Monday, 5 August 2013

Wakulima wa Kenya, wanasiasa wapambana na marufuku ya Uingereza dhidi ya mirungi

Na Julius Kithuure, Nairobi

Wanasiasa, wakulima na wasafirishaji wa Kenya wanatoa wito kwa serikali kuanza mazungumzo ya haraka na Uingereza kuhusu marufuku inayokuja juu ya mirungi, au miraa, mmea ambao unatoa athari za kuchangamsha yanapotafunwa.

Mkulima wa Kenya, Mzee Isai akionesha rundo la mirungi lililokatwa kutoka mti wake wenye umri wa miaka 300 katika Jimbo la Meru. [Na Simon Maina/AFP]

Marufuku ya Uingereza inaweza kusababisha kuporomoka kwa sekta ya kilimo cha mirungi cha mamilioni mengi, watetezi wasema.

Hapo tarehe 3 Julai, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza Theresa May alitangaza kwamba nchi yake inapanga kupiga marufuku mirungi, licha ya maombi kutoka kwa Baraza la ushauri la Uingereza la matumizi Mabaya ya Madawa kuwa mmea huo usipigwe marufuku, kwa kusema kuwa hauna uhusiano na uhalifu mkubwa wa kupangwa.

Hata hivyo, May alisema kuwa sababu kuu za serikali yake kuamua kuupiga marufuku zilikuwa za kisiasa, kama ilivyo nchi nyingi za Ulaya, pamoja na Marekani na Canada ambazo zimeupiga marufuku mmea huo.

Mwanamume wa Kisomali akitafuna mirungi huko Uithoorn, Uholanzi, tarehe 12 Januari, 2012. Serikali ya Uholanzi hapo tarehe 10 Januari ilipiga marufuku majani hayo yanayochamsha, yanayotumiwa zaidi na watu kutoka Somalia, Ethiopia, Kenya na Yemen. [Na Koen Van Weel/ANP/AFP]

"Kukosa kuchukua hatua za maamuzi na kubadilisha msimamo wa kisheria wa Uingereza kuhusu mirungi utaiweka Uingereza katika hali mbaya ya kuwa nchi pekee, kitovu cha kanda cha kupatikana na biashara isiyo halali ya mirungi," alisema katika taarifa bungeni. 


"Kukamata mirungi inayopitia Uingereza ikiwa njiani kuelekea Uholanzi tayari kumeongezeka kiwango na mara nyingi tangu pale Uholanzi ulipoipiga marufuku mapema mwaka huu."

Licha ya ukosefu wa uwezo wa baraza la la ushauri kutoa ushahidi wa mwisho wa athari zinazodaiwa za mirungi, May alisema kuwa ina madhara kwa jamii.

"Mirungi inaendelea kuwa kipengele maarufu miongoni mwa madhara ya kiafya na kijamii, kama vile kiwango cha chini na kuvunjika kwa familia, kama ilivyotajwa na jamii zilizoathirika na polisi na viongozi wa maeneo wanaofanyakazi pamoja nao," alisema, akiongeza kuwa kumilki mirungi kunapaswa kuchukuliwa kwa namna ile ile kama kumiliki bangi, na maonyo na faini kabla ya kukamatwa.

Mirungi na uchumi wa Kenya
Kupiga marufuku mirungi Uingereza kunaweza kuwa na athari hasi kwa uchumi wa Kenya, wabunge wa Meru na na wafanyabiashara waonya.

Sekta ya kilimo cha mirungi inaajiri zaidi ya wakulima na wafanyabiashara 500,000, kwa mujibu wa Utafiti wa Kiuchumi wa Kenya uliotayarishwa mwaka 2012 na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS). Mirungi ni bidhaa ya nne ya Kenya ya usafirishaji katika vipengele vya ujazo, kwa thamani ya karibu shilingi bilioni 16.5 (dola milioni 189), kwa mujibu wa data za KNBS.

Wabunge na viongozi wa biashara ambao wanawakilisha mikoa ambako mirungi inalimwa wamekosoa kile walichokisema kuwa ni kusita kwa serikali kutetea kuifanya mirungi kua ni zao la fedha badala ya dawa.

"Kitu pekee tunachotaka ni kwa serikali yetu kuanzisha mazungumzo na serikali ya Uingereza ili waweze kuzuia marufuku juu ya mirungi, ambayo ni [chanzo] cha kujipatia riziki kwa watu wa Meru na Kenya kwa jumla," alisema Kimanthi Munjuri, mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Miraa wa Nyambene.

Kabla ya Uholanzi kupiga marufuku mirungi hapo mwezi Januari, Uingereza ilikuwa soko la pili la miraa kimataifa kwa ukubwa, linaloagiza tani 20 hadi 25 kwa wiki za mirungi iliyolimwa Kenya. Sasa, Uingereza inawakilisha muagizaji mkubwa zaidi, ikichukua tani 30 za mirungi kutoka Kenya, Munjuri aliiambia Sabahi.

Nchini Uingereza, watumiaji wakubwa wa mirungi ni wahamiaji kutoka Somalia, Kenya, Ethiopia na Yemeni.

Kipkorir Menjo, mkurugenzi wa Jumuiya ya Wakulima wa Kenya, alisema kuwa serikali za Uingereza na Kenya zinahitaji kufahamu athari za marufuku ya mirungi.

"Maelfu ya wakulima, wafanyabiashara, wasambazaji na wasafirishaji watabaki hawana kazi na hii sio habari njzuri wakati serikali ya Jubilee inakabiliwa na ukosefu wa ajira," aliiambia Sabahi. "Sekta yote inaelekea kuporomoka kwa sababu Uingereza ni soko kuu ambalo limekuwa likiwaleta watu wetu mapato makubwa, na wakati huo huo kuipa nchi fedha zakigeni zinazohitajika sana."

Wabunge wa Kenya wazishinikiza Uingereza, Kenya kupitia upya marufuku
Gavana wa Kaunti ya Meru, Peter Munya, na Seneta Kiraitu Murungi wameapa kuwaongoza wanasiasa kupiga kampeni kwa serikali ya Uingereza kuipitia upya marufuku hiyo.

"Mirungi inasaidia mamilioni ya maisha nchini Kenya," Murungi aliiambia Sabahi. Alisema alikuwa anajitayarisha kuishawishi serikali ya Uingereza kupambana na marufuku ya mirungi. "Pia ninapanga ujumbe wa kumuona Rais [Uhuru][ Kenyatta juu ya suala hilo hilo hivi karibuni."

Tarehe 25 Julai, Munya na Murungi waliwasilisha ombi la malalamiko kwenye Balozi wa Uingereza nchini Kenya, Christian Turner, wakiomba kuondolewa kwa marufuku na kuanzishwa kwa majadiliano juu ya vipi kuimarisha usalama katika matumizi ya mirungi.

Wanasiasa wa Kaunti ya Meru pia wanatishia kuhamasisha wakulima wa mirungi na serikali kushinikiza kufungwa kwa vituo vya mafunzo ya kijeshi vya Uingereza na mashamba yanayomilikiwa na Uingereza, pamoja na kugomea bidhaa zinazoingizwa nchini kutoka Uingereza.

"Hata hivyo, nina matumaini kuwa haitafikia hatua hiyo," alisema Florence Kajuju, mwakilishi wa wanawake kwa kaunti ya Meru katika Bunge la Taifa. "Tuna imani kwamba bunge la Uingereza [halitashikilia marufuku hiyo] wakati muda utakapowadia. Pia tuna matumaini kwamba rais wetu ataingilia kati kwa kutuma ujumbe wa biashara kukutana [na] maofisa wa serikali ya Uingereza."

Watunga sheria pia waliilalamikia serikali ya Kenya kubadilisha msimamo wake kuhusu mirungi, kwani Mamalaka ya Taifa ya Kampeni Dhidi ya Matumizi ya Dawa za Kulevya (NACADA) imeorodhesha mirungi kama dawa za kulevya.

Tarehe 29 Julai, Mtandao wa Kidunia wa Wahusika wa Kiwanda cha Miraa na wanasiasa wa eneo la Meru walifungua kesi katika mahakama kushtaki NACADA. Mlalamikiwa anataka mirungi kuainishwa kama zao na kwa watunga sheria kupitisha sheria inayotaka wizara ya kilimo kuitetea.

Jambo lililotia maudhi na serikali ya shirikisho walikataa kuingilia kati, watunga sheria wameunda kamati ya wajumbe 29 kuchunguza athari za kiafya za mirungi na matokeo yake kiuchumi katika Meru mahali ambapo kiburudisho hicho kinalimwa.

"Tutachunguza masuala yote yanayohusiana na mirungi kwa kina," Kajuju aliiambia Sabahi. "Hatutaacha kitu bila kushughulikiwa na ninaahidi kwamba tutazingatia na kupitia tena matokeo ya tafiti zote na kutoa mapendekezo bungeni ndani ya kipindi cha siku 90."

Biashara ya mirungi yaleta changamoto ya usalama

Wachambuzi wa masuala ya usalama na waangalizi wanasema jambo muhimu na linaloleta hofu liko katika mjadala kuhusu mirungi -- biashara yake inazalisha kiasi kikubwa cha fedha kisichohesabika.

Kiasi hicho hakipitii katika mfumo wowote halali wa kibenki na kutoa mianya ya uwezekano wa kupatikana fedha za ugaidi na wenye siasa kali katika Pembe ya Afrika, alisema Paul M. Taiti, mchambuzi mwandamizi katika Kituo cha Taarifa za Usalama Nairobi.

Matumizi makubwa ya mirungi kwa wanamgambo kama al-Shabaab nchini Somalia na al-Qaeda nchini Yemen yameleta kichochezi cha sifa mbaya sana, aliiambia Sabahi.

"Wakati wote kuna shaka ambalo bado halijathibitishwa inayounganisha mamilioni ya dola zinazoongezeka kutokana na biashara ya miraa kugharimia mitandao ya ugaidi katika Pembe ya Afrika na kaskazini-magharibi mwa Afrika," Taiti alisema. "Hii ndiyo maana Umoja wa Ulaya na Uingereza wana wasiwasi na biashara nzima ya mirungi."

Chanzo - sabahionline.com