Sunday, 25 January 2015


  Prof Sospeter Muhongo akizungumza na waandishi wa habari hii jana wakati akitangaza kujiuzulu wadhifa wake wa Uwaziri wa wizara ya Nishati na Madini.
Baadhi ya waandishi na maofisa mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia maelezo ya kujiuzulu Waziri Prof. Sospeter Muhongo hii  jana.
----
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa wake wa uwaziri hii  jana.

Prof. Muhongo ametangaza uamuzi huo asubuhi ya jana katika mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Nishati na Madini.

Akitangaza uamuzi huo Prof. Muhongo amesema ameamua kuachia wadhifa huo ili kupisha nchi ijadili na kufanya mambo muhimu ya maendeleo badala ya kuendelea kujadili masuala ya Escrow.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Masha J. Musomba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.Uteuzi huo ulianza Alhamisi iliyopita, Januari 22, 2015.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Musomba alikuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
25 Januari, 2015