Monday, 2 March 2015

RAIS KIKWETE AONGOZA KUAGWA MWILI WA KAPTENI KOMBA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Eaus Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma, wakitoa heshima zao, wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Kapteni John Komba, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili wa marehemu Komba iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam. Baadaye mwili ulisafiriwa kwa ndege kwenda mkoani Ruvuma kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho katika kijiji Lituhi. 
 Rais Kikwete akimfariji mjane wa Kapteni Komba, Salome Mwakangale Komba, baada ya kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Komba
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa heshima kwa mwili wa Kapteni John Komba leo, Karimjee jijini Dar es Salaam
 Salome Mwakangale Komba akitoa heshimaa za mwisho kwa aliyekuwa mumewe, Kapteni John Komba, wakati wa shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili huo, leo jijini Dar es Salaam
 Baada ya heshima akaubusu mwili wa aliyekuwa mumewe
 Binti wa Marehemu Komba akisaidiwa kutoa aheshima za mwisho
 Mtoto wa Kapteni Komba akitoa heshima za mwisho
 Mmoja wa waombolezaji akitoa heshima  za mwisho
 Muombolezaji akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu
 Makamu wa Rais Dk. Muhammed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Kapteni Komba
 Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akitoa heshima za mwisho
 Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akitoa heshima za mwisho
 Spika wa Bunge Anna Makinda akitoa heshina za mwisho
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akitoa heshima za mwisho 
 Katibu wa NEC, SUKI, CCM, ambaye pia ni Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro akitoa heshima za mwisho
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, CCM, Nape Nnauye akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa John Komba 
 Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho
 Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Yussuf Makamba akitoa heshima za mwisho
 Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia akitoa heshima za mwisho
 Mwenyekiti wa Kampuni za UPP Reginald Mengi akitoa heshima za mwisho
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akitoa heshima za mwisho
 Katibu wa NEC, CCM, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib akitoa heshima za mwisho
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa John Komba
 Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Komba 
 Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Maduni, Profesa Sospeter Muhongo akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa John Komba

Umati wa watu ukiwa kwenye shughuli hiyo ya kutoa heshima za mwisho
Umati a wananchi kwenye foleni ya kutoa heshima za mwisho 
 Mwili wa Kapteni Komba akiingizwa katika gari baada ya kuagwaa, tayari kwenda Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam, kwenda kwenye mazishi katika Kijiji cha Lituhi mkoani Ruvuma 
 Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilibroad Slaa akipitia ratiba wakati wa shughuli a kuaga mwili wa kapteni Komba 
 Mzee Mkapa akisalimiana na Mzee Mangu walipowasili kwenye Viwanja vya Karimjee
 Mzee Mkapa akimsalimia Katibu Mkuu wa CCM, Mzee Kinana alipowasili kwenye viwanja wa Karimjee 
 Waombolezaji
 Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kim,ataifa, Bernard Bembe akimsalimia Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Pius Msekwa alipowasili iwanja vya Karinmjee 
 HIYO SAWA: Mzee Mkapa anaonekana kana anasema hivyo kumwambia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana walipokuwa wakibadilishana mawazo kwenye viwanja vya Karimjee wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa Kapteni Komba 
 Jeneza lenye mwili wa John Komba lilipowasili kwenye Viwanja vya Karimjee
 Rais Jakaya Kikwete na viongozi wengine wakiwa wamemama kwa heshima ya kuwasili mwili huo wa marehemu Komba
 Rais Kikwete akitafakari jambo baada ya mwili wa kapteni Komba kuwasili Viwanja vya Karimjee
 Mwakilishi wa Mkuu wa Kambni a Upinzani Bungeni, Mbunge Joshua Nasari akizungumza kwa niaba ya kambi hiyo
 Nasari akimsalimia kwa heshima Rais Kikwete baada ya kutoa salam
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo a Jamii Saidi Mtanda, akitoa salam za Kamati hiyo. Komba alikuwa Makamu Mwenyekiti katika kamati hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasilisha salam za CCM wakati wa shughuli hiyo ya kuagwa mwili wa John Komba
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Mzee Kingi Kiki, wakiongoza baadhi ya wasanii kuimba wimbo maalum wa maombolezo ya kifo cha Kapteni John Komba wakati wa shughuli hiyo ya kuaga mwili huo
 Ana Makinda akitoa salam kwa niaba ya Bunge
 Baadhi ya watunmishi wa CCM wakiwa kwenye shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Komba
 Wasanii wakiimba wimbo maalum wa maombolezo. Picha zote na Bashir Nkoromo, theNkoromo Blog