UP-DATE: Dkt Ulimboka azungumza kilicho mpata
 
 
Mweneyikiti wa Jumuia ya Madaktari nchini Dk Stephen Ulimboka, amepigwa na kujeruhiwa vibaya na watu wasiofahamika. 
Dkt
 Ulimboka anadaiwa kuvunjwa mbavu, miguu yote miwili, kung’olewa meno 
yote ya mbele na kuumizwa vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Tukio
 hilo la kikatili na kusikitisha limetokea usiku wa kuamkia leo jijini 
Dar es Salaam, na linadaiwa kufanywa na watu wa sio julikana ambapo 
kabla ya kufanya unyama huo walidaiwa kumteka na kumpiga kabla ya 
kumtelekeza katika eneo la msitu wa Pande Mabwepande.
DKT. ULIMBOKA ASIMULIA TUKIO
Akisumulia
 tukio hilo Dkt Ulimboka alisema kuwa  jana usiku alipigiwa simu na mtu 
aliyejitambulusha kwake kuwa anaitwa Hemed, aliyemwambia kuwa anahitaji 
kuongea naye, na ndipo walipopanga kuonana katika eneo la Leaders 
Kinondoni.
Dk
 Ulimboka aliyekuwa akiongea kwa tabu, aliendelea kusimulia kuwa wakati 
akiongea na mtu huyo anayekiri kuwa alikuwa akifahamiana naye kabla, 
alikuwa na wasiwasi kwani kila mara alikuwa akipokea simu na kuwasiliana
 na watu wengine ambao hawakuwapo eneo hilo.
Alisema
 baada ya muda alishangaa kuona wanaongezeka watu wengine watano wakiwa 
na silaha, kisha wakamwambia kuwa anahitajika kituo cha Polisi na 
kumvuta na kumuangusha barabarani kabla ya kumuingiza katika gari lenye 
rangi nyeusi na kuondoka naye.
Dkt
 Ulimboka alisema kuwa wakiwa njiani walimpiga, na kumfikisha katika 
msitu huo wa pande na kuendelea kumpiga paka alipoteza fahamu.
MADAKTARI NAO WALONGA
Akisimulia
 mkasa huo mmoja wa madaktari wenzie aliyefahamika kwa jina moja la Dkt 
Deo, alisema kuwa alipigiwa simu na mtu hasiyemfahamu na kumfahamisha 
tukio hilo.
Alisema
 alipofika katika kituo cha Polisi cha Bunju, alimkuta akiwa katika hali
 mbaya na ilikuwa ngumu kumtambua kwakuwa alikuwa na majeraha mengi eneo
 la usoni.
Aliongeza kuwa akiwa na wenzie waliamua kumchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya matibabu.
"Hali
 yake kwakweli ni mbaya sana, amepigwa mno na ameumizwa kwakweli 
tumemleta hapa hili aweze kupata matibabu, lakini mimi nilivyomkuta mara
 ya kwanza nilishindwa hata kumtambua kwa jinsi alivyokuwa 
ameumizwa"alisema Dkt Deo
Alisema
 kuwa alisimuliwa na Dkt Ulimboka kwamba watu hao waliomteka na kumpiga 
walikuwa na silaha na kwamba alishindwa kuwatambua.
Aliongeza
 kuwa Dkt Ulimboka alidai kuwa wakati akiwa katika halimbaya alikuwa 
akisikia mazungumzo yao, wakibishana juu ya kumuua wengine wakisisitiza 
achomwe sindano, na wengine wakitaka kumpiga risasi.
Alisema
 wakati mabishano yakiendelea kati yao, Dkt Ulimboka aliinuka akiwa na 
lengo la kukimbia lakini watu hao walipiga risasi hewani iliyomshtua na 
kuangua chini.
Kwa
 upande wake Dkt Cathbeth Mcharo ambaye ndiye aliyempokea Dkt Ulimboka 
Hospitalini hapo, alisema kuwa hali yake ni mbaya na kwamba wanajitahidi
 kumpatia huduma za haraka.
Alisema kuwa kwa hatua za awali amefanyiwa vipimo mbalimbali, hili iweze kufahamika aina ya matibabu anayotakiwa kupatiwa.
POLISI
Kamanda
 wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova 
amezungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo la utekaji nyara na
 kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka 
anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika klabu ya
 Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.
Kamanda
 Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka 
kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezi kuwa msamaria mwema 
huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa 
kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua 
maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa
 ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kamanda
 Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa 
ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni
 tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote 
watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na 
sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo 
MUHIMBILI
Wakati
 hayo yakitokea inadaiwa kuwa Askari Kanzu mmoja alikumbana na kipigo 
kikali kutoka kwa madaktari hapo Muhimbili kwa kile kilochodaiwa 
kutambuliwa na Dkt Ulimboka kuwa mmoja wa watu walio mjeruhi.
Pia
 inadaiwa kuwa Askari huyo aliingia chooni na kufanya mawasiliano na 
wenzake huku Madaktari hao wakimsikiliza na kutokana na alichokua 
akiongea chooni humo ndipo alipotoka aliambulia kichapo kikali.
Pia
 baadhi ya madkatari na wauguzi walikuwa wakisukuma gari alilokuwa 
amepanda Dkt Ulimboka huku wakiimba nyimbo za Umoja na Mshikamano Daima 
miongoni mwao.
Hali ya ulinzi ilikuwa kali Hospitalini hapo kwani Picha zilikuwa haziruhusiwi kupigwa.
 
 
 
