Wednesday, 9 September 2015

KAMPUNI YA SIMU YA TIGO NA DTBi WAZINDUA HUDUMA YA KUREJESHA KUMBUKUMBU NA KUZUIA WIZI WA SIMU ZA MKONONI DAR ES SALAAM LEO
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk.Binilith Mahenge (kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha oparesheni  cha Kampuni ya MagilaTech, iliyotengeneza teknolojia ya tigo backup inayowezesha kurejesha kumbukumbu na kuzuia wizi wa simu za mkononi Dar es Salaam leo. 
Wanahabari na wadau wengine wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez (kulia), akitoa hutuba yake.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Hassan Mshinda (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya DBTi, Balozi Ami Mpungwe.
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk.Binilith Mahenge, kwa niaba ya Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharib Bilal aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo akisoma hutuba.
Meneja wa mradi huo kutoka Tigo, Atuletye Mwamila (kulia), akielekeza jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi na kuwezesha kuipata simu iliyopotea na kumbukumbu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Magila Tech iliyotengeneza Teknolojia ya Tigo Backup, Godfrey Magila akielezea jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi.
Mwenyekiti wa Bodi ya DBTi, Balozi Ami Mpungwe (kushoto), akizungumza katika uzinduzi huo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Hassan Mshinda.
Wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Maofisa wa ufundi, Rahim Hussen (kushoto) na Mkupete Mkamba (kulia), wakitoa maelezo wa kifaa mfano wa ndege kinachorushwa angani na kuweza kubaini magonjwa katika mimea walicho kibuni.
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Binilith Mahenge (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha oparesheni  cha Kampuni ya Magila Tech, iliyotengeneza teknolojia ya tigo backup inayowezesha kurejesha kumbukumbu na kuzuia wizi wa simu za mkononi Dar es Salaam leo, kilichopo Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech). Kituo hicho kinashirikiana na kampuni ya simu ya tigo, Dar Teknohama Business Incubator (DTBi), pamoja na Costech kuendesha mradi huo. Kutoka kulia ni Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Magila Tech iliyotengeneza Teknolojia ya Tigo Backup, Godfrey Magila na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Magila Tech iliyotengeneza Teknolojia ya Tigo Backup, Godfrey Magila (kulia), akitoa maelezo kwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Binilith Mahenge jinsi kituo hicho cha oparesheni kinavyofanya kazi.


Na Dotto Mwaibale


KAMPUNI ya Mawasiliano ya simu ya Tigo kwa kushirikiana na Kituo cha Kukuza Vijana Wenye Mawazo ya Sayansi na Teknolojia (DTBi), wamezindua huduma itakayowawezesha watumiaji wa simu za kisasa (smartphone) kurejesha kumbukumbu na kupatikana kwa simu iliyopotea au kuibiwa.

Akizungumza kabla ya kuzinduliwa rasmi huduma hiyo Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dar es Salaam leo asubuhi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk.Binilith Mahenge, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez, alisema huduma hiyo inaitwa 'Tigo Backup' itakuwa na uwezo wa kurudisha majina yote kwenye simu, picha, video, ujumbe mfupi 'sms' na vitu vingine vilivyopotea.

Alisema mteja ataweza kugundua na kurejesha simu zao zilizopotea au kuibiwa na pia huduma hiyo itamuwezesha mteja kuwa na uwezo wa kupata picha ya aliyemuibia kwani simu itapiga king'ora.

" King'ora hicho kitaonesha simu ilipo, simu itajifunga ili kuzuia matumizi mabaya, kumjulisha mwenye simu pindi abadilishapo laini na kwamba huduma hiyo imebuniwa na mwanafunzi mzawa kutoka DTBi ," alisema Gutierrez.

Kwa upande wa Waziri, Dk. Mahenge alizishukuru kampuni hizo kuwajengea uwezo na kuwawezesha Watanzania kuleta maendelea katika nchi yao na kujijengea utajiri kupitia ubunifu huo.

Alisema Tanzania nchi inayoungwanishwa kidigitali zaidi kwa kutumia sismu kuliko kompyuta na kwa mujibu wa takwimu za watumiaji wa simu zinaonesha kuna ongezeko kubwa kutoka watu milioni 2.96 mwaka 2005 hadi milioni 33 mwaka huu.


Alisema kwa kutambua nchi ni changa ambayo watu wake asilimia 50 ni vijana, wamejikita katika kutoa elimu ya ufundi katika sayansi na teknolojia yenye ubunifu.