Saturday 11 March 2017

“RC SHIGELLA AITAKA TEMESA KUMPATIA ORODHA YA WADAI SUGU”


Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akisisitiza jambo wakati akifungua kikao cha Bodi ya Barabara (Road Boad) ambapo alisisitiza umuhimu wa wabunge wa mkoa wa Tanga kutumia nafasi zao kusaidia kuelezea changamoto zinazozikabili barabara zetu ili zipewe msukumo
Meneja wakala wa barabara Mkoani Tanga (Tanroad) Mhandisi Alfred Ndumbaro akisisitiza jambo kwenye kikao hicho kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu
Meneja wa Temesa Mkoa Mhandis Margareth Gina akitolea ufafunzi baada ya maswali yaliyoulizwa na wajumbe wa kikao hicho

 Wajumbe wakifuatilia hoja zilizoainishwa kwenye makabrasa kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kilindi (CCM) Omari Kigua na Mkuu wa wilaya ya Kilindi Sauda Mtondoo
 Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso akifuatilia jambo kwenye kabrasha lake wakati kikao hicho kikiendelea
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji katika wakati wa kikao hicho
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto,Kazimbaya Makwega akiperuzi kabrasa kwenye kikao hicho
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Musa Mbaruku na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba
 Mbunge wa Jimbo la Mkinga(CCM) Dustan Kitandula kushoto akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Rashid Gembe
 Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akifuatilia kwa umakini kikao hicho
 kulia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda akifuatilia kikao hicho
 Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo akifuatilia kwa umakini kikao hicho
 Mwandishi Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji la TBC Mkoani Tanga,Bertha Mwambela akiandaa taarifa za kikao hicho
WAKALA wa Ufundi na Umeme Mkoani Tanga (Temesa) wameagizwa kuwasilisha orodha ya majina ya wadaiwa sugu wa taasisi mbalimbali za serikali kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa ikiwemo kuharakisha ulipwaji wake.
Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela wakati wa kikao cha kwanza cha Bodi ya barabara mkoani hapa ambapo alisema wao kama serikali ya mkoa hawapo tayari kuona wakala huyo akishindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo kutokana na juhudi zao kurudishwa nyuma kimaendeleo.

Katika kuhakikisha suala hilo linapata mafanikio makubwa yenye tija alimtaka Meneja wa wakala wa Ufundi na Umeme (TEMEMSA) Mkoa Tanga, Mhandisi Margareth Gina kumpelekea idadi ya wadaiwa sugu na taasisi hiyo ili kuweza kuangalia namna ya kuweza kupata malipo yao.

Hatua hiyo inafuatia taarifa ya Meneja wa Temesa Mkoa kuonyesha zipo taasisi nyingi za Serikali zinazodaiwa fedha nyingi bila kuwepo jitihada zozote za ulipwaji wa madeni hayo huku tasisi hizo zikiendelea kupatiwa huduma na taasisi hiyo ya Serikali.

Alisema ifike wakati kwa taasisi zote za umma zinazopata huduma kutoka kwa wakala huo wa ufundi na umeme wahakikishe wanalipa madeni yao kwa wakati kabla majina hayo ya wadaiwa hao sugu hayaja wekwa hadharani.

Mkuu huyo alisisitiza umuhimu wa majina ya wadaiwa wote sugu
yaorodhoshwe bila ya kuoneana aibu na taasisi za Serikali ambazo inadaiwa kuwa ndio vinara wakubwa wa kudaiwa ili kuweza kuangalia namna ya kupunguza madeni hayo ambayo ni hatari kwa ukuaji wa wakala huyo.

Awali akizungumza katika kikao hicho,Meneja wa Temesa Mkoa Mhandis Margareth Gina alisema temesa imekuwa ikitoa huduma bora kwa taasisi za Serikali kutokana na kuwepo na wataalamu wengi waliobobea katika fani mbalimbali huku wakishindwa kufikia malengo kutokana na kutolipwa
na wateja wao.

Mhandisi Gina alisema ipo orodha kubwa ya majina ya wadaiwa sugu ambapo ipo haja ya kuyaweka hadharani kama Mkuu wa Mkoa alivyoagiza na kufanya hivyo kunaweza kusaidia kwa namna moja au nyingine kuweza na kukusanya madeni hayo.

“Zipo taasisi za serikali zanadaiwa hadi milioni 100 na orodha yote ya wadaiwa sugu ninayo na naweza kuyataja ila naona itakuwa kufedheheshana tu mbele ya kikao hiki”Alisema

Aidha alisema taasisi za Serikali kwa asilimia kubwa zimekuwa miongoni mwa wateja wanaoikwamisha temesa kuendelea na ufanisi wa shughuli zake jambo ambalo linatakiwa litafutiwe ufumbuzina wa haraka kukomesha tabia hiyo iliyozoeleka.

Kwa upande wake, katibu Tawala Mkoa Tanga Mhandisi Zena Saidi alisema hakuna sababu ya kuficha wanaodaiwa lazima waorodheshwe na walipe madeni yao kwa wakati ili temesa iweze kuendelea na majukumu yake.
habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.