Rais Kikwete safarini Saudi Arabia, Ujerumani, Ufaransa na Ethiopia
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mjini Riyadh, Saudi Arabia,asubuhi ya leo, Jumapili, Januari 25, 2015, kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita.
Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.
Mjini Berlin, Ujerumani ambako Rais Kikwete alitarajiwa kuwasili kesho, Jumatatu, Januari Ishirini na Sita, akitokea Riyadh, Saudi Arabia, anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Global Alliance for Vaccines and Immunization (GAVI Alliance) ambako viongozi mbali mbali duniani watajadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea.
Baada ya kumaliza ziara yake Ujerumani, Rais Kikwete atakwenda Ufaransa ambako miongoni mwa mambo mengine atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ufaransa.
Aidha, Rais Kikwete atafungua jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania katika Ufaransa na pia nyumba ya balozi.
Rais Kikwete baada ya kumaliza ziara zake za kikazi katika Ujerumani na Ufaransa atakwenda Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).
ENDS
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
25 Januari, 2015
Rais Kikwete akiwasili mjini Riyadh, Saudi Arabia, asubuhi ya Jumapili, Januari 25, 2015 |
Related Posts:
- Mwanao anapojiondolea ‘presha’ kwa ‘kukupotezea’ - Fahamu uhusiano wako na mwanao unavyoathiri tabia yake(photo: colourbox.com) Ili kujihami na hali ya kujiona mpweke asiyeeleweka, mbinu ni kutumia akili kugundua kile hasa kinachoweza kumfanya mzazi …Read More
- Mbwana Samata awajibika na CSK Moscow mazoezini SpainMbwana Ally Samata mchezaji wa soka Mtanzania aliyekuwa akiichezea timu ya Congo DRC ya TP Mazembe, yupo katika klabuu ya Urusi ya CSK Moscow kwa… Read More
- Aaga kurudi nyumbani, mauti ikamfika akiwa kwa 'mchepuko'John Haule (35) mkazi wa Lupapila Manispaa ya Songea amefariki Dunia ghafla wakati akifanya mapenzi nyumbani kwa mpenzi wake jina linahifadhiwa. Akizu… Read More
- Madiwani Moshi wakataa kupitisha bajeti hadi kiwaja kirudiMadiwani na wanahabari wakiwa nje ya lango la Ofisi ya Manispaa ya Moshi Kikao cha Bajeti ya Hamlashauri ya Manispaa ya Moshi kimeshindwa kuamua … Read More
- The real reason for cheaper gas in winterThe reason for the price change is that winter gasoline and summer gasoline are produced using a different formula of additives. The practice of u… Read More