Thursday, 15 August 2013


Foleni ya Waumini wakisubiri zamu yao kwenda kumjulia hali Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda aliyelazwa kwenye wodi binafsi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (Moi) akipatiwa matibabu leo


Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa na mkewe Hadija Ahamad alipomtembelea jana. Picha na Beatrice Moses na Venance Nestory   
--
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda amesema alichanganyikiwa kiasi cha kushindwa kujielewa kwa muda baada ya kupigwa risasi.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi kwenye wodi binafsi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (Moi) alikolazwa jana, Sheikh Ponda alisema kutokana na hali hiyo hakumbuki matukio yaliyofuata baada ya hapo.
“Sikumbuki hata nilipata huduma ya kwanza hospitali gani kwa sababu sikuwa katika hali ya kawaida. Mambo mengine yaliyotendeka kabla ya kujeruhiwa ninayakumbuka vizuri,” alisema Ponda ambaye inasadikiwa kwamba alipigwa risasi ya begani, Ijumaa iliyopita mjini Morogoro.Kwa Habari Zaidi Bofya na Endelea...>>>>>>