Friday, 7 August 2009

waraka wa kanisa katoliki Tanzania

Manufacturer of the
Year Award...

President Jakaya Mrisho Kikwete presents Presents a trophy to this year overall winner for the President's Manufacturer of the Year Award to the General Manager of Shelys Pharaceuticals Company Mr.Ashok Gupta during a colourful function held at Movenpick Hotel in Dar es Salaam last night. Others in the picture are from left the event's sponsor the NBC Managing Director Christo de Vries, The outgoing CTI Chairman Reginald Mengi(Third left) and the new CTI Chaiman Mr.Felix Mosha(Fourth left).


Waraka wa kanisa katoliki Tanzania

BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA
(TEC)
MPANGO WA KUHAMASISHA
HUDUMA YA KICHUNGAJI KATIKA JAMII
KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2010
Idara ya Kichungaji
TUME YA HAKI NA AMANI - TEC
MPANGO WA KUHAMASISHA HUDUMA YA KICHUNGAJI
KATIKA JAMII KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2010
DIRA
Mungu anakuita, anakuhitaji.
Dunia imeumbwa na Mungu ili iendelee kuwa mahala panapodhihirisha Ufalme wa wake. Ukuu wa uumbaji huu ni mwanadamu ambaye ndiye kiumbe aliyekirimiwa utashi na uelewa ili awe mshiriki na mdhamini wa kazi ya Mungu. Mungu ametuchagua tuchukue wajibu huu, na pamoja naye tupunguze uovu na taabu, na kujenga dunia ambamo upendo na maelewano vinamhakikishia kila mmoja kufurahia utu wake.
Kama wakristo, tunapokea mwaliko wa Kristu uwe mwaliko wetu.. “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa” (Lk 4: 18 – 19).
Kwa kutilia mkazo mwaliko huu, tunaelezwa kuwa Mwana wa Mtu atakaporudi atayahukumu mataifa kwa kigezo cha huduma tuliyotoa kwa wenye njaa, kiu; walio wageni, uchi, wagonjwa na wale walio kifungoni (rej. Mt. 25: 31 – 46).
Mungu alipomuumba Mwanadamu alimpa wajibu wa pekee, sio tu kuwa mlinzi na mdhamini wa dunia/uumbaji, bali pia kuwa mshiriki katika kuumba, na kutunza. Ni wito wa kushirikiana na Mungu katika kupambana ili kuuondoa uovu katika jamii yetu na kujenga ulimwengu ambamo kila mmoja ana wajibu wa kutekeleza na wakati huo huo ana haki ya kufurahia matunda ya dunia yetu.
Programu yetu ya kulihamasisha Kanisa kutekeleza wito wa kichungaji katika mambo ya kijamii ni kuwatia moyo waamini wote kutambua na kukubali wito wao wa Kikristo, wito wa kuwapelekea watu habari njema ya Yesu katika mambo ya kijamii na ya kitaifa. Kutakatifuza malimwengu, kuifanya nchi yetu na watu wetu kuishi pamoja huku manufaa ya kila mmoja yakiwa yanatimizwa: kupata huduma msingi za maisha na kuheshimiwa utu wa kila mmoja. Hapa maslahi na manufaa ya wote na ya kila mmoja katika jamii yanapaswa kuzingatiwa. Huu ni wajibu wa kila mmoja.
Mungu anakuhitaji, haya si maneno tu, bali ni uamuzi wa makusudi wa Mungu anayetukabidhi wajibu huu. Kutopokea mwaliko huu unaotoka kwa Mungu ni kushindwa kutimiza wajibu wetu, ni dhambi ya kutotimiza wajibu wa wito wetu wa Kikristo. Wito wa kutimiza wajibu wa kijamii, ambao ni kutia chachu ya tunu za injili na Mafundisho ya Kristo katika masuala na shughuli za kijamii, kiuchumi na kisiasa ya taifa letu.
Wito huu haujaeleweka vema na jumuiya zetu. Watu wengi wanadhani kwamba mambo ya umma sio sehemu ya majukumu yetu ya kidini na kiimani, na hivyo Kanisa halipaswi kujishughulisha na mambo hayo. Kinyume chake Kristo anatualika kuleta mafundisho ya Mungu, maadili ya asili yetu ya kibinadamu kama tulivyoumbwa na Mungu. Tunaalikwa kuyafanya hayo yawe ndio msingi na mwanga unaoongoza maamuzi na sera zetu.
Tunaona kwamba ikiwa maadili hayo yatakuwa sio msingi wa maisha yetu ya pamoja na kuyashuhudia katika utendaji wetu na mienendo yetu, hapo tutaingia haraka katika uovu na ubinafsi na uchoyo, mambo ambayo yanaangamiza jamii yetu.
Katika miaka ya hivi karibuni sote tumeshuhudia haya yakitokea na tumepata madhara yake katika amani na utulivu katika taifa letu. Kumekuwa na mgawanyiko miongoni mwetu, kumejengeka matabaka ya wenye mali nyingi na watu wengi ambao wana mali kidogo sana , maskini na fukara hasa . Mwelekeo huu unatishia na kuhatarisha amani na moyo wa ujamaa tuliokuwa nao na kushamiri kwa utengano na chuki kati yetu.
Sote tunawajibika kwa nchi yetu na taifa letu. Ndio maana Mungu ametujalia sote kuenzi hadhi ya utu wetu sawa. Kwa hiyo tusiruhusu nchi yetu Tanzania ikawa na watu ambao thamani ya utu wao ni zaidi ya wengine. Tusisahau kila mmoja wetu ameumbwa katika sura na mfano wa Mungu (Taz. Mwa 1: 28).
Ni kwa sababu hiyo tunazindua programu hii ya kuhamasisha jumuiya zetu kuelewa wito wao wa kijamii, kuinjilisha na kuifanya jamii yetu iwe ya kiutu kulingana na mpango wa Mungu wa uumbaji na haswa kwa jamii ya wanadamu. Msingi wa utu wa mwanadamu ni asili yetu ya kwamba tumeumbwa na Mungu. Huu ndio msingi ambao dini zote zinausadiki na kuuheshimu. Kwa hiyo tunaweza kushirikiana na waislamu, wahindu, na watu wenye kufuata dini za jadi. Sote kwa pamoja tujenge dunia yetu kulingana na mpango wa Mungu.
WITO
Tumetumwa katika jumuiya zetu, Parokia na jumuiya ndogo ndogo, kuwahamasisha watu wafanye tafakari juu ya hali halisi ya maisha na kujua ni kwa namna gani mafundisho ya Kanisa na Injili yanatupatia mwanga wa namna ya kuboresha maisha yetu na katika Taasisi za jamii yetu. Tunachukua hatua katika kurekebisha mambo yanayokwenda vibaya na kuimarisha mambo mazuri. Ni mwaliko wa kuwasaidia watu katika kutekeleza maamuzi yaliyothibitishwa katika ahadi yao waliyoweka wakati wa ubatizo.
Hatua zifuatazo zinapendekezwa kutumika katika utekelezaji:
- Kuchunguza hali, kutambua na kubaini tatizo.
- Kutumia Mwanga wa mafundisho ya Kristo na kutoka katika Mafundisho ya Kanisa kuhusu Jamii.
- Kuamua hatua ya kuchukua na namna ya kufuatilia utekelezaji.
UTARATIBU WA KUZINGATIA (METHODOLOJIA)
Programu hii ya kichungaji inahitaji uongozi mzuri na hatua madhubuti za ufuatiliaji. Hapo tutaweza kufanikiwa na kuleta matokeo katika maisha ya Jumuiya ya Kanisa na ya taifa letu.
Katika hatua ya utekelezaji wa programu hii tunapendekeza:
1) Kufanyika mikutano ya makleri na viongozi wa halmashuri walei. Ni lazima katika mkutano huu ijadiliwe programu hii katika ngazi ya Jimbo na kupewa umuhimu unaostahili.
2) Wajumbe wa Mkutano huu: Wakurugenzi wa Kichungaji na Wajumbe wa Tume ya Haki na Amani watakuwa wakufunzi – kueleza na kufafanua mada za programu yetu.
3) Katika kazi ya kuongoza mkutano (no. 1), wajumbe wa CPT na wawakilishi wa Serikali waalikwe kutoa maelezo juu ya hali halisi pale watu wanamoishi.
4) Inapendekezwa paundwe timu ya Jimbo kwa ajili ya ufuatiliaji wa programu hii.
5) Katika ngazi ya Parokia programu ilenge kufundisha wanavijiji/watu mitaani na katika Jumuiya Ndogo Ndogo ili waweze kujadili masuala yaliyomo katika programu.
6) Ripoti za majadiliano hayo zitumwe Parokiani (Paroko na Halmashauri) kila baada ya miezi mitatu. Ripoti hizo zionyeshe mambo yaliyojadiliwa na maamuzi yaliyofikiwa.
Kwa kupata uelewa zaidi mada zilizojadiliwa katika mkutano wa Wakurugenzi wa Kichungaji na Wajumbe wa Tume ya Haki na Amani (TEC) ni:
1) Vipaumbele kwa mujibu wa Mafundisho ya Kanisa kuhusu Jamii.
2) Umuhimu wa uongozi wenye maadili katika kuleta mabadiliko ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kidini katika Tanzania .
3) Mfumo wa Sheria Tanzania : Nguvu na Changamoto.
4) Haki za Binadamu katika sera za biashara na fedha.
5) Mtazamo wa kimaadili katika mfumo wa kisiasa na kiuchumi.
6) Hifadhi ya jamii.
Mada hizi zinapatikana kwa kiswahili na kiingereza, kama unazihitaji wasiliana na:
- Ofisi ya CPT - St. Josephs Cathedral Dar es Salaam
Tel: 022-2127675/ 0713-329984
E.mail: http://us.mc1102.mail.yahoo.com/mc/compose?to=cptprofessionals@yahoo.co.uk
Tunaweza pia kukusaidia kupata Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa utatujulisha mahitaji yako.
MADA KUU ZA TAFAKARI
Agenda hizi ndizo zilizoazimiwa katika Mkutano wa Wakurugenzi wa Kichungaji na Wajumbe wa Tume ya Haki na Amani TEC uliofanyika tarehe 20 – 22 Januari, 2009.
1. UTU
Utu aliokirimiwa kila mwanadamu bado haujawa ndio kiini na msingi wa mienendo yetu kama watu binafsi, katika vikundi na kama jamii. Kasoro hii tunaiona katika jumuiya za kidini, katika mila, desturi na tamaduni zetu, katika shughuli zetu za kiuchumi na katika uwanja wa kisiasa.
Kila mwanadamu ana utu sawa na utu wa mwingine na kwa hiyo lazima utu wa kila mmoja uheshimiwe na wengine: watu binafsi, taasisi na utawala.. Ikiwa mwanadamu anapewa hadhi kutokana na utu wake, na haki zake atajengeka na kuwa na utu kamili, na yeye mwenyewe atajenga uwezo wake kikamilifu.
Vile vile bila kufanya hivyo jamii yetu haiwezi kamwe kukua na kuwa jamii yenye watu wenye kuenzi ukweli, utu na usawa. Kuigawa jamii katika matabaka ni kosa na ni dhambi, licha ya kuwa huko ni kuzuia jamii kufikia uwezo wake kamili na kuwa jamii yenye furaha. Katiba ya Jamuhuri imeweka bayana kwamba haki, wajibu na uhuru wa binadamu lazima vilindwe, viheshimiwe na kutolewa sawa kwa wote.
Kwa hiyo tunapaswa kufundisha watu dira hii katika:
- Ngazi ya familia, katika ujirani na Jumuiya ndogo ndogo. Ni hapa ndipo msingi wa jamii na kanisa unapojengwa.
- Katika mashule, tuangalie upya sera zetu za elimu na malezi na upande wa kimaadili tuchunguze yaliyo katika mitaala na ratiba katika mashule. Kwa sasa hakuna msisitizo wa kutosha katika malezi ya ubora/sifa za kiutu.
- Katika mambo ya kisiasa na kiuchumi: heshima na utu wa mtu sio suala la kubaki katika maneno na hotuba nzuri na matamko. Taasisi na sheria zetu lazima zikumbuke kuwa kanuni za kimaadili yapasa ziongoze kazi yao .
- Katika ngazi za Kanisa: mkazo zaidi uwekwe katika kuwajenga watu katika mambo ya kiroho ambayo ni ya lazima katika kuongoza tabia ya kijamii. Hapa ni zaidi ya kuweka kanuni na taratibu. Kinachohitajika hasa ni roho ya kiinjili na wito wa kinabii.
Mambo yanayopendekezwa kufanywa katika kufundisha na kuhamasisha utu ni:
- Mafungo katika ngazi ya Parokia na taasisi za Kanisa.
- Mikutano na wazazi ili kuwahamasisha na kutafakari namna ya kufundisha maadili katika ngazi ya familia.
- Semina na Waalimu.
- Kujadili na mamlaka ya elimu ngazi ya wilaya na mkoa.
- Tathmini ya kiroho ili kupima mambo ya kiroho na kupendekeza dhamira za kichungaji ambazo zinaweza kutumika katika mahubiri na miongozo ya katekesi.
- Kufanya utafiti katika ngazi ya Parokia ili kujua nini vijana wanapendelea na kutafuta njia ya kuwajengea hadhi ya utu wao kwa kutumia mambo yanayowavutia vijana.
- Kuchunguza vitabu vinavyotumika mashuleni kama vinahimiza au vinachochea maadili mema.
2. UONGOZI
Dira
Suala la uongozi ni pana. Kuna aina nyingi za uongozi (kiroho, kiutamaduni, kielimu, kiutawala, kisiasa, kiuchumi). Vile vile zipo ngazi mbalimbali za uongozi (familia, ujirani, vijiji, taasisi, kidini, kitaifa). Uongozi unahitaji watu wenye sifa ya huduma, wanaojali, walio wazi, wanaowajibika, wanyenyekevu, wenye hekima na upendo. Uongozi kila mara unashawishika kutenda kinyume na hayo na kuwa na uchoyo na kutumia madaraka vibaya. Kwa hiyo ni muhimu kuandaa viongozi, kushirikiana nao na kushikamana nao na kuwadhibiti kwa lengo la kuwasaidia kuwa jasiri walio waaminifu katika kazi zao.
Hali yetu inadhihirisha kuwa:
- Katika miaka ya hivi karibuni tumeona matatizo mengi ya uongozi. Kwanza kabisa yapasa tujadili kiini chake na kisha tutafute tiba yake.
- Katika uwanja wa kisiasa tunapaswa kuangalia namna wagombea wa na vyoteuliwa na vyama vyao. Tunahitaji kutafuta taarifa ya njia na vyanzo vya upatikanaji wa fedha za vyama vya siasa na namna wanavyozitumia. Watu wajadili kama mfumo wa uwakilishi kiuwiano (proportional representation system) haungeweza kuwa bora kuliko ule wa sasa. Kuna haja kubwa pia ya kusaidia watu kuijua Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
- Ni lazima katika mambo ya kijamii tuwahimize watu kueleza matatizo wanayokumbana nayo katika maisha yao na kuyatolea taarifa katika ngazi ya Parokia hadi Jimbo/Wilaya. Tuwasaidie kushiriki katika utawala tangu ngazi ya Serikali za kijiji/mitaa hadi ngazi ya halmashauri ya wilaya na kutafuta taarifa kisha kufuatilia nini watumishi wa umma wanafanya katika kuhudumia watu. Njia nzuri ni kuanza na kundi mahalia kushughulikia matatizo ya hapo walipo.
- Katika Kanisa tuhimize watu kutoa maoni yao katika Jumuiya ndogo ndogo na kusaidiana kuwa waaminifu katika wito wa Kikristo. Jumuiya ya Kanisa ni mahala ambapo mtu anakuwa na nafasi ya kutimiza wajibu wake wa kushiriki vilivyo katika shughuli za jumuiya. Hiarakia ya Kanisa haimaanishi kuwa ni kutoa amri tu kwa watu wa ngazi ya chini, bali kazi ya Hiarakia ni kuongoza namna ya kutimiza ahadi tuliyoweka wakati wa ubatizo.
Kwa agenda hii tunapendekeza:
Katika ngazi ya kisiasa: kuunda timu ya CPT na wajumbe wa halmashauri kutengeneza maswali maalum, kuendana na hali mahalia, watu wajadili na ili kutoa mawazo na maoni mazuri, wapatiwe habari zinazohitajika kwa ajili ya tafakari. Hapa tusiwape nafasi wale ambao ni wagombea wa kisiasa kutawala mjadala.
Kijamii: Watu watafute ni mashirika gani yapo hapo na huduma zipi hutolewa, na wangeweza kupata msaada gani katika kutatua matatizo yao . Ni taarifa gani tunapaswa kuwapatia watu ili waweze kufanya tafakari katika Jumuiya ndogo ndogo.
Kanisa: Tunawezaje kuimarisha tafakari katika jumuiya juu ya namna Parokia inavyoendeshwa. Halmashauri inafaa iwe chombo ambamo tathmini hiyo inaweza kufanyika. Ikumbukwe Parokia sio chombo cha utawala, bali lazima iwe ni jumuiya hai ya kusaidiana katika kuleta ubora wa maisha ya kiimani, matumaini na mapendo. Kwa pendekezo hili tufanye tathmini ya kiroho katika dhamiri na kuweka ahadi ya uwajibikaji katika kuwa zaidi mashahidi wa ujumbe wa Kristo katika hali halisi ya Tanzania leo.
3. HAKI
Dira
Lazima mfumo wa sheria uwe ni kwa ajili ya jumuiya ya watu katika kulinda na kudumisha amani, ukweli, haki, uhuru, mshikamano na usalama. Mfumo huu unapoleta ukosefu wa haki, watu wanapoteza imani nao.
Tutafute:
- Kwa njia gani tutawasaidia watu kujua haki zao na kuelewa sheria zinazoathiri maisha yao .
- Kuona kama shule zetu zinafundisha Katiba ya nchi na umuhimu wake.
- Tuone kama Wabunge wanawasiliana na majimbo yao na kuwa kweli wawakilishi wao. Kujadili kama wanadhibiti ya kutosha utendaji wa serikali. Ni kwa vipi watu wanapeleka masuala yao katika vyombo vya serikali na kusikilizwa?
- Mahakama za mwanzo zinahudumia watu wengi lakini ziko katika hali mbaya. Je, tunaweza kuziboresha vipi?
- Watu wanaona adhabu zinatolewa kwa makosa madogo, lakini wenye makosa makubwa, wanaachwa tu. Kwa nini watu wanafikiri hivi?
- Lazima tufikiri njia mbadala ya kutoa adhabu na kuona wafungwa kama watu wenye haki pia. Vile vile kutambua kuwa lengo la magereza ni kujenga amani na kurekebisha watu waliofanya makosa.
- Kila mara mfumo wa sheria unafanya kazi taratibu na hivyo watu husubiri mno haki kutendeka. Kukosa ufanisi na utaratibu wa utekelezaji vinasababisha ukosefu mwingi wa haki. Tunawezaje kuboresha hali hii?
Katika mjadala tulenge kuona kwamba “Mamlaka za siasa zichaguliwe na uamuzi wa hiari wa raia, nazo lazima zijali kanuni ya “utawala wa sheria,” ambamo ukuu ni wa sheria na si wa matashi ya watu wasio na sheria.”1
4. BIASHARA NA FEDHA
Dira
Hizi ni taasisi za biashara na fedha na shughuli nyingine zinazotoa huduma katika jumuiya. Biashara zinazotoa mahitaji ya vitu/bidhaa na kubadilishana na bidhaa hizi. Taasisi za fedha zinatunza thamani ya fedha, kwa kuweka kiwango cha kubadilisha fedha.
- Katika biashara, motisha haipaswi kuwa katika faida tu. Biashara inawafikishia watu bidhaa, hivyo isiendeshwe kiunyonyaji.
- Ni vipi tunaweza kuwasaidia watu kutetea maslahi yao na kuzuia wasinyonywe.
- Moyo wa ushirika umepungua mno na matokeo yake watu wameathiriwa na biashara zilizokosa uwaminifu. Tunawezaje kusaidiana.
- Mfumo wetu wa benki unafikisha huduma kwa watu wachache tu, na hasa kwa watu wa mijini na kwa wale wenye kiwango kizuri cha kipato. Lazima tusaidiane, hasa wale ambao hawana kipato cha kutosha, kuunda SACCOS na vikundi vya kusaidiana. Kanisa lazima lifanye bidii kuhamasisha hayo.
- Wachache walio katika mamlaka au katika nafasi za juu za utawala wana marupurupu mengi mno. Tusukume kupunguziwa hayo ili wawe na maisha ya kawaida.
- Tuwe makini na uporaji wa ardhi unaofanywa na makapuni makubwa na watu binafsi, matajiri. Tukumbuke ardhi ni ya thamani na ni hitaji la lazima kwa kila mmoja.
- Rushwa katika biashara, huduma duni, bidhaa duni vinaleta sifa mbaya, na hii ni tabia iliyo dhambi. Miongoni mwa watu hali hii inawajengea hasira na kukosa uaminifu na vile vile watu hujitetea kwa nguvu na kujengea watu fikra ya kulipiza kisasi.
- Udanganyifu katika biashara ni kushusha sifa mmiliki kwa wateja.
- Serikali iwe makini katika kuweka mikataba na wawekezaji wa umma na watu binafsi. Imekwishabainika kuwa katika mikataba hiyo maslahi ya wananchi hayalindwi kikamilifu badala yake wawekezaji hupewa unafuu mkubwa kwa kisingizio kuwa ni kivutio kwao.
- Makapuni ya ndani ni lazima yatiwe moyo na kuungwa mkono ili yaweze kuboresha utendaji wao uwe wenye tija.
5. UCHUMI.
Dira
Uchumi ni kwa ajili ya kuhudumia watu ili wawe na maisha mazuri: wapate mahitaji msingi na walindwe dhidi ya hali zinazowakuta na kutishia usalama wao na majanga mengine yanayoadhiri ubora wa maisha. Maadili katika shughuli ya kiuchumi na kuhakikisha mahitaji haya muhimu katika kumpatia mtu maisha mazuri yanapatikana. Sera za kiuchumi ni lazima ziweke kipaumbele kwa kuzingatia maadili na hivyo kufikia manufaa kwa wote na kulinda utu wa kila mmoja. Kwa hiyo tujadili pamoja na kama jumuiya za kanisa ni lazima tujifunze kuhimiza mahitaji yetu yazingatiwe na wenye maamuzi. Maoni yetu yasikilizwe na kufanyiwa kazi, tunu za kikristo tunazosimamia zionekane katika sera na katika mgawanyo wa bajeti ya serikali.
- Tunaweza kupunguza umasikini kwa kiasi kikubwa katika nchi yetu ikiwa watu wataelewa wajibu wao na kushiriki katika kutatua matatizo yetu: kwa mfano: kushiriki katika namna ya kupata huduma ya maji vijijini, namna ya kudhibiti matumizi ya fedha zinazotumwa katika serikali za mitaa.
- Ni kwa njia gani madiwani watafikisha maombi ya watu wao katika mgawanyo wa bajeti ngazi ya wilaya..
- Je, matumizi katika serikali ngazi ya chini yanawekwa wazi kwa wananchi kujua?
- Wabunge na viongozi katika ngazi ya Mkoa wanatoa fursa ya watu kuwauliza na kuwaeleza mahitaji yao? Tunawezaje kuboresha hali hiyo?
- Je, wakristo wetu wanazielewa fursa zilizopo; huduma zinazotolewa na serikali, mipango ya kusaidiana kama SACCOS, MVIWATA, vyama vya ushirika, jitihada za TASAF. Kwa nini wakristo wetu hawafanyi bidii kuanzisha vikundi/mipango ya kusaidiana? Pia parokia zetu ziwajibike vema katika kujenga ushirikiano na kujenga uwajibikaji wa kijumuiya ili kuboresha maisha.
- Kwa nini watu wetu hawaaminiani? Na tunawezaje kujenga moyo wa uaminifu miongoni mwetu?
- Kwa nini wakristo wetu wanaogopa kuzungumza na wenye mamlaka na walio katika huduma za utawala ili kupeleka malalamiko na kufuatilia utekelezaji wa maamuzi yaliyofanyika. Pia tutafakari namna ya kupambana na tabia ya uvivu.
- Tuna mali nyingi, lakini kila mara tunasubiri “wengine “ au “Serikali” kufanya kitu au kutuletea fedha. Lazima tujifunze kutumia vipaji vyetu na uwezo wetu katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu. Kusaidiana kwa kuunganisha nguvu zetu na uwezo wetu ni wajibu wa kikristo. Mungu ametupa vipawa, lazima tuvitumie.
- Umaskini wa fikra, umaskini wa utashi duni na uwajibikaji ndio hasa husababisha umaskini. Ni kwa vipi jumuiya ya wakristo wanaweza kuwa mahala pa uwajibikaji ili kuweza kuboresha hali yetu.
6. HIFADHI YA JAMII
Dira
Mungu ametujalia uhai na anatupa mwaliko wa kutunza maisha na kuongeza ubora wa maisha. Mungu pia anatutaka kujali kwa namna ya pekee watu wasio na uwezo katika jamii yetu: yatima, wajane, walemavu, wagonjwa, watoto wa mitaani na wazee.
Hifadhi ya jamii maana yake ni kuweka mipango ya kuwahakikishia watu mahitaji na huduma ili wasiishi katika hali ya kukosa hifadhi/ usalama. Tunapozungumzia hifadhi ya jamii haswa tunamaanisha mifuko ya pensheni, elimu, bima ya afya na misaada ya kijamii.
Watu wengi miongoni mwetu hawafikiwi na huduma hii na familia zao zinakwama wanapoingia katika kuhitaji huduma hizo. Tunapaswa kuwa na mtazamo fikiriki ili kuweza kupata njia za kusaidiana. Mipango rasmi iliyoanzishwa na serikali au mashirika ya umma ama makampuni binafsi zinawafikia watu wachache tu ambao ni kama asilimia sita (6%) ya kundi la wafanyakazi.
- Jumuiya ndogondogo wangeweza kuwa chombo cha kusaidiana katika mahitaji ya kila siku ya wanajumuiya wao. Tunawezaje kuzifanya jumuiya zetu zitimize wajibu huu?
- Kutoaminiana ni kikwazo kikubwa katika kuwa na mipango na mifuko endelevu ya jumuiya. Tunawezaje kujenga moyo wa uaminifu? Viongozi wazuri walio tayari kuhudumia wanawezaje kupatikana na tutawawajibishaje viongozi wabovu?
- Lazima tutafute taarifa juu ya huduma na fursa zilizopo. Katika ngazi ya Parokia iundwe timu kwa ajili ya kutafuta taarifa na kuzifikisha katika Jumuiya ndogo ndogo. Taarifa hizo ni pamoja na zihusuzo mfuko wa afya ya jamii, sera ya serikali juu ya karo ya shule, sheria zinazohusu huduma ya tiba kwa mama na mtoto, wazee.
- Katika jamii yetu kuna watu walemavu wengi: Takwimu zinaonyesha kuwa walemavu ni 10% ya watu wote. Hawa ni wenye ulemavu wa namna moja ama nyingine. Kwa kawaida wahitaji hawa wanabaki kutegemea wanafamilia wao wachache, hasa mama au bibi. Kundi hili ndio maskini kupindukia kwa sababu jitihada za kuwainua ni ndogo sana .
Tatizo hili sio rahisi kulitatua. Lakini kwa kutegemea mifumo rasmi ya hifadhi ya jamii tu haitoshi na huduma hii kwao haitakuwa endelevu. Kwa hiyo tunapaswa kutafuta njia ambazo misingi yake ni katika njia za kizamani za kusaidiana, tuzitumie katika mazingira yetu ya leo kwa namna ya kisasa. Wazo hili linaweza kutekelezekaje?
PROGRAMU YA KUHAMASISHA HUDUMA YA KICHUNGAJI KATIKA JAMII KUELEKEA
UCHAGUZI MKUU 2010
(2009 - 2011)
TUKIO
WALENGWA
WAPI/NGAZI
LINI
MHUSIKA/MWEZESHAJI
Mkutano wa Taifa wa kutengeneza Programu
- Wakurugenzi wa Kichungaji
- Wajumbe wa Tume ya H & A (Majimbo)
TEC
20 – 22 Januari, 2009
- Katibu wa Idara ya Kichungaji TEC
- Katibu Tume ya Haki ya Amani – TEC
+ CPT (T)
Kukamilisha programu (booklet form)
TEC
Februari 2009
,,
Kutuma Programu Majimboni
- Maaskofu
- Wakurugenzi wa Uchungaji – Majimbo
- Viongozi wa Tume Majimbo
TEC
Machi 2009
,,
Mkutano wa Jimbo kuzindua Programu
- Mapadre, Watawa
- Halmashauri na vyama vya Kitume
- Taasisi
Jimbo
Aprili 2009
I. Kuanza Mapadre na Watawa, wa
II. Walei
- Askofu
- Mkurugenzi
- Tume (Jimbo)
Mkutano wa Makatekista
Makatekista
Jimbo
Aprili 2009
- Mkurugenzi Uchungaji
- Tume/Mkurugenzi Katekesi
Semina/Mikutano ya Walei/Vyama
Halmashauri (Viongozi wa JNN & Vyama, Kamati)
Parokia
Mei - Juni 2009
- Paroko/mjumbe kutoka Jimboni
- Kamati Tendaji, Viongozi wa vyama
Kufikisha Programu JNN
Waumini/Wakazi
JNN
Julai – Sept. 2009
- Paroko
- Halmashauri ya Parokia
Mijadala na utekelezaji
,,
- JNN
- Vyama vya Kitume
Okt – Des. 2009
- Paroko, Kamati tendaji
- Viongozi wa Jumuiya
Mkutano wa Taifa
(Tathmini ya I)
- Wakurugenzi wa Kichungaji
- Wajumbe wa Tume
TEC
Januari 2010
- Katibu Mtendaji Idara ya Kichungaji
- Katibu Tume – TEC
+ CPT (T)
Mwendelezo wa Mijadala na utekelezaji
Waumini na Wakazi
- Jimbo
- Parokia
- JNN
Febr. – Sept. 2010
- Askofu
- Paroko
- Walei
Kushiriki Uchaguzi kwa tathmini
Waumini na Wakazi
- Taifa
- Jimbo
- Parokia, JNN
Okt – Des. 2010
,,
Mkutano wa Taifa (Tathmini ya II) + kubainisha agenda
- post election
- post synodial
- Wakurugenzi wa Kichungaji
- Wajumbe wa Tume
TEC
Januari 2011
- Katibu Mtendaji Idara ya Kichungaji
- Katibu Tume
+ CPT (T)
Mwendelezo wa Programu
- Post Election
- Post Synodial
Waumini na Wakazi
- Jimbo
- Parokia
- JNN
Febr. - Sept. 2011
- Askofu
- Paroko
- Walei
Kuandaa Ripoti ya Majimbo na kutuma Taifa
Jimbo
Oktoba 2011
- Mkurugenzi wa Uchungaji
- Viongozi wa Tume
Kuandaa Ripoti ya Kitaifa ya utekelezaji wa Programu.
TEC
Novemba



Photos:Ayoub mzee
The British High commissioner in Tanzania Diana Lousse with former Premier Cleopa Msuya

Message from the new British High Commissioner
Karibu!
I am delighted to be in Tanzania. In my short time here so far I have received a wonderfully warm welcome from Tanzanian people. I am much looking forward to visiting all regions of the country to meet more "Wananchi" and get a sense of the opportunities for development and the challenges that still face many Tanzanians.
I expect my three years here to be spent on further strengthening the UK's multi-faceted partnership with Tanzania. I will work with Tanzanian partners on issues of concern to us both which affect peace and security, both regionally and more broadly in the international arena. With a renewed commitment to UK assistance for Tanzania's development, the UK will continue to be Tanzania's largest provider of General Budget Support (GBS). A vitally important priority will be to find ways to improve the environment for trade and investment between our countries, more important than ever in the current economic climate, and for increasing Tanzania's prosperity.
I will also be keen to explore how the UK and Tanzania can work together on other issues, such as mitigating the impact of climate change on the environment, and managing migration between our countries and in the region. And I look forward to experiencing at first hand Tanzanian multi-party democracy in action, in the run up to the 2010 General Election and beyond.
So welcome to our website. I hope you will find it both a source of useful and interesting information about British Government policies and procedures, and a tool for building stronger links between us. If you have any comments, suggestions or queries please feel free tocontact our High Commission



This is summer time in the UK

For the rest of summer, rainfall is likely to be near or above average over the UK and much of northern Europe


What do we mean by average rainfall?
This final forecast for Summer 2009 covers the month of August. The UK average rainfall for August from 1971-2000 is 84.6 mm



For the UK and much of northern Europe temperatures for the rest of the summer are likely to be near or above average.
What do we mean by average temperature?
This forecast covers the final month of summer, August. The UK average temperature in August from 1971-2000 is 14.7 °C








Have Your Say on Policing in London
The Metropolitan Police Authority (MPA) is consulting on London's policing priorities. We are interested in your opinion.
Please take part in a short questionnaire to tell us your views. To complete a questionnaire click on
www.mpa.gov. uk/publications/ policingplans/ or call 020 7202 0063, leave your name and address and we will send you a paper copy.
If you require a telephone questionnaire please call 020 7202 0063, leave your name and telephone number and somebody will call you back.
We look forward to hearing your views on policing in London.