Tuesday, 2 September 2014


 AHMED Z. MSANGI – SACP-KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
---

KATIKA TUKIO LA KWANZA:


MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FUNUA MAGOKO (35) MKAZI WA ITUMBI ALIUAWA KWA KUPIGWA FIMBO SEHEMU ZA KICHWANI NA WATU WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. LUGANO GEORGE (33) NA 2. MOSSES MWACHILA (30) WOTE WAKAZI WA ITUMBI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA.


TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 00:30 HUKO KATIKA KIJIJI CHA ITUMBI, KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILO NI KULIPA KISASI KWANI INADAIWA KUWA MAREHEMU NA WENZAKE WANA TUHUMIWA KUHUSIKA KATIKA TUKIO LA MAUAJI.