Thursday 15 October 2015

IMG_8050

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akipokea wageni nyumbani kwake kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa jijini Dar.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

IMG_8060

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (katikati) akimtambulisha mmoja wa wageni waalikwa kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo (kulia).

IMG_8109

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini, Joyce Mends-Cole (kulia) akifurahi jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (kushoto) wakati wa zoezi la kupokea wageni waalikwa kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa Tanzania. Katikati ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues.

IMG_8121

Wageni mbalimbali wakiendelea kuwasili na kupokelewa na wakuu wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.

IMG_8163

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Alvaro Rodriguez (kushoto) akiongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim mara tu alipowasili kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini.

IMG_8144

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo (kulia) akifurahi jambo na mmoja wa wageni waalikwa. Katikati ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez.

IMG_8326

Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy pamoja na Katibu wa Dkt. Mahadhi wakiwa kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.

IMG_8315

Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akisherehesha mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.

IMG_8347

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa Tanzania, nyuma yake ni wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa Tanzania.

IMG_8350

Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Liberata Mulamula, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez wakitazama moja ya 'Documetary' ya Malengo Endelevu ya dunia katika mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.

IMG_8387

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim akitoa salamu za Serikali ya Tanzania kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nyuma yake ni baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo.

IMG_8401

Msaidizi wa Mh. Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Hoyce Temu na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Naibu Waziri huyo.

IMG_8353

Sehemu ya wageni waalikwa, wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Mabalozi, viongozi wa Serikali pamoja na wadau wa maendeleo waliohudhuria mnuso huo.

IMG_8357

Cake maalum iliyoandaliwa kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini.

IMG_8408

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim wakifanya 'cheers' ya kutakiana afya njema na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

IMG_8411

Tunywe kwa afya.

IMG_8432

Fataki zikipamba mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.

IMG_8427 IMG_8449

Balozi wa Umoja Ulaya nchini, Mh. Filiberto Sebregondi (kulia) na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues wakibadilishana mawazo na baadhi ya waalikwa kwenye mnuso huo.

IMG_8548

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akibadilishana mawazo na Balozi wa Umoja Ulaya nchini, Mh. Filiberto Sebregondi kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini.

IMG_8579

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim wakikata cake ya birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.

IMG_8587

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim akiendelea na zoezi la kukata vipande vya cake huku baadhi ya wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa wakishuhudia zoezi hilo.

IMG_8598

Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akifurahia picha pale camera ya Modewjiblog ilipommulika.

IMG_8612

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim akifurahi jambo na viongozi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania.

IMG_8487

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo, Mkurugenzi Mtendaji wa MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS Bw. Walter Bugoyam pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem.

IMG_8402

Wageni waalikwa katika picha ya pamoja.

IMG_8457

Kiongozi wa Mabalozi na wawakilishi wa nchi mbalimbali Tanzania Balozi Juma Mpango kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akibadilishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo.

IMG_8662

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Bi.Tonia Kandiero kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.

IMG_8474

Waalikwa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakiendelea kupata viburudisho katika mnuso wa kukata na shoka wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.

IMG_8476

Usia Nkhoma Ledama na Naibu Mkurugenzi Mkazi-Oparesheni wa UNDP, Bw. Titus Osundina wakifurahi kwenye mnuso huo.

IMG_8652

Musa Haji wa YUNA na Phillip Musiba wa UNIC Dar es Salaam kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.

IMG_8490

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole (katikati) akipozi kwa picha na baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wadau wa maendeleo.

IMG_8636

Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akibadilishana mawazo na Balozi wa Umoja Ulaya nchini, Mh. Filiberto Sebregondi.

IMG_8469

Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo na kuendelea kuburudika kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.

IMG_8648

IMG_8452

Wageni waalikwa wakiendelea kubadilishana mawazo.

IMG_8732

Hoyce Temu (wa pili kulia) na Usia Nkhoma Ledama (kushoto) wakipata picha ya ukumbusho na wadau wa MISA-TAN pamoja na UTPC.

IMG_8742

Dada Petra Karamagi na Zoe Glorious wa ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania wakipata picha ya ukumbusho.

IMG_8761

Pichani juu na chini Vijana wa YUNA katika picha ya kumbukumbu.

IMG_8782

IMG_8670

Balozi wa Umoja Ulaya nchini, Mh. Filiberto Sebregondi akibadilishana mawazo na wafanyakazi wa East Africa Radio Nasser Kingu (kulia) na Isaac Lukando (katikati).

IMG_8787

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kutoka kushoto ni Petra Karamagi, Laurean Kiiza na Beatrice Mkiramweni wakipata ukodak.

IMG_8659

IMG_8617

Mshauri wa masuala ya Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa UN Tanzania, Bi. Chitralekha Massey, Mkurugenzi Mtendaji wa MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS Bw. Walter Bugoya, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Valerie Nsoka pamoja na Mwandishi wa Habari mkongwe Mama Eda Sanga wakipozi kwa picha kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa.

IMG_8673

Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulida Hassan (kulia). akipozi na familia ya Usia Nkhoma Ledama (wa pili kulia)

IMG_8680

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakipozi na Familia ya Usia Nkhoma Ledama.

IMG_8697

Kutoka kushoto ni Mzee Mushi na Petra Karamagi (katikati) wa ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwenye mnuso huo.

IMG_8831

Wageni waalikwa katika picha ya pamoja.

IMG_8844

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na wnahabari.

IMG_8700

Wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika picha.

IMG_8711

Kutoka kushoto ni Prosper Makene, Hoyce Temu, John Badi na Lauren Kiiza wakipata Ukodak.

IMG_8492

Burudani mbalimbali zikiendelea kusherehesha birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.

IMG_8527

IMG_8646

Baadhi ya waandishi wa habari katika picha ya pamoja.