Sunday 5 May 2013

 Sehemu inayosadikiwa kitu kama bomu kulipuka
 Baadhi ya viatu vya waumini mbalimbali waliojeruhiwa
 Baadhi ya majerui wakiwa nje ya kanisa wakisubiri msaada wa kupelekwa hospitali.
 Picha Juu na chini ni baadhi ya majerui wakipatiwa matibabu hospitali
Picha juu ni baadhi ya wauminina viongozi mbalimbali wa kanisa wakiwa  nje ya kanisa muda mfupi baada ya kitu kichachosadikiwa kuwa ni bomu kulipuka nakusababisha majeruhi zaidi ya 30 leo asubuhi.Picha Zote kwa Hisani ya Mdau Frederick M. Katulanda
 ---
Na Mwandishi Wetu



Bomu limelipuka majira ya saa 5 leo asubuhi katika uzinduzi wa Parokia mpya ya Olasiti, Jijini Arusha wakati Askofu Mkuu Josephat Louis Lebulu na Balozi wa Baba Mtakatifu nchini, Askofu Mkuu  Francisco Montecillo Padilla wakiwa wamejiandaa kuanza maadhimisho ya misa ya kutabaruku kanisa hilo kwa kuwabariki waumini hao tayari kwa ibada.



Taarifa za awali zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas zinasema kuna majeruhi zaidi ya 30, lakini wanne walikuwa na majeraha makubwa, na amewataka wananchi kutoa ushirikiano kuweza kuwabaini waliorusha na/au kutega bomu kwenye eneo hilo la Ibada.



Akiahirisha Ibada hiyo Vicar General wa Jimbo Katoliki la Arusha Padre Simon Tengesi aliwataka wakristo wote kuondoka eneo hilo na uzinduzi huo umeahirishwa hadi pale itakapotangazwa tena, na watu wameondoka eneo hilo ili kuruhusu vyomvyo vya ulinzi na usalama viweze kuanza uchunguzi.



Chanzo chetu cha habari kinasema eneo lilipolipuka bomu kuna damu nyingi na watu wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili, Tutaendelea kuwajuza zaidi.

  PICHA YA KWANZA YA MAJERUHI WA KANISA LILILOPIGWA BOMU LEO ARUSHA!!



.
.

.
Hii ni baada ya mlipuko
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Baada ya mlipuko.
.
Hawa ni baadhi ya walionusurika.
.
.
.
.
.
.
.
Picha zote zimepigwa na thechoicetz.com
.
Polisi wakiendelea na uchunguzi
.

The Tanzania president  is  on  a  two  day  state  visit to  Kuwait

 

Taswira Rasmi Kutoka IKULU:Rais Jakaya Kikwete Atua Kuwait Kwa Ziara Rasmi ya Siku Mbili

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mtawala wa Dola ya Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah wakipokea mashada ya mauwa alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei 5, 2013 tayari kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika nchi hiyo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mtawala wa Dola ya Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei 5, 2013 tayari kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika nchi hiyo.
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mtawala wa Dola ya Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah wakiingia sehemu ya mapokezi na kukagua gwaride rasmi mara tu alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei 5, 2013 tayari kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika nchi hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mtawala wa Dola ya Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah katika mazungumzo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei 5, 2013 tayari kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika nchi hiyo.Picha na IKULU