Thursday, 10 October 2013

BREAKIN NEWZZZZ!! PENNY AKIMBIZWA HOSPITALI LIVE!!hos

Penny Akimbizwa Hospital Baada Ya Kuona Picha Za Wema Na Diamond …Story zilizopo ni juu ya msanii wa bongo Fleva Daimond anavyo endelea kuwachanganya wasichana wa kibongo na hii ni mpya kabisa  baada ya Penny kuzidiwa pale alipoona picha muda mfupi uliopita kwenye mitandao ya kijamii, Kuwa Diamond na Wema wako wote kwa mara nyingine tena  apo ndipo ikampelekea  Dvj Penny kupoteza fahamu na kukimbizwa Hospitali.

WAZIRI  AFUNGUKA KUHUSU KUFUNGIWA KWA MAGAZETI MAWILI NCHINI!!!Mheshiwa Dkt. Fenella Mukangara
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARIIdara ya Habari – MAELEZO, inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kwamba Mheshiwa Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo amepokea maombi kutoka kwa wamiliki wa Magazeti ya Mwananchi na Mtanzania wakiomba kupunguziwa adhabu au kusamehewa adhabu wanazozitumikia kuanzia 27 Septemba, 2013.

Wakati Mheshiwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo anatafakari maombi hayo, amesikitishwa kuona kwamba magazeti haya mawili yamekiuka masharti ya adhabu walizopewa.

Wamiliki wa Gazeti la Mtanzania baada ya kufungiwa wameamua kuligeuza gazeti la kila wiki la RAI kuwa la kila siku bila ya kibali cha Msajili wa Magazeti. Kwa mujibu wa ratiba ,gazeti la RAI linapaswa kutoka kila siku ya Alhamisi.

Wamiliki wa gazeti la Mwananchi nao wameendelea kuchapisha gazeti hilo katika mtandao kinyume na agizo la kufungiwa.

Serikali inawataka wamiliki wa vyombo habari nchini kuwa na utamaduni wa kutii sheria za vyombo vya habari zinazotumika wakati huu. Hivyo serikali kwa mara nyingine tena inawataka wamiliki wa Gazeti la MTANZANIA, kuzingatia ratiba yao ya kutoa gazeti lao kila siku ya ALHAMISI.

Aidha, serikali inawataka wamiliki wa Gazeti la Mwananchi kuacha mara moja kuchapisha gazeti lao katika mtandao kama amri ya kufungiwa ilivyoanisha.

Imetolewa na,
Idara ya Habari – MAELEZO
10 Oktoba, 2013