Wednesday, 25 March 2015

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale akizungumza na Wataalamu washauri mbalimbali wa Sekta ya barabara nchini (hawapo pichani) kuhusu upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa ubia wa barabara ya Dar es salaam – Chalinze utakaoendeshwa kwa ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi (PPP).

 Kiongozi wa jopo la Wataalamu washauri kutoka Korea, Kunho-Jung, akifafanua jinsi mradi huo utakavyoendeshwa kwa ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi (PPP).

Wataalamu washauri kutoka Sekta ya barabara wakiwa katika mkutano kujadili upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa ubia wa barabara ya Dar es salaam – Chalinze utakavyokuwa. Ujenzi wa barabara hiyo utahusisha barabara sita (6) kutoka Dar es salaam – Mlandizi na barabara nne (4) kutoka  Mlandizi- Chalinze.

Jopo la Wataalamu washauri kutoka Korea wakimsikiliza kwa makini mtoa mada (hayupo pichani) katika mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali ya sekta ya barabara nchini kujadili upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa ubia wa barabara  ya Dar – Chalinze.Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa kujadili kuhusu upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa ubia wa barabara ya Dar – Chalinze uliofanyika jijini Dar es salaam.