Thursday, 25 September 2014

 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Sarah Brown, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza na Mwenyekiti Mtendaji wa Global Business Coalition for Education muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa ‘Getting Serious About Results: The Grand Convergence of Education and Health” ulioandaliwa na Taasisi ya Mama Sarah Brown kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa. Mkutano huo umefanyika huko New York tarehe 23.9.2014.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Bwana Gordon Brown kabla ya kuanza mkutano uliozungumzia mambo ya elimu na afya kwa vijana duniani tarehe 23.9.2014. 
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza wakati wa mkutano uliojadili masuala ya elimu na afya kwa vijana duniani huku viongozi wengine mashuhuri wakisubiri kuzungumza. Kushoto kwa Mama Salma ni Dkt. Rajiv Shah, Afisa Mtendaji kutoka USAID, akifuatiwa na Bwana Mark Dybul, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Fund to fight AIDS na wa mwisho ni Bwana V. Shanker, Afisa Mtendaji Mkuu wa Afrika, Mashariki ya Kati, Ulaya na Marekani kutoka Standard Chartered. 
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa :’Getting serious about Results: The Grand Convergence of Education and Health’ ambao ulizungumzia mambo ya elimu na afya kwa vijana hapa duniani. Mkutano huo ilifanyika huko New York tarehe 23.9.2014.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Dkt. Sarah Maongezi, Mkurugenzi wa Idara ya Afya katika Taasisi ya WAMA muda mfupi kabla kuanza mkutano huo.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Dkt. Andy Shih, Makamu wa Rais Mwandamizi anayeshughulikia masuala ya sayansi kutoka katika Shirika la ‘Autism Speaks” (masuala ya usonji) wakati mgeni huyo alipomtembelea Mama Salma kwenye hotelin aliyofikia huko New York, nchini Marekani tarehe 23.9.2014