WATUMISHI HOUSING COMPANY, BENKI YA CRDB WATIA SAINI MKATABA WA MIKOPO YA NYUMBA KWA WATUMISHI WA UMMA
Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambo (kulia), akitia saini mkataba huo. Kutoka kushoto ni Chief Operation Officer wa WHCTZ, Weja Ng'olo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Oscar Mgaya, Mkurugenzi wa Watumishi Housing Company, Dk.Fred Msemwa na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Charles Kimei.
Hapa hati zikioneshwa kwa wanahabari baada ya kusainiwa.
Mkurugenzi wa Watumishi Housing Company, Dk. Fred Msemwa akizungumza katika mkutano huo.
wadau kutoka benki ya CRDB na Watumishi Housing Company wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
TAASISI ya Watumishi Housing Campany (WHC ),imeingia mkataba na Benki ya CRDB ikiwa ni katika kuwawezesha watu wa hali ya chini kupata mikopo ya nyumba bora kwa bei nafuu.
Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi Mkurungezi wa wa taasisi hiyo, Dk.Frank Msemwa alisema wameamua kuanzisha mikopo ya nyumba za bei nafuu ikiwa ni mkuinua watu wenye vipato vidogo.
Dk Msemwa alisema tayari wameshalenga soko la nyumba nchini watajenga nyumba zenye gharama nafuu ambazo kila mtu ataweza kukopa.
"Zitakuwa ni nyumba bora na kwa gharama nafuu kabisa kila mtu ambaye anakipato ataweza kukopa nyumba hizo," alisema Dk Msemwa.
Alisema mahitaji ya nyumba nchini ni zaidi ya bilioni 1.9 ambapo kwa jiji la dar es salaam pekee hitaji la nyumba ni laki nne kwa kila mwaka.
Naye Mkurugenzi wa CRDB Charles Kimei alisema Dira ya taifa inaangalia nymba ikiwani kama azina ya kudumu na isiyo haribika huivyo ni vyema watu wakawekeza kwenye nyumba.
Alisema nyumba nzuri ni matokeo ya watoto wenye uelewa mzuri shuleni kwani hupata sehemu safi kwa kujisomea .
"CRDB ilikuwa ikikopesha nyumba ila si kwa njia rahisi kama hii inayoanza leo hivyo watu waje kwa wingi kukopa nyumba ambazo ni bora,"alisema Kimei.