Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti katika bustani ya Jumba
la Rideau Hall jijini Ottawa katika siku ya pili ya ziara yake rasmi
nchini Canada huku akishuhudiwa na Gavana Jenerali wa nchi hiyo Mhe
David Johnson na mkewe Mama Sharon Johnson Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen
Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo, ambapo viongozi
hayo wawili walifanya mazungumzo Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisimama wakati wimbo wa Taifa wa
Tanzania ukipigwa mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la
askari shujaa katika bustani ya Confederation Square jijini Ottawa
Alhamisi Octoba 4, 2012. Mbele yake ni baadhi ya veterani wa kijeshi
waliohudhuria hafla hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi
la askari shujaa katika bustani ya Confederation Square jijini Ottawa
Alhamisi Octoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha
wageni mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la askari
shujaa katika bustani ya Confederation Square jijini Otttawa Alhamisi
Octoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha
wageni mara baada ya kupokelewa katika Bunge la Seneti la Canada. Kulia
ni Spika wa Bunge hilo Mhe Noel Kinsella, anayefuatiwa na Waziri Mkuu wa
Canada Mhe Stephen Harper na Spika wa Bunge la wawakilishi la Canada
(House of Commons), Mhe Andrew Scheer pamoja na viongozi wengine wa
bunge hilo Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen
Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo, ambapo viongozi
hayo wawili walifanya mazungumzo Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi toka kwa Waziri Mkuu
wa Canada Mhe Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi
hiyo, Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi ya sanduku la Zanzibar
(Zanzibar chest) Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper katika jengo
la Bunge la Seneti la nchi hiyo Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Spika wa Bunge
la Seneti la Canada ramani ya dunia na njia za meli, pamoja na
kuoneshwa chemba ya mikutano ya Maseneta wa Bunge la Canada Alhamisi
Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa katika ofisi ya Spika
wa Bunge la Wawakilishi la Canada (House of Commons) Mhe Andrew Sheer.
Spika huyu, mwenye umri wa miaka 32, ndiye kiongozi kijana kuliko wote
katika historia ya nchi hiyo waliopata kuchaguliwa kuongoza bunge hilo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Waziri
Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper wakishudia uwekaji sahihi mkataba wa
ushirikiano kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa
wa Tanzania Mhe. Bernard Membe na Waziri wa Canada katika Bunge la
seneti la nchi hiyo Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Waziri
Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper wakishudia uwekaji sahihi mkataba wa
ushirikiano kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa
wa Tanzania Mhe. Bernard Membe na Waziri wa Canada katika Bunge la
seneti la nchi hiyo Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Spika wa Bunge la Seneti la
Canada ramani ya dunia na njia za meli, pamoja na kuoneshwa chemba ya
mikutano ya Maseneta wa Bunge la Canada Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Waziri Mkuu
wa Canada Mhe Stephen Harper wakitembea kuelekea kwenye chumba cha
mkutano kuongea na wanahabari. Zuria jekundu na bendera za Canada za
kiongozi wa nchi husika huwekwa sehemu hiyo kwa heshima na wakati wa
ziara ya kiongozi wa nchi ya nje aliye katika ziara rasmi nchini humo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Canada Mhe
Stephen Harper wakiongea na wanahabari katika jengo la Bunge la Seneti
la nchi h
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Watanzania Richard Katambi
Masalu na mkewe Patricia katika jengo la Rideau Hall jijini Ottawa
kabla ya kuondoka kuelekea Edmonton
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo (wa pili mbele kushoto) na Balozi wa Tanzania
nchini Canada Mhe Alex Massinda (mbele kushoto) wakiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa makampuni ya Canada baada ya mazungumzo katika
jengo la Rideau Hall jijini Ottawa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mabalozi wa nchi za Afrika wanaowakilisha
nchi zao nchini Canada, na baadaye kupiga nao picha ya pamoja
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Gavana Jenerali wa
Canada Mhe David Johnson baada ya kuihitimisha ziara yake ya siku mbili
jijini Ottawa. Baada ya hapo alielekea jijini Edmonton ambako pamoja na
shughuli mbalimbali alitarajiwa kufungua mkutano wa Diaspora wa
Watanzania wanaoishi Canada pamoja na wawamkilishi wa makampuni na
mashirika waliotoka Tanzania kuhuduria mkutano huo.Picha na IKULU