Sunday, 14 October 2012

Waziri mkuu Mh Pinda kukutana na watanzania UK

Waziri mkuu mh Mizengo Pinda atakutana na watanzania waishio UK dhumuni likiwa ni kuzungumzia mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu kisiasa, kiuchumi, n.k. Pamoja na hayo pia maswala yaliyozungumzwa kwenye ziara yake ya mara ya kwanza yataelezewa.
Siku: Jumanne 16, October 2012
Mahali: Tanzania High Commission
Time: 17:00 jioni (saa kumi na moja jioni).
Inashauriwa wale wote wanaopenda kuhudhuria wajiandikishe kupitia email:
Wote mnakaribishwa.

NI SIMANZI NA VILIO,MAOMBI YATAWALA MBAGALA LEOAskofu mkuu wa KKKT Alex Malasusa akiwaasa wakristu kuwa watulivu wakati huu wakati mamlaka za dola zikishughulikia swala hili,wakati huu wadumu katika maombi na wawasamehe ndugu zao waislamu. na kuwaombea.Mungu atawapiganiawaumini wakiwa katika maombi na huyu akilia kwa uchungu
Mchungaji wa TAGP akiongoza maombi wakristo wakiwaombea waislamu.Mpaka muda huu hakuna kiongozi yeyote wa serikali ameshafika eneo la matukio na uongozi wa kanisa unawasubiria viongozi wa kiserikali

MAUAJI YA KINYAMA YATIKISA NCHI HUKO MWWANZA

 

Picture
Liberatus Barlow

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Barlow ameuawa saa tisa usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa
blogu ya Said Powa na tovuti ya gazeti la Habari Leo:

Tukio hilo linahusishwa na ujambazi.

Taarifa kutoka Mwanza ambazo zimethibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema, zinasema kuwa Kamanda Barlow wakati akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake akitoka kumrudisha dada yake ambaye alikuwa kwenye kikao cha harusi ya ndugu yao huko Kitangili.

Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai DCI Robert Manumba akiwa na kikosi cha makachero tayari wameshakwenda mwanza kuongeza nguvu katika upelelezi mkali ambao umekwishaanza.

---

Kwa mujibu wa
blogu ya CCM Chama:

Kamanda Barlow alipigwa risasi na watu wasiojulikana kiasi cha saa sita usiku, atika eneo la Kitangiri, kwenye kona ya Bwiru, Mwanza.

Inadaiwa kuwa Kamanda huyo alikuwa akimwendesha mwanamke mmoja ambaye bado hajatambulika, akimpeleka nyumbani kwake baada ya kutoka kwenye sherehe ya harusi.

“Inadaiwa kwenye harusi hiyo kuna mwanamke alimwomba ampeleke nyumbani, akamchukua katika gari na kumpeleka, walipofika eneo la Kitangiri, pale kona ya Bwiru, walitokea watu ambao wamempiga risasi moja shingoni...” (amesema mtoa habari kutoka Mwanza


Source: http://www.wavuti.com/#ixzz29BX7rHhJ