Monday, 16 December 2013


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU)  Dkt Dlamini Zuma kwa hotuba ya kusisimua aliyoitoa  wakati wa mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013. Kushoto ni Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Malawi Mhe. Joyce Banda. Rais Kikwete alialikwa kuzungumzia sifa za mapambano ya ukombozi aliyoongoza  Mzee Madiba ambapo Tanzania ndiyo ilikuwa ni nchi yake ya kwanza kusaidia mapambano yote ya ukombozi kusini mwa Afrika kwa kuwahifadhi  na kuwapa misaada ya hali na mali wapigania ukombozi wake.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wageni wengine akitoka katika hema maalumu lililotumika kwa shughuli za  mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013. Wa tatu kulia ni Mrithi wa kiti cha Ufalme wa Uingereza Prince Charles.Picha na IKULU