Tuesday 8 October 2013

Kituo cha kisasa cha vijana cha Iringa Football for Hope Centre kinatarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa wiki hii mjini Iringa ikiwa ni sehemu shamrashamra za uzimwaji wa Mwenge wa Uhuru.

Akizungumza mjini Iringa juzi Katibu Mkuiu wa TFF, Angetile Osiah alisema kituo hicho kilichojengwa na Shirika la Vijana, Walemavu na Watoto (IDYDC) la mkoani Iringa kimefadhiriwa na shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA) ili ukuza vipaji vya mpira na kutoa elimu na ushauri nasaha.
 
"Mradi huu haupitii moja kwa moja katika vyama vyetu vya michezo bali katika taasisi zinazotoa eklimu za kijamii na kufundisha soka" alisema Angetile.

Alipongeza shirika la IDYDC kwa kukamilisha mradi huo na kusema kitendo hicho kitafanya FIFA kutoa fedha zaidi kwa ajili ya miradi kama hiyo nchini.
 
"FIFA watafurahi kuiona fedha walizotoa zinatumika ipasavyo kitu ambacho kitawafanya wawe radhi kutoa misaada zaidi na hii itasaidia kukuza soka letu".

Mkurugenzi wa IDYDC Jonnie Nkoma alimweleza Katibu Mkuu wa TFF kwamab kwa sasa ujenzi wa kitu hicho uko katika hatua za mwishoni kukamilika na kwamaba kitaanza kuhudumia timu za watoto na vijana zaidi ya 120 kitakapofunguliwa.
 
Nkoma alisema kituo hicho kitakuwa kinatumika usiku na mchana kwani wanafunzi na watoto watakuwa wakipata mafunzo nyakati za jioni wakati vina na watoto wa mitaani watatumia usiku kwa ajili ya mazoezi ya kukuza vipaji vyao.
 
"Mbali na michezo vijana watakuwa wanapata mafunzo ya afya ya uzazi na ugonjwa waUkimwi na pia watapata nafasi ya kujua afya zao kwa kupima Ukimwi butre hapahapa kituoni.

Mbali na uwanja kituo hicho kina ofisi, vyumba vya kutoa elimu na ushauri nasaha, upimaji wa VVU, chumba cha kompyuta na darasa.
 
Mkurugenzi wa Shirika la Vijana, Walemavu na Watoto (IDYDC) mkoani Iringa, Jonnie Nkoma akimweleza Katibu Mkuiu wa TFF, Angetile Osia juu ya kituo kipya cha Iringa Football for Hope Centre kitakachozinduliwa wiki hii ili kukuza vipaji vya watoto na Vijana mkoani humo. Kushoto ni Mwanachama wa Tabata Veteran, Ipyana Mwakasege.
Picha na Mpoki Bukuku