Sunday, 5 March 2017

Mmoja wa washiriki wa mafunzo kwa wanahabari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Mara, Geita na Simiyu, walionufaika na mafunzo yaliyotolewa na taasisi MISA Tanzania, akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa mwakilishi wa taasisi ya FES Tanzania (katikati), iliyofadhiri mafunzo hayo.

#BMGHabari
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, imewatunuku vyeti vya ushiriki wanahabari kutoka vyombo mbalimbali katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

 Wanahabari waliopatiwa vyeti hivyo ni waliopatiwa mafunzo ya kuwajengea uelewa juu ya Sheria Mpya ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 na Kanuni zake za mwaka 2017.

Mafunzo hayo ya siku mbili yalianza juzi alihamisi na kutamatika jana katika Hotel ya Adden Pallace Jijini Mwanza, yakifadhiliwa na Taasisi ya Friedrick Ebert Stiftung (FES) tawi la Tanzania.

Akizungumza mapema kabla ya kukabidhi vyeti kwa washiriki, mwakilishi wa taasisi ya FES Tanzania, Violet John, aliwahimiza wanahabari kutumia vyema hayo vyema katika kuboresha kazi zao huku pia akiwahimiza kufikisha kwa wenzao yale waliyojifunza.

Edwin Soko ambaye ni mmoja wa wanahabari waliopatiwa mafunzo hayo, aliishukuru MISA Tanzania kwa kutambua umuhimu wa wanahabari kujifunza kuhusu Sheria Mpya ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 na Kanuni zake za mwaka 2017 na kubainisha kwamba elimu hiyo wataifikisha kwa wenzao.
Reply Reply to All Forward More