Website: www.ccmuk.org, ccmuk.org/blog, Facebook –
chama cha mapinduzi uingereza, Twitter CCM UK.
WATANZANIA
WENGI JIJI LA CARDIFF-WALES (UK) WAJIUNGA NA CCM.
Katika ufunguzi huo Jumamosi tarehe 11 Mei
2013 ulijaa shamrashamra na nderemo na
kuhudhuriwa na viongozi wote wa Tawi la CCM UK, Mwenyekiti wa Tawi la
CCM UNITED KINGDOM Ndg Maina Ang'iela
Owino, Makamu Mwenyekiti Ndugu Said
Sukwa, Katibu Bi. Mariam Mungula, Naibu Katibu Ndugu Albert Ntemi, Katibu wa
Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Leybab Mdegela, Naibu Katibu Itikadi, Siasa na
Uenezi Ndugu Abraham Sangiwa, Katibu wa Uchumi na Fedha Ndugu John Juma Lyimo,
Naibu Katibu Uchumi na Fedha Ndugu Mohamed Upete na wanaCCM toka mashina
mbalimbali ya CCM UK.
Mwenyekiti wa Tawi la CCM UNITED KINGDOM
Ndg Maina Ang'iela Owino aliwashukuru
Watanzania hao kwa kujitokeza kwa wingi kuandaa, kuyakubali madhumuni na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi. Ndg Owino
aliwakumbusha kuwa uhalali wa shina lao unajumuishwa katika Sera ya nje
na matawi yake katika Katiba ya CCM.
Ndg Owino aliwakumbusha kuwa kujiunga na
CCM kunaambatana na kuzingatia masharti ya kuheshimu watu, kufanya juhudi za
kuielewa, kuielezea, kuitetea na kuitekeleza Itikadi na Siasa ya CCM. Pia
kwamba CCM inathamini haki na wajibu wa mwanachama.
Aidha Ndg Owino hakusita kuwakumbusha kuwa
CCM na Serikali yake inaendelea kujijenga na kuboresha taasisi zake ili
kuendana na mahitaji ya kizazi na wakati uliopo na hivyo basi wanaCCM Cardiff wasioneane haya wala kuogopa
kuchagua viongozi wenye sifa za kutosheka na wasio tawaliwa na tamaa na watakao
zingatia miiko ya uongozi kama inavyoainishwa katika katiba ya CCM.
Kabla ya kuhitimisha hotuba yake Ndg Owino
alichambua na kuainisha kwa kina na kuishirikisha halaiki kufanya tathmini ya
wazi ya jinsi CCM imeiongoza serikali kutekeleza ilani yake ya uchaguzi ya
2005/2010 na mafanikio dhahiri yanayopatika katika kutatua kero za wananchi.
Aidha alisema baadhi ya changamoto zilizopo nchini ni matokeo ya mabadiliko
endelevu, kukua na kuendelea kwa mifumo na taasisi za umma na sekta binafsi na
kwamba CCM na serikali yake inaendele kujiimarisha kuyakabili kwa mikakati na
mipango endelevu ya muda mfupi na mrefu, pia Ndugu Maina aliwakumbusha Wana CCM
UK Kuwa mchango wao unathaminiwa na ni wamuhimu katika kuleta mabadiliko
yatayowanufaisha wengi katika nyanja mbalimbali muhimu za kimaendeleo na
kichumi
Idara ya Itikadi Siasa na Uenezi na ile ya
Uchumi na Fedha walitoa machache yanayohusu idara zao na namna zinavyofanya
kazi ili kuwapa mwanga wanachama wapya na viongozi katika shina hilo.
Ufunguzi huo ulifuatiwa na uchaguzi wa
Viongozi mashina uliosimamiwa na Katibu wa CCM UK, Bi Mariam Mungula.
Viongozi waliochaguliwa katika shina hilo
jipya la Cardiff – Wales ni;
- Chande Kigwalilo Mwenyekiti wa Shina
- Bi. Rosemary Kiputa Katibu wa Shina
- Prudencia Kimiti Mjumbe wa Shina
- Munde Nyirambo Mjumbe wa Shina
- Alen
Mguto Mjumbe wa Shina
Mara baada ya uchaguzi huo Mwenyekiti wa shina jipya la Cardiff Ndugu
Chande Kigwalilo alitoa machache na kushukuru wajumbe na wanachama kumpa nafasi
ya kuliongoza shina na kushukuru uongozi wa tawi kwa kufanikisha ufunguzi huo
na kuwakarakibisha Jijini Cardiff.
Imetolewa na Idara ya Itikadi Siasa na
Uenezi
CCM TAWI LA UNITED KINGDOM