Saturday, 10 November 2012

JIMBO LA UCHAGUZI-KIGOMA KASKAZINI
08.11.2012


Rais Jakaya Kikwete Akiwasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma Leo
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye Muda mfupi baada ya Rais Jakaya Kikwete Kuwasili Mkoani Dodoma leo  tayari kuongoza vikao na mkutano mkuu wa nane wa CCM

Jumuiya ya watumiaji wa huduma mbalimbali nchini kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter imezindua rasmi shindano la kusaka kampuni zinazotoa huduma na bidhaa mbovu kwa wateja nchini Tanzania.

Jumuiya hiyo inawajumuisha watu wa kada mbalimbali wakiwemo wanasheria, wanaharakati, waandishi wa habari, viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara na wateja wa huduma na bidhaa mbalimbali nchini Tanzania.

Lengo la jumuiya hiyo ni kushinikiza wafanyabiashara nchini kutoa huduma na bidhaa bora kwa wateja na kuwakumbusha umuhimu wa wateja. Kauli mbiu ya wanajumuiya hao ni Mteja ni Mfalme.

Katika wiki ya kwanza tangu jumuiya hiyo kuzinduliwa jumla ya makampuni 21 yameingizwa katika shindano hilo kwa wateja wao kuwasilisha malalamiko yao. Kwa taarifa zaidi kuhusu ni fuatilia akaunti ya Twitter @hudumambayatz au kundi la Facebook linalojulikana kama HUDUMA BONGO.

Ili kuweza kupiga kura yako unahitajika kuwa na akaunti hai (yenye mawasiliano mara kwa mara) katika mtandao wa Twitter au Facebook na kujiunga na jumuiya hiyo. Mara tu utakapowasilisha kero yako utaifanya kampuni unayoilalamikia kuingia katika mchuano mkali wa kumsaka bingwa wa huduma mbovu kwa wateja nchini.

Huduma Bongo inatoa wito kwa makampuni yote kuboresha huduma na bidhaa zao ili kuweza kuwapatia wateja kilicho bora zaidi katika soko hili la ushindani.

Imetolewa na 
Mshauri wa Habari wa Huduma Bongo 
Novemba 9, 2012

 Barabara za katikati ya mitaa ya manispaa ya Dodoma zikiwa zinatengenezwa kwa kiwango cha Lami.
Wajasiriamali wakiwa wameweka biashara zao kwenye moja ya mageti ya makao makuu ya CCM,kipindi hiki cha mkutano mkuu kumekuwa na maongezeko ya mahitaji ya bidhaa za chama bora Tanzania,hivyo kutoa fursa kwa wafanya biashara wengi kuuza bidhaa za chama hicho.Picha na Adam Mzee-Dodoma
Mkurugenzi wa Kampuni ya Best Import Zanzibar  Issa Kassim Issa kushoto akimkabidhi Katibu wa Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Abadallah Ali Abadallah dola 2000 za kimarekani kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Katibu wa Mufti Zanzibar Skeikh Fadhil Soraga katika Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Vuga mjini Zanzibar.Picha na Yussuf Simai Maelezo Zanzibar.
---
Na : Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar

Kampuni ya Best Imports Zanzibar inayojishughulisha na biashara ya uuzaji Kuku (Paja Nono) imetoa jumla ya Dola 2000 za kimarekani kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Katibu wa Mufti Zanzibar Skeikh Fadhil Soraga.

Akitoa msaada huo leo kupitia kwa Katibu wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar,Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Issa Kassim Issa amesema wameamua kutoa mchango huo kutokana na kuguswa na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Sheikh Soraga na kwamba kiasi hicho cha pesa kitatumika kusaidia matibabu yake.

Issa amesema wamiliki wa Kampuni hiyo David Aloy na Carlos Ajala wamestushwa na kitendo alichofanyiwa Sheikh Soraga ambaye ni mtu muhimu katika jamii kutokana na mchango wake mkubwa.

Ameongeza kuwa Shekh Soraga ni mtu mwenye heshima kubwa Zanzibar kutokana na shughuli zake za kila siku na kwamba kitendo alichofanyiwa kinapaswa kulaaniwa na kila mtu.

Kwa upande wake Katibu wa Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Abadallah Ali Abadallah aliishukuru Kampuni hiyo kwa kuwa wa kwanza kutoa msaada wa kifedha na kuahidi kiasi hicho cha fedha kitapelekwa sehemu husika.

Aidha Katibu huyo amewaomba wananchi kumuombea Shekh Soraga apone haraka na wale wenye uwezo kuiga mfano wa Kampuni ya Best Import ili kufanikisha matibabu hayo.

Sheikh Soraga ambaye anatarajiwa kupelekwa India kwa ajili ya matibabu zaidi ameumia sehemu za usoni,mikononi na kifuani  baada ya kumwagiwa Tindikali na mtu asiyejulikana wakati alipokuwa akifanya mazoezi viwanja vya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi Unguja.
ZANZIBAR ALHAMISI NOVEMBA 8, 2012.
 Viongozi wa Jumuiya mbili za Kiislam Kisiwani Zanzibar wanaotuhumiwa kwa makosa tofauti ya kutoa lugha za uchochezi na kusababisha ghasia na vitendo vya uvunjifu wa amani uliopelekea uharibifu wa miundombinu ya barabara ambao leo walifikishwa Mahakama Kuu ya Vuga mjini Zanzibar, wamerudishwa tena Rumande.

Kesi hiyo ambayo inawakabili Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar Sheikhe Faridi Hadi Ahmedi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Sheikhe Mselem Ali Mselem, Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid Hamdan, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman na  Ghalib Ahmada Omar iliitwa mahakama kuu kwa kutajwa baada ya kuahirishwa mwezi uliopita.

Hata hivyo, kabla ya kutajwa tena kwa kesi hiyo, huku kukiwa na ulinzi mkali wa Makachero wa Polisi na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia, ndani ya Mahakama hiyo kulizuka mabishano makali ya kisheria huku kila upande ukionyesha ujuzi wao wa kisheria.

Kwa upande wa Mawakili wa Watuhumiwa Bw. Salum Toufik na Bw. Abdallah Juma Kaka, wakiwasilisha hoja mbalimbali za uvunjifu wa haki za watuhumiwa ikiwemo ya kunyolewa ndevu wakiwa Rumande katika Chuo cha Mafunzo jambo ambalo ni kinyume na uhuru wa kuabudu kwani wamesema ndevu kwa mashehe ni sehemu ya ibada.

Baada ya kuwasilisha hoja hizo, Mwanasheria wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ramadhani Nassibu, akinukuu vifungu vya sheria vilivyopo kwenye Katiba ya Zanzibar na kusema kuwa kama kuna haki zinazovunjwa na chombo chochote ama mtumishi wa Serikali kuna mahala pengine pa kupeleka malalamiko hayo.

Baada ya mabishano hayo, Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Mh. George Kazi, aliamuru watuhumiwa wote warudishwe tena rumande hadi Novemba 20, mwaka huu itakapokuja tena katika Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa kutajwa.
  Na
 Mohammed Mhina,
Jeshi la Polisi Zanzibar
Hon. Dr. Harrison G. Mwakyembe- (MP), Tanzania Minister for Transport  
---
Britain Tanzania Society (BTS) Annual general meeting will be held at  Westminster Central Hall, Saturday 10 November 2012, starts at 2PM. Hon. Dr. Harrison G. Mwakyembe- (MP), Tanzania Minister for Transport - guest speaker, will be talking on "The Quest for a New Constitution in Tanzania: Prospects and Challenges".
The next BTS Seminar is at SOAS on December 6th at 5PM, on the media and democracy in Tanzania.
Malaika Kids, a childrens charity familiar to many of you, is having it's annual London reception on November 20th from 6-8.30PM at 120 Moorgate,and BTS members are welcome to attend. 
Also, there are fascinating article on the BBC website recently about the spread of the internet in Tanzania, which might well be of interest.  The pace of change is quite extraordinary.  

  U.S. Ambassador to Tanzania Alfonso E. Lenhardt (right), present's ambulance keys to the Chief of Medical Services of the Tanzania Peoples Defense Force (TPDF), Major General AS Mwabulanga, (left), during a donation ceremony held yesterday at the TPDF Headquarters in Dar es Salaam.
US Ambassador to Tanzania, Alfonso E. Lenhardt, (fourth from right), Chief of Medical Services of the Tanzania Peoples Defense Force (TPDF), Major General AS Mwabulanga, (fourth from left) following the donation ceremony by the United States yesterday at the TPDF Headquarters in Dar es Salaam. Others officials pictured are Country Director, Walter Reed Army Institute of Research (WRAIR), Edward Sekonde, (right); Master Chief, Operations Coordinator, Defense Attaché Office, Vladimir T. Narvaez, (second from right); Brigadier General LS Msangi, (third from right); and Colonel DB Maganga, (left); Senior Defense Official/Defense Attache, Lieutenant Colonel, Kevin C. Balisky, (second from left); and General Officer Command of General Military Hospital Brigadier General VT Lyimo, (third from left).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua rasmi ujenzi wa bomba la gesi asilia toka Mtwara hadi Dar es salaam leo Novemba 8, 2012 maeneno ya Kinyerezi njijini Dar es salaam. Nyuma yake ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na viongozi wengine wakimsikiliza  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo miundombinu ya  bomba la gesi asilia toka Mtwara hadi Dar es salaam leo Novemba 8, 2012 maeneno ya Kinyerezi njijini Dar es salaam. Nyuma yake ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na ujumbe wa kampuni inayojenga bomba la gesi asilia kutoka Mtwata hadi Dar es salaam, Benki ya Exim ya China na viongozi waandamizi wa serikali alipowakaribisha Ikulu kwa mazungumzo baada ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa bomba hilo maeneo ya Kinyerezi jijini Dar es salaam.Picha na IKULU