Monday 12 October 2015

KAMPUNI YA SIMU YA TECNO YAZINDUA SIMU MPYA YA PHANTOM 5 WENGI WAICHANGAMKIA


  Meneja Mauzo wa Simu za Tecno, Fred Kadilana akionesha simu aina ya Phanton 5 wakati wa uzinduzi wa tolea jipya la simu hizo uliofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Wadau mbalimbli wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Uzinduzi wa simu hiyo toleo jipya ukiendelea.

 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
  Meneja Mauzo wa Simu za Tecno, Fred Kadilana  (kulia), akiwagawia zawadi ya simu hiyo baadhi ya waandishi waliouliza maswali mbalimbali.
 Wanahabari wakipokea zawadi ya simu hiyo ya kisasa toleo jiopya.

Na Dotto Mwaibale

MAKAMPUNI yanayozalisha Simu nchini yameshauriwa kuhakikisha wanakuwa wabunifu katika kusanifu na kulizasha simu bora ili kwenda sambamba na soko la dunia.

Wito huo umetolewa na Meneja mauzo wa simu za Tecno, Fred Kadilana wakati wa uzinduzi wa tolea jipya la simu ya Phantom 5 uliofanyika Dar es Salaam juzi.

Kadilana alisema soko la bidhaa zao linakuwa kwa kasi hususan barani Afrika hivyo wanafanya jitihada kuhakikisha wanakwenda sambamba na soko la dunia.

"Soko la dunia linakuwa kwa kasi na hata bidhaa zetu pia hivyo tunajitahidi kila kukicha kwenda sambamba na ukuaji wa mahitaji ya wananchi," alisema Kadilana.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa kampuni hiyo, Daniel Xu alisema falsafa ya kutengeneza simu bora ni kulenga mahitaji ya soko la dunia.

Alisema simu ya Phanthom 5 ni toleo linalowapa wateja usanifu wa kipekee wenye uwezo 32GB katika uhifadhi wa taarifa na pia 3 GB katika mfumo wa kusoma na kuperuzi katika simu kwa haraka zaidi.

"Simu hii ina uwezo wa 300m Ah katika betri lake hivyo kuondoa usumbufu wa kuchaji simu mara kwa mara," alisema Xu.

Xu alisema kutokana na changamoto za kidunia simu hiyo ina uwezo wa kufurahia mawasiliano katika mazingirq mbalimbali.

Aliongeza kuwa kwa kuzingatia ubora Tecno imeweza kushinda tuzo ya dunia kwa ubora na kwa sasa wanaongoza kwa mauzo kwa kipindi cha miaka mitano sasa barani Afrika.