Wednesday, 21 August 2013

DIAMOND AFUNGUKA KUHUSU SKENDO YAKE YA MADAWA YA KULEVYA


 
Msanii Wa Muziki wa Bongofleva mwenye jina kubwa Town na mwenye Mkwanja mkubwa hapa nchini Nasseeb Abdulmaliki “Diamond” amejitokeza na kukanusha kuwa hahusiki na biashara ya madawa ya kulevya.
Ni kwa muda mrefu sasa kumekuwa na taarifa za Diamond kujihusisha na biashara hiyo hasa kutokana na ukaribu wake na wfanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya wenye maskani yao nchini Afrika Kusini. Taarifa zaidi zinasema ni wafanyabiashara hao waliohusika kwa karibu kuusafirisha mwili wa marehemu Albert Mangwair, aliyefia huko huko Afrika Kusini ambaye taarifa za kifo chake ziligubikwa na matumizi ya madawa ya kulevya.

Akikanusha taarifa hizo Diamond alisema “ni kweli mimi nina pesa za kutosha kuniwezesha kuishi maisha ninayotaka lakini sijawahi kujihusisha na biashara hiyo. Kufanya kazi kwa bidii kunalipa na kazi yangu inaonekana na ndiyo inayoniwezesha kuwa na fedha ambazo leo watu wameanza kuzitilia shaka. Sielewi nia ya watu hawa ni nini?”

Taarifa za Diamond kuhusishwa na mtandao huu zimeanza kushika kasi kufuatia miongoni mwa watu wake wa karibu kuonekana wakiwa karibu sana na akina Agnes Gerald “Masogange” (25) na Melisa Edward (24) kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere wa Dar es Salaam kabla hawajapanda ndege kuelekea Afrika Kusini ambako walikamatwa.

Source; 24Hours Mix