Tuesday 20 January 2015

 Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari akiwasili katika mkutano huo.
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki ,Ndolakindo Kessy akizungumza katika  mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Ghalani ,mji mdogo wa Himo ,mkutano uliokuwa na lengo la kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Vunjo kukipa chama hicho viti vingi katika uchaguzi wa serikali za Mitaa,vijiji na Vitongoji.
 Mh Nassari na Mh Mbatia wakitoa salamu kwa mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo .
 Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akizungumza na wananchi katika jimbo la Vunjo,wakati wa mkutano wa hadhara ulioitishwa na Chama cha NCCR-Mageuzi kwa lengo la kuwashukuru kwa kuchagua wenyeviti wengi waliotokana na chama cha NCCR-Mageuzi,mkutano uliohutubiwa pia na Mbunge wa kuteuliwa na rais,James Mbatia.
 Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi ,James Mbatia akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya ghalani katika mji mdogo wa Himo jimbo a Vunjo alipokuwa akiwashukuru wakazi wa jimbo hilo kwa kukipa ushindi chama chake katika uchaguzi wa serikali za Mitaa ulimalizika hivi karibuni.
 
  Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo.