Thursday 19 December 2013

TASWIRA ZA KIJIJI CHA QUNU ALIKOZIKWA MZEE NELSON MANDELA

Qunu ni kijiji kidogo katika jimbo la Eastern Cape la Afrika Kusini, kilomita 32 Kusini-Magharibi ya mji wa Mthatha, katika barabara ya Butterworth na Mthata. 
Kijiji cha Mvezo, pembezoni mwa mto Mbashe, ni jirani ya mahali ambapo Mzee Nelson Mandela alizaliwa. Hapo Qunu ndipo alipokulia na aliweka nadhiri ya kurejea. 
Kijiji cha Qunu ndipo baba yake Mandela alipohamia baada ya kuvuliwa Uchifu wa Mvezo. Katika kitabu chake cha ‘Long Walk to Freedom’ Mzee Mandela amekitaja kijiji hicho kuwa ndipo alipoishi maisha ya furaha wakati wa utotoni. 
Jumapili ya Desemba 15, 2013 Mzee Mandela alizikwa kijijini Qunu katika mazishi ya Kitaifa yaliyoshuhudiwa dunia nzima. Alizikwa kwa heshima zote za kiongozi wa Taifa katika sehemu aliyochagua mwenyewe kuwa nyumba yake ya milele.
 Daraja la waendao kwa miguu likipita juu ya barabara mpya ya lami inayojengwa kuelekea kijijini Qunu.
Siku ya mazishi barabara ya kuelekea Qunu ilifungwa na ni magari yaliyokuwa na kibali tu ndiyo yaliyoruhusiwa kupita
Ulinzi ulikuwa mkali kila sehemu kijijini Qunu
Wageni wakiwa katika geti kuu la nyumba ya Mzee Mandela hapo Qunu
Nyumba ya Mzee Mandela
Nyumbani kwa Madiba kijijini Qunu