Friday 15 August 2008

bbc

Agosti 13, 2008BBC Idhaa ya Kiswahili,kama kawaida inaendelea kutoa burudani ya soka isiyo na kifani kwa mashabiki waliopo Afrika Mashariki na Kati kupitia kipindi chake maarufu, BBC Ulimwengu wa Soka.
Kikosi kizima cha BBC Ulimwengu wa Soka - Alex Mureithi, Charles Hilary,Idd Seif, Hassan Mhelela, Peter Musembi and Salim Kikeke, kitakuletea maelezo na matokeo ya mechi zote za ligi kuu ya soka ya England msimu huu, inayoanza Jumamosi Agosti 16.Katika kuanza msimu,BBC Ulimwengu wa Soka itakutangazia moja kwa moja mchezo kati ya Hull itakayocheza na Fulham,kwenye uwanja wa KC. Matangazo ya mchezo huo yataanza saa kumi na nusu Afrika Mashariki.
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC Solomon Mugera anasema:" Tulianza matangazo ya moja kwa moja ya ligi kuu ya England mwaka 2006. Wasikilizaji wetu wanatuambia kipindi cha BBC Ulimwengu wa Soka kimewanufaisha kupindukia, kuwaburudisha na kufuatilia vilivyo mechi za soka, na kwa lugha wanayoielewa vyema ya Kiswahili. Tutatangaza tena msimu huu wote, na nina hakika wasikilizaji wetu watafurahia sana".
Jinsi ya kupata matangazo ya BBC Ulimwengu wa Soka:Nchini Burundi,BBC Ulimwengu wa Soka inapatikana mjini Bujumbura kupitia 90.2 FM,
na katika 105.2 FM kwa maeneo mengine.
Nchini Kenya,BBC Ulimwengu wa Soka inapatikana kupitia redio washirika Radio Simba mjini Nairobi katika 102.7 FM,Sheki FM mjini Mombasa katika 106.6 FM na kupitia West FM mjini Bungoma katika 94.9 FM.
Nchini Rwanda,BBC Ulimwengu wa Soka inapatikana mjini Kigali katika 93.9 FM,
mjini Butare katika 106.1 FM, na mjini Kibuye katika 93.3 FM.
Nchini Tanzania,BBC Ulimwengu wa Soka inapatikana mjini Zanzibar katika 94.1 FM na Pemba katika 93.5 FM.Vilevile unaweza kupata matangazo haya kupitia radio washirika:
Radio Free Africa mjini Dar Es Salaam katika 98.6FM,
Mwanza katika 89.8FM,Shinyanga katika 88.2FM, Kagera katika 94.1FM, Arusha katika 89.0FM, Mbeya katika 88.8FM,Dodoma katika 89.0FM,Rukwa katika 89.1FM, Ruvuma katika 89.6FM, Mtwara na Lindi katika 89.0FM,Singida katika 88.3FM, Iringa katika 93.5FM, Tanga katika 99.3FM, Tabora katika 90.0FM, Kigoma katika 90.0FM,Morogoro katika 93.8FM, Kilimanjaro katika 88.2FM, Mara katika 93.5FM na katika 1377 AM/MW kwenye maeneo yote Tanzania.
Pia kupitia Radio One mjini Dar Es Salaam katika 89.5 FM, Arusha katika 95.3 FM, Dodoma katika 100.8 FM, Mwanza katika 102.5 FM, Moshi katika 1323 AM na katika 1440AM kwenye maeneo mengine yote. Radio 5 mjini Arusha katika 105.7 FM, na Sky FM katika 101.4 mjini Dar es Salaam.
BBC Ulimwengu wa Soka pia inapatikana kote Afrika Mashariki na Kati kwenye
masafa Mafupi katika 11705 kHz,na vilevile kwenye tovuti:
www.bbcswahili.com
BBC Idhaa ya Kiswahili pia itakuletea matangazo ya mechi zifuatazo:Jumamosi,Agosti16,2008 Hull v FulhamJumamosi,Agosti 23,2008 Liverpool v MiddlesbroughJumamosi,Agosti 30, 2008 Everton v PortsmouthJumamosi,Septemba 13,2008 Blackburn v ArsenalJumamosi,Septemba 20,2008 Liverpool v StokeJumamosi,Septemba 27,2008 Man Utd v BoltonJumamosi,Oktoba 04,2008 Chelsea v Aston VillaJumamosi,Oktoba 18,2008 Liverpool v WiganJumamosi,Oktoba 25,2008 Tottenham v BoltonJumamosi,Novemba 01,2008 Chelsea v SunderlandJumamosi,Novemba 08,2008 Man City v TottenhamJumamosi,Novemba 15,2008 Arsenal v Aston VillaJumamosi,Novemba 22,2008 Chelsea v NewcastleJumamosi,Novemba 29,2008 Tottenham v EvertonJumamosi,Disemba 06,2008 Bolton v ChelseaJumamosi,Disemba 13,2008 Tottenham v Man UtdJumamosi,Disemba 20,2008 Arsenal v Liverpool
Ratiba hii inaweza kubadilishwa wakati wowote na mamlaka husika.
BBC haihusiki na mabadiliko hayo.Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:
Solomon Mugera,Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBCsolomon.mugera@bbc.co.ukChristine George,Assistant International Publicist,BBC World Service+44(0)207557 1142;christine.george@bbc.co.uk