Sunday, 13 September 2015

 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli aliyenyanyua kofia (katikati) akiwasili katika uwanja wa  CCM mjini Bariadi kwa ajili ya kuwahutubia kwenye mkutano wa kampeni mkoani Simiyu.
 PICHA NA MICHUZI JR-SIMIYU.

 Wananchi wakishangilia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni mjini Bariadi
 Wananchi wa Nanga wilaya ya Itilima wakishangilia ujio wa Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipita kuwasalimia
 Umati wa wakazi wa kijiji cha Mwanhunzi wilaya ya Meatu wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni za CCM mjini Meatu,mkoani Simiyu jioni ya leo
 Wananchi wakimsiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufui alipokuwa akiwahutubia mjini Meatu jioni ya leo.Dkt Magufuli leo ametembelea wilaya ya Busega,Bariadi,Itilima pamoja na wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi, Dk.Magufuli akiwahutubia wakazi wa mji wa Mwanhunzi jioni ya leo mjini Meatu mkoani Simiyu,Dkt Magufuli alisema kuwa atakapokuwa Rais atakuwa karibu na wananchi wanyonge na kuwa yeye anatoka katika familia ya watu maskini na anajua nini maana ya umaskini,Alisema anatoka kwenye familia ya wakulima na wafugaji  hivyo anajua nini ambacho anatakiwa kufanya kuboresha maisha ya makundi hayo mawili na kwenye hilo atahakikisha anaweka mazingiza mazuri ya matumizi bora ya ardhi.

Alisema Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema na kwenye hilo ana uhakika atafanya kazi nzuri maana kwake yeye ni kazi tu na hakuomba kuwa Rais ili awe mwanasiasa bali anaomba nafasi hiyo kwa kujua anajua namna ambavyo amejipanga kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote.

"Nitakuwa upande wenu wananchi wanyonge.Serikali yangu ni marufuku watu wa bodaboda kushikwa na polisi.Serikali yangu haitakuwa ya kunyanyasa mama ntile na kudaiwa kodi za hovyo.Hivyo sitakuwa tayari kuona mama ntile wanatozwa kodi.Najua nitaimarisha ukusanyaji wa kodi kwenye serikali yangu lakini nitawabana wafayabiashara  wakubwa ambapo baadhi yao hawalipi kodi,"alisema Dk.Magufuli.

Aliwataka wananchi kumuamini kwa yale ambayo amekuwa akiyasema kwenye mikutano yake ya kampeni na kuongeza anachoahidi ndicho ambacho atakitekeleza kwenye serikali yake na kwenye maisha yake huwa hataki kutoa ahadi za uongo.

Dk.Magafuli aliweka wazi anapenda mabadiliko yenye tija na kwamba Serikali yake itasimamia nidhamu kwa watumishi wa umma ili wafanye kazi ya kuwatumikia waanchi usiku na mchana na ndio maana atawalipa vizuri na kuongeza hapendi watu wavivu kwenye kazi.

 Umati wa wakazi wa kijiji cha Mwanhunzi wilaya ya Meatu wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni za CCM mjini Meatu,mkoani Simiyu jioni ya leo.

 Wananchi wa Mwanhunzi mjini Meatu wakifautilia mkutano huo wa hadhara wa kampeni.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea Ubunge na Madiwani kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni  Mwanhunzi,mjini Meatu jioni ya leo mkoani Simiyu.
 Wakazi wa Lamadi ndani ndani ya wilaya ya Busega,Mkoani Simiyu wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika mjini humo leo.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Busega,Raphael Chegeni akiwahutubia wananchi wa Busega mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.
 Mwenyekiti wa Wazazi CCM Taifa Ndugu Abdallah Bulembo akimkaribisha mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kuwahutubia wananchi wa Busega,mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Busega mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Busega mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.Dkt Magufuli aliwaomba wananchi hao kuitunza amani waliyonayo na kuwa kuwapuuza wale wote wenye maneno ya kuleta ufarakanishi katika nchi yetu
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mkula,alipokuwa akipita kuwasalimia wananchi hao akielekea Wilayani Busega kwenye mkutano wa hadhara.
 Maandalizi ya kumpokea Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ndani ya uwanja wa CCM mjini Bariadi yalikuwa kama hivyo pichani.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa Mwanhunzi,alipomaliza kuwahutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo mjini Mwanhunzi,Wilayani Meatu mkoani Simiyu.