Friday 28 September 2012

 

MAGEREZA SASA WAONGEZEWA VITENDEA KAZI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Fanuel Mbonde ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla fupi ya kukabidhi mabasi kwa Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Fidelis Mboya kwa niaba ya Jeshi la Magereza. Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria iliyopo ndani ya Wizara ya Katiba na Sheria imekabidhi magari 12 kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kubeba mahabusu pamoja na kusindikiza msafara wa mahabusu wanapopelekwa mahakamani na kurudishwa gerezani. Hafla hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Gereza la Keko, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wa pili kutoka kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Fanuel Mbonde (wa tatu kutoka kulia) wakikagua sehemu ya magari madogo yaliyokabidhiwa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa ajili ya kusindikiza msafara wa mabasi yanayosafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani
Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia) akipokea funguo ya basi la mahabusu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Fanuel Mbonde katika fupi ya kukabidhi mabasi kwa Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Fidelis Mboya kwa niaba ya Jeshi la Magereza. Programu ya Maboresho katika Sekta ya Sheria iliyopo ndani ya Wizara ya Katiba na Sheria imetoa magari madogo matano na mabasi saba kwa ajili ya kusafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika leo katika viwanja vya Gereza la Keko, jijini Dar es Salaam.
             IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
       WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.