Thursday, 17 January 2013

 Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akifurahia jambo na Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume Mabadiliko ya Katiba jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Jan 16, 2013). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya. Kushoto ni Mwenyekiti Jaji Joseph Warioba na kulia ni Mjumbe wa Tume Dkt. Salim Ahmed Salim, Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid.
 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akibadilishana mawazo na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Jan 16, 2013). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya
 Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa (kulia) akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani (katikati) na Dkt. Salim Ahmed Salim. Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo (Jumatano, Jan 16, 2013) jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya
 
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Cleopa Msuya akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu mchakato wa Katiba Mpya leo (Jumatano, Januari 16, 2013) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba.Picha na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
THE HAGUE, Netherland, January 16, 2013/ -- ICC Prosecutor Fatou Bensouda (http://www.icc-cpi.int) today formally opened an investigation into alleged crimes committed on the territory of Mali since January 2012. This decision is the result of the preliminary examination of the Situation in Mali that the Office had been conducting since July 2012.
“Since the beginning of the armed conflict in January 2012, the people of Northern Mali have been living in profound turmoil” said Prosecutor Bensouda. “At each stage during the conflict, different armed groups have caused havoc and human suffering through a range of alleged acts of extreme violence. I have determined that some of these deeds of brutality and destruction may constitute war crimes as defined by the Rome Statute”
Following the referral of the Situation in Mali by the Malian State, the Office may investigate and prosecute any crime within the ICC jurisdiction committed on the territory of Mali since January 2012. In the course of the preliminary examination, the Office has identified potential cases of sufficient gravity to warrant further action.
Prosecutor Bensouda has determined that there is a reasonable basis to believe the following crimes were committed: (i) murder; (ii) mutilation, cruel treatment and torture; (iii) intentionally directing attacks against protected objects; (iv) the passing of sentences and the carrying out of executions without previous judgement pronounced by a regularly constituted court; (v) pillaging, and (vi) rape. 
“My Office will ensure a thorough and impartial investigation and will bring justice to Malian victims by investigating who are the most responsible for these alleged crimes”.
Based on the information gathered to date, the investigation will focus on crimes committed in the three northern regions of Mali.
“There is still turmoil in North Mali and populations there continue to be at risk of yet more violence and suffering” said Prosecutor Bensouda. “Justice can play its part in supporting the joint efforts of the ECOWAS, the AU and the entire international community to stop the violence and restore peace to the region. Key regional and international organizations have acknowledged the need for justice as part of the resolution of the crisis in Mali. The international crimes committed in Mali have deeply shocked the conscience of humanity.”
Distributed by the African Press Organization on behalf of the International Criminal Court.
Background
Contact:
SOURCE 
International Criminal Court -
 Office of the Prosecutor
Balozi wa Uingereza anayemaliza muda wake Mhe. Diane Corner akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Kitabu cha historia ya Uendeshaji Jeshi la Wananchi wa Tanzania kilichoandikwa kwa ushirikiano wa wataalamu wa historia kutoka JWTZ na ubalozi wa Uingereza, wakati balozi huyo alipokwenda kumuaga ikulu jijini Dar es Salaam Jana bada  ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi nchini. Picha na Freddy Maro-Ikulu


Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Jumanne Nyamlaniakionyesha fomu
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Jumanne Nyamlani akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania leo asubuhi.Picha na Dande Francis
---
Wadau watatu wa mpira wa miguu wamechukua fomu za kuwania urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kufanya idadi ya waliojitosa katika uchaguzi huo utakaofanyika Februari 24 mwaka huu kufikia 30.

Hata hivyo, idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za TFF, kwani vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.

Waliochukua leo (Januari 16 mwaka huu) kuwania urais ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Jumanne Nyamlani, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA), Jamal Emil Malinzi na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kigoma, Omari Mussa Nkwarulo.

Mwengine aliyechukua leo ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), Elias Mwanjala anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kuwakilisha Kanda ya Iringa na Mbeya.

Orodha kamili ya wadau waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF ni Athuman Jumanne Nyamlani, Jamal Emil Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais), Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (umakamu wa rais).

Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).

Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo na Elly Mbise (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).

Athuman Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es Salaam).

Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF mpaka sasa ni wawili tu. Yusuf Manji amechukua fomu ya uenyekiti wakati Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti.

WAHARIRI, WAANDISHI WAPIGWA MSASA KANUNI ZA UCHAGUZI
Wahariri na Waandishi wa Habari zaidi ya 40 wameshiriki kwenye semina kuhusu Kanuni za Uchaguzi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyofanyika leo (Januari 16 mwaka huu).

Wawezeshaji katika semina hiyo iliyofanyika ofisi za TFF walikuwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Deogratias Lyato na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)  Mstaiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa 

 Mstaiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa amewakaribisha na kuwaeleza jinsi walivyoweza na wanavyoendelea kukusanya mapato.

Mstaiki Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula na ujumbe wa kamati yake ya fedha wametembelea halmashauri ya manispaa ya Ilala kwa maagizo ya Mhe.Waziri Mkuu kuja kujionea mbinu za kisasa za kukusanya mapato.
--
Mstaiki meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula na ujumbe wa kamati yake ya fedha wametembelea halmashauri ya manispaa ya Ilala kwa maagizo ya Mhe.Waziri Mkuu kuja kujionea mbinu za kisasa za kukusanya mapato.
Mstaiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa amewakaribisha na kuwaeleza jinsi walivyoweza na wanavyoendelea kukusanya mapato.
SOURCE:haki ngowi