Kwa heshima
Nakuletea mwaliko huu kukualika rasmi kwenye mkutano wa kuzungumzia maswala muhimu ya kitaifa yanayotugusa Wa-Tanzania wote.  Mkutano huo utafanyika Reading siku ya Jumamosi tarehe 01/06/2013 kuanzia saa 9.00 (saa tisa) jioni hadi 12.00 (kumi na mbili) jioni.
Kama waTanzania wapenda maendeleo, tumeonelea kuna umuhimu wa kuwaunganisha Wa-Tanzania kuchambua na kuzungumzia mambo muhimu yanayotuhusu sisi sote. Kwa kufanya hivi tutakuwa tumeruhusu na kuwapa Wa-Tanzania sauti (platform) ya kuyazungumzia maswala mbali mbali kwa uwazi. Hivyo basi tumeandaa mjadala utakaorekodiwa na kurushwa kupitia YouTube channel. Katika mjadala huu, Wa-Tanzania wote wenye mapenzi na nchi yao wanategemewa kuhudhuria bila kujali itikadi, dini, rangi au kabila. Mjadala huu utazungumzia mambo manne ambayo ni UTAIFA, KATIBA, ELIMU, na MUUNGANO.
Uwakilishi weko utaongeza chachu na kupeleka ujumbe kwamba waTanzania tulioko UK tuko mstari wa mbele kuyachambua maswala yanayoihusu jamii yetu kwa ueledi mzuri (with maturity) bila kuleta ushabiki wa kidini, kichama, n.k.
Vyama mbali mbali vya kisiasa, Wawakilishi kutoka vikundi vya kidini na vikundi mbali mbali hapa UK vitahudhuria.
Kutokana na hayo, tunachukua fursa hii kukualika kuhudhuria mjadala huu ambao unatuhusu sisi sote Wa-Tanzania na siyo wa kichama au kidini. Hakutakuwa na nembo au maneno ya kuashiria kwamba hii imeandaliwa na chama au kikundi Fulani bali zitatandazwa nembo za taifa. Hii katika kuonesha nia na madhumuni yaliyopelekea sisi kuandaa mjadala huu.
Wako katika maendeleo ya nchi.