayo ni kampuni ya kidijitali, imeanza kuendesha kampeni ya kuhamasisisha wateja wake na umma kwa jumla kupitia vyombo vya Habari inayolenga kuwaepusha na athari za matumizi ya simu bandia.

 ``Kwa mujibu wa maelekezo ya TCRA matumizi ya simu za mkononi ambazo namba zake za utambulisho wa kimataifa (IMEI) ni bandia yatapigwa marufuku kutumika kwa mitandao yote ya simu nchini Tanzania kuanzia Juni 16 mwaka huu. Ili kujiepusha na usumbufu wowote utakaotokana na hatua hii tunawashauri wateja wetu kujipatia simu halisi na bora kutoka maduka ya Tigo yaliyo karibu nao,`` alisema Mkuu wa  Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano wa Tigo, David Zakaria.
Ripoti ya utafiti ulichapishwa katika tovuti ya GSMA ("http://www.gsma.com" www.gsma.com ) inasema kwamba tofauti na ilivyo kwa simu halali ambazo hupitia mamia ya hatua mbalimbali za kuhakiki ubora wake kabla ya kupelekwa sokoni, simu bandia hazifanyiwi majarbio ya ubora na kuna taarifa za kitafiti zinazoonyesha kuwa baadhi ya simu bandia zina kiwango kikubwa cha madini ya risasi na vitu vingine ambavyo ni hatari kwa mazingira na afya ya binadamu.
Ripoti hiyo inaendelea kusema kuwa simu feki zinatengenezwa na malighafi dhaifu zisizokidhi viwango na zimeshaonesha kuwa kiwango cha hatari cha vyuma na kemikali kama risasi hadi kufikia kiwango cha mara 40 zaidi kuliko kiwango kilichoidhinishwa na sekta ya mawasiliano duniani kwa mujibu wa na Jukwaa la Watengenezaji wa Simu za Mkononi (MMF).
Akizungumza kuhusu hatua ya Tigo kutoa tahadhari kwa wateja wake Zakaria alisema, ``Wanunuzi wanatakiwa kuwa waangalifu wakati wanaponunua simu mpya au vifaa vya mawasiliano madukani au katika intaneti kwa sababu bidhaa nyingi feki zinatengenezwa kwa kuigaa muundo na nembo za kibiashara za bidhaa halisi kwa makusudi ili kuwalaghai wateja.
``Ili kuweza kuelewa iwapo simu yako ni feki au ni halisi unatakiwa kupiga namba namba *#06# ambapo atapokea  namba ya IMEI ya simu hiyo na kisha kutima kwa njia ya jumbe mfupi kwenda namba 15090 ambapo utapata jibu iwapo simu hiyo ya mkononi ni halisi au ni bandia,” alisema Zacharia. Mwisho 

Tuesday, 16 February 2016

Mabalozi wa Huawei wakipozi siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Balozi wa Huawei akikabidhi zawadi kwa mteja siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Balozi wa Huawei akikabidhi zawadi kwa mteja siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Baadhi ya wateja wakipata picha ya ukumbusho na balozi wa Huawei siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Balozi wa Huawei akikabidhi zawadi kwa wateja siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Bw. Sylvester Manyara, Meneja Mwandamizi  Huawei Tanzania(Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wateja walioshiriki katika uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania.
Bw. Sylvester Manyara, Meneja Mwandamizi  Huawei Tanzania(Kushoto) akimkabidhi Mteja mfuko wa zawadi pamoja na kadi katika uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3   inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki hii, Mlimani City Dar es Salaam.

Baadhi ya wateja wakipata maelezo kutoka kwa mabalozi wa Huawei siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam. 

Na Mwandishi wetu, 
Kampuni ya simu ya Huawei, inayoshika nafasi ya tatu kwa utengenezaji na uuzaji wa simu za mkononi ulimwenguni imezindua promosheni ya Valentine ya muda wa wiki 3 inayohusisha vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na utoaji zawadi kwa wanunuzi wa simu za Huawei kutoka kwenye maduka yao mbalimbali ya rejareja yaliyosajiliwa.
Promotion hiyo itahusisha simu kuu mbili ambazo ni Huawei P8 na Huawei G8. Zawadi zinazotolewa kwa wateja ni pamoja na “selfie sticks, spika za Bluetooth na T-shirts. Pamoja na zawadi zote hizo ,wateja hao pia wanapewa fursa ya kupata picha nzuri za kumbukumbu ili waweze kuzitumia kwenye mitandao ya kijamii kama instagram na mingine.
Kampeni hii Iliyozinduliwa wikiendi hii mjini Dar es Salaam eneo la  Mlimani City, inawaahidi wateja wa Huawei kuona thamani ya pesa yao kutokana na zawadi watakazopatiwa .
Kwa mujibu wa report ya simu za mkononi ya hivi karibuni nchini Tanzania ilivyochapishwa mwaka jana na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), idadi ya watanzania wanaotumia simu za mkononi, waliojisajili imeongezeka kwa asilimia 16 kwa mwaka 2014 kufikia milioni 31.86 hiyo ni sawa na asilimia 67 kwa watanzania wote wanaotumia simu.
Huawei Tanzania wanaahidi kuendelea kutatua uhitaji wa wateja wao kwa kuwapatia   simu zenye ubora wa hali ya juu na orijino.
Tunatarajia kutoa huduma bora ya mawasiliano na intanet kwa bei nafuu kwa wananchi na pia kuwazawadia wateja wetu wale wazamani na wapya,  vifaa bora na vya kisasa vitakavyoweza kuongeza wigo katika matumizi ya simu zao za smatiphone  na intaneti pia” alisema Bw. Peter Zhangjunliang, Meneja wa Huawei nchini Tanzania katika uzinduzi wa Promotion hiyo.
Akielezea promosheni hiyo, Bw. Peter Zhangjunliang alisema; promosheni hii ya wiki 3 ni ya nchi nzima na ipo wazi kwa watanzania wote watakao nunua simu za G8 na P8 kutoka Huawei.”

Huawei, rafiki yako kwa simu origino.

Kuhusu Huawei
Kampuni ya Huawei imejizatiti katika kutengeneza bidhaa bora kwa matoleo tofauti ulimwenguni, kutoa huduma rafiki za simu, kwenye intaneti kwa wateja wake. Kampuni ya Huawei inajulikana duniani katika utengenezaji wa simu za mkononi, huduma za intaneti na vifaa vya majumbani.
Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2015, bidhaa vya Kampuni ya Huawei zinapatikana  zaidi ya nchi 150 ulimwenguni kote. Huawei ni kampuni ya 3 katika usambazaji wa simu (2015) ikiwa imesambaza zaidi ya milioni 100 ulimwenguni. Kampuni ya Huawei imeanzisha ushirikiano  na makampuni makubwa duniani kama Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel, Sasatel, TTCL, SmileCom, Safaricom, MTN, CellC, Telefónica, China Mobile, Vodafone, T-Mobile, BT, China Telecom, NTT Docomo, France Telecom, na China Unicom. 
Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea www.huaweidevice.com