Thursday, 29 August 2013

                  BREAKING  NEWS!!!
AMBOKILE WETU  WA LONDON  ATEULIWA KUWA KAMISHNA MKUU IDARA YA UHAMIAJI.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Sylvester Ambokile Mwakinyule kuwa Kamishna Mkuu, Idara ya Uhamiaji.
Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana, Agosti 28, mwaka huu, 2013.
Ndugu Mwakinyule anachukua nafasi ya Ndugu Magnus Ulungi ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Sylvester Ambokile Mwakinyule, alikuwa Naibu Kamishna wa Uhamiaji na Mwambata wa Uhamiaji katika Ubalozi wa Tanzania, London, Uingereza
Rais pia amemteua Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro kuwa Msaidizi wa Rais, Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda.
Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana Agosti 28, mwaka huu, 2013.
Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro alikuwa Mkurugenzi wa Sekta za Uzalishaji (Productive Sectors) katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

I want to  burn  my  Nigeria passport