| Baadhi ya wana CCM waliohudhuria mkutano huo. | 
| Mfanyabiashara Davis Mosha akitangaza uamuzi wake wa kutojihusisha tena na siasa,uamuzi uliosababisha wanaccm kushindwa kujizuia na kuanza kuangua vilio. | 
| Baadhi ya wana CCM wakilia kwa uchungu mara baada ya Davis Mosha kutangaza kutogombea tena Ubunge . | 
| Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro,Michael Mwita alilazimika kwenda kumuomba kubadili uamuzi wake huo. | 
| Vilio havikuwa kwa wanawake peke yao hata wanaume walishindwa kuvumilia. | 
| Wengine walitishia kujinyonga mbele yake. | 
| Uamuzi wa Davis Mosha kuamua kutogombea tena Ubunge unatokana na kile alichodai kuwa baadhi ya viongozi wa CCM kushiriki kumuhujumu katika harakati za kuwania ubunge. | 
| Wengine sura zao zilibadilika zikawa tofauti na zile tulizozizoea. | 
| Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Moshi,Elzabeth Minde aliingilia kati kujaribu kuomba Mosha kubadili uamuzi wake huo bila ya mafanikio. | 
| Wanaccm wengine walilazimika kupanda jukwaani bado walizuiliwa. | 
| Wengine walizimia na kupatiwa msaada wa huduma ya kwanza. | 
| Mosha aliondolewa uwanjani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi kutokana na wanachi walioonekana kutofurahishwa na uamuzi wake huo. | 
| Msafara wake ulisindikizwa na askari Polisi. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. | 
 
 
 
