Saturday 30 June 2012

Mbunge wa Korogwe Vijijini(CCM) Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu", akizungumza na waandishi habari 
 
Mbunge wa Korogwe Vijijini(CCM) Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu", akizungumza na waandishi habari 
-
Mbunge wa Korogwe Vijijini(CCM), Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu", akizungumza na waandishi habari mjini Dodoma jana, amekanusha madai kuwa alilieleza Bunge kuwa mkasa uliompata Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari na Kamati ya kufuatilia haki zao, Dkt. Steven Ulimboka, kuwa alistahili, SI YA KWELI na KUOMBA RADHI Madaktari nchini kwa jinsi alivyonukuliwa vibaya wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni tarehe 28 Juni 2012.

Jana, Mbunge huyo alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa alisema, "kipigo alichopata Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dkt. Steven Ulimboka, kinastahili ili naye apate machungu wanayopata wagonjwa wengine mahospitalini."

Kauli hiyo ilisababisha tafrani kidogo bungeni, ambapo  Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda  alilazimika kuingilia kati kumzuia Ngonyani asiendelee kutoa kauli hiyo kwa vila suala la madaktari bado liko Mahakamani. 
Nukuu Ya  Mwanzo Ya  Mbunge wa Korogwe Vijijini(CCM) Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu"
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani maarufu kwa jina la Profesa Maji Marefu (pichani),jana amesema bungeni kuwa kipigo alichopata Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, kinastahili ili naye apate machungu wanayopata waginjwa wengine mahospitalini.

Profesa Maji Marefu aliitoa kauli hiyo wakati akichangia hoja katika bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, bungeni Dodoma.

Kauli hiyo ilisababisha tafrani kidogo bungeni na  kumfanya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuingilia kati kumzuia Maji Marefu asiendelee kutoa kauli hiyo kwani jambo la madaktari bado liko mahakamani.