Makamu
 wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, aliendelea 
na Ziara yake ya jana hapa nchini Uingereza. Mheshimwa Seif, jana 
alikutana na Waziri wa Uingereza anashugulikia maswala ya Afrika Bw. 
Mark Simmonds. Kwenye mazungumzo yao walibadilishana mawazo kuhusu 
maswala ya Tanzania na hususan hali ya kisiasa ya Zanzibar, mazungumzo 
hayo yalihudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, 
Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe. Vile vile Mheshimiwa Makamu wa Rais, 
aliweza kukutana na Mabalozi wa nchi za Afrika ya Mashariki na Viongozi 
wa Jumuiya ya Waingereza waliowahi kuishi Tanzania, ijulikanayo kama 
Britain Tanzania Society (BTS).
Leo
 hii siku ya Ijumaa, Jioni, kuanzia Saa 18:00pm mpaka saa 21:00, 
Mheshimiwa Makamu wa Rais atakutana na Watanzania wote waishio London, 
katika Ukumbi wa University of London Union, Mtaa wa Malet Street, WC1E 7HY
Watanzania wote wenye nafasi ya kufika mnakaribishwa.
Watakao hudhuria mnaombwa sana kuzingatia muda uliopangwa.
Makamu
 wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Seif Sharif Hamad, siku ya Alhamisi
 tarehe 14/9/12 alikutana na Waziri wa Uingereza anashugulikia maswala 
ya Afrika Bw. Mark Simmonds. Kwenye mazungumzo yao walibadilishana 
mawazo kuhusu maswala ya Tanzania na hususan hali ya kisiasa ya 
Zanzibar, mazungumzo hayo yalihudhuria na Balozi wa Tanzania nchini 
Uingereza, Balozi Peter Kallaghe
Makamu
 wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, akiwa pamoja
 na Mabalozi wa nchi za Afrika ya Mashariki. Mheshimiwa Seif alikutana 
na Mabalozi hao jana kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, London. 
Katikati
 ya picha ni Mheshimiwa, Makamu wa Rais, Balozi wa Tanzania, Mheshimiwa 
Peter Kallaghe (kushoto), Balozi wa Rwanda, Mheshimiwa Ernest Rwamucyo 
(Pili kushoto), Balozi wa Uganda, Mheshimiwa Joan Rwabyomere (Pili 
kulia), na Balozi Mdogo wa Burundi, Mheshimiwa Bernard Ntahiraja (Kwanza
 kulia).
Makamu
 wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, akisalimiana na 
Viongozi na Wawakilishi wa Jumuiya ya Waingereza walio wahi kuishi 
Tanzania (Britain Tanzania Society). Aliyepewa mkono na Mheshimiwa 
Makamu wa Rais ni Bwana  David Brewin Mhariri wa Jarida la kila mwezi 
linalotolewa na BTS,  Mama Liz Fennell, Makamu wa Rais BTS (mbele 
kulia), Mama Valerie Leach - Katibu (kwanza kushoto), Bwana Dan Coo- 
 Mwanachama BTS, Bwana Ron Fennel, Afisa wa Miradi ya BTS kwa Tanzania 
na Bwana Andrew Coulson, Afisa Mkuu wa Mipango ya Jumuiya hiyo ya BTS.
 
 
 
