Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ukiwasilia katika mkutano wa hadhara wa kampeni,Korogwe vijijini.

MGOMBEA
 urais kwa teketi ya CCM, Dk.John Magufuli akifafanua jambo kwa 
msisitizo huku akibainisha kuwa iwapo atachaguliwa kwenye uchaguzi mkuu 
mwaka huu, basi Serikali yake itahakikisha inaboresha maslahi ya 
watumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini kutokana na kutambua 
mchango wao katika kulinda amani ya nchi yetu.
Dkt Magufuli alisema kuwa anataka kuona watumishi wa jeshi hilo wanakuwa na mishahara mizuri na hiyo itawezesha kufanya kazi ya ulinzi na usalama wa nchi kwa ufanisi zaidi huku akitumia nafasi hiyo kuomba Watanzania kudumisha amani ya nchi kwani ikipotea hakutakuwa na maendeleo ya aina yoyote.
Dk.Magufuli alitoa kauli hiyo leo katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Korogwe, Mkinga na Lushoto ikiwa ni sehemu ya mikutano ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa rais ambapo alisema anatambua kazi nzuri inayofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama na kuongeza kuwa serikali yake itaboresha maslahi ya wanajeshi wa majeshi yote Nchini . PICHA NA MICHUZI JR-LUSHOTO,TANGA

Mgombea
 Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Bumbuli 
wakiwaaga wananchi wa Bumbuli waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa 
kampeni uliofanyika mjini humo jioni ya leo.
Mgombea
 wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa 
Lushoto kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jitegeme.
  Lushoto ikiwa imefurika watu tayari kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea
 Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasili kwenye mkutano wa 
hadhara  katika uwanja wa Togotwe-Mponde wilayani Bumbuli kuwahutubia 
wananchi na kuwaomba ridhaa ya kuwaongoza katika awamu ya tano.
  Mgombea
 wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa ubunge
 jimbo la Bumbuli Ndugu January Makamba kwenye mkutano wa kampeni 
uliofanyika kwenye viwanja vya Togotwe.
Mgombea
 Ubunge jimbo la Bumbuli Ndugu January Makamba akisisitiza jambo kwa 
Wananchi wake katika jimbo la Bumbuli jioni ya leo kwenye mkutano wa 
kampeni 
uliofanyika kwenye viwanja vya Togotwe.
 Wakazi
 wa Jimbo la Bumbuli wakifuatilia kwa makini mkutano wa Mgombea wa Urais
 kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya 
leo. 
  Mgombea
 wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa 
kata ya Magoma wakati akiwa njiani kuelekea Korogwe mjini kwenye mkutano
 wa kampeni za CCM.
  Mgombea
 wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa 
Mashewa wilayani Korogwe kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo 
aliwaambia wananchi hao kuwa serikali yake itakuwa ya kuchapa kazi kwa 
maendeleo ya wananchi na nchi kwa jumla.
  Mgombea
 wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM pamoja na kumnadi mgombea Ubunge wa
 Jimbo la Korogwe Vijijini Ndugu Stephen Ngonyani kwenye mkutano wa 
kampeni uliofanyika Kwamazandu, Korogwe Vijijini.
Bangozzzz
 Mgombea
 wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea ubunge
 wa Jimbo la Korogwe mjini  Mary Chatanda Ilani ya uchaguzi ya CCM 
kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya chuo cha ualimu 
Korogwe.
Mwenyekiti
 wa Wazazi CCM Taifa,Ndugu Bulembo akimkaribisha mgombea Urais wa CCM 
Dkt John Pombe Magufuli kuwahutubia wananchi katika uwanja wa 
Togotwe-Mponde wilayani humo.
Wakazi wa Bumbuli waliojitokeza kwa wingi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa kampeni wa CCM jioni ya leo,
 Mgombea
 wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa 
Bumbuli kwenye viwanja vya Togotwe ambapo aliwaahidi kuwajengea barabara
 ya lami pamoja na kufuatilia suala la kiwanda cha Chai cha Mponde.

Wananchi wakifuatilia mkutano.
  Mgombea
 Ubunge jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba akifafanua jambo mbele ya umati wa wananchi  wa 
Jimbo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya 
Togotwe.
Wananchi wa Lushoto mjini wakishangilia jambo mara baada ya kumsikia Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia .