Monday 6 May 2013

TUKIO ZIMA LA KULIPUKA KWA BOMU KANISANI ARUSHA jana!!!

DSCN2227Hali ya eneo mlipuko ulipotokea
DSCN2220Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea
DSCN2228Ulinzi umeimarishwa
DSCN2252Viongozi wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa habari kabla ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
DSCN2246Wanasualama Mkoa wa Arusha, wakijadiliana jambo katika eneo la tukio
DSCN2282Meya wa Manispaa ya Arusha, Mh gaundence Lyimo akielekea eneo la tukio kwa miguu baada ya utaratibu wa kutumia magari kuwa mgumu kutokana na idadi kubwa ya watu na magari yaliyoziba njia.
DSCN2258Magesa Mulongo akiteta na RCO wa Mkoa wa Arusha
DSCN2273Mkuu wa Mkoa wa Arusha, magesa Mulongo akijiandaa kuzungumza na wananchi kanisani hapo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha watu wote waliohusika na jaribio hilo ovu, pamoja na mtandao wao wanakamatwa. Alidai pia vikosi vya Jeshi maalumu kwa kuchunguza milipuko vitafika eneo hilo ili kufanya uchunguzi. Taarifa za eneo la tukio zinaeleza kuwa tayari kuna mshukiwa mmoja ameshatiwa mbaroni na yuko mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
DSCN2236Eneo lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu kilipoangukia. Pichani unaweza kuona wigi za kichwani na viatu vya waumini vikiwa vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao wakiwa ni majeruhi.
DSCN2251
DSCN2267Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa mapadri wa Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani hapo.
DSCN2276
DSCN2255
DSCN2281
DSCN2225
DSCN2222
DSCN2215
DSCN2218
DSCN2219

PICHA YA KWANZA YA KANISA LA KATOLIKI LILILOPIGWA BOMU LEO ARUSHA!! & MAELEZO YA MKUU WA POLISI MKOA WA ARUSHA.


MOJA YA SEHEMU INAVYOONEKANA HAPA KANSANI JINSI MRIPUKO ULIVYOFANYA HAPA KANSANI,NAMSHUKURU MOLA NIKO SALAMA

RPC- ARUSHA ATHIBITISHA KUWA KILICHOLIPUA KANISA NI BOMU….WATU 3 WANAHALI MBAYA, 50 WAMEJERUHIWA

Mkuu wa Mkoa Mulongo naye  amefika  eneo  la  tukio  na  kuwafariji  wahanga  wa  tukio  la  bomu….
RPC  wa  mkoa  wa  Arusha  naye  aliambatana  na  mkuu  wa  mkoa  na  muda  huu  alikuwa  anatoa  nasaha  zake  kwa  wananchi….
 
RPC  ameeleza  kuwa  tukio  hili  ni  la kigaidi. Katika  maelezo  yake, RPC amesema kuwa  aliyehusika alijitokeza nyuma ya jengo kwa kujificha na kurusha bomu. …
 
Amesema Polisi wanawasaka waliohusika  na  unyama  huu  na  ameomba yeyote  mwenye taarifa yoyote aisaide polisi. ..
Waliojeruhiwa ni 50 .Hao wana majeraha ya kawaida  na 3 wako  mahututi. Mpaka sasa  mtu mmoja anashikiliwa  na  polisi kwa mahojiano  zaidi