Saturday, 21 January 2012


Press TV

20th January 2012

PRESS RELEASE: Ofcom Bans Press TV in the UK

OFCOM HAS REVOKED Press TV Limited’s Television Licensable Content Service licence. It means that the British public can no longer watch Press TV on BSkyB’s Sky platform. Press TV International has released the following statement:


The British government's media regulatory body, Ofcom, has banned Press TV's broadcast in the UK and removed the channel from the Sky platform without responding to a letter sent from Press TV's CEO to Ofcom's chief executive earlier this month.

This after Ofcom fined Press TV Limited in London a hundred thousand pounds for the channel's airing of a 10-second news clip. At the same time, Ofcom made moves to revoke the license of Press TV Limited in the UK for what it called Press TV Limited's lack of control over the channel's broadcast. We asked Ofcom, if Press TV Limited did not have control over the broadcast, why was it getting fined; if it did have control, why would the license be revoked?

Ofcom’s contradictions are nothing new for Press TV. The British government's tool to control the media has on several occasions changed its decisions regarding Press TV in its two-year campaign against the alternative news channel.

In response to Press TV's complaints about Ofcom's subservience to the British government and the monarchy, which have been a focus of Press TV's critical coverage in recent years, Ofcom claims it is not a government organization. But there is every indication that it is. It gets both its authority and funding from the British government. Ofcom was created by an Act of Parliament and gets most of its funding from governmental grant-in-aid. Britain's Office for National Statistics has also said Ofcom must be classified as a central government unit.

As a news channel broadcast in the UK, Press TV has shed more light on the British government's domestic and foreign policies. It has aired critical views regarding Britain's involvement in wars of aggression in Iraq and Afghanistan. It has also shown the close ties between the British Royal family and UK-founded monarchies in the Persian Gulf region, including the autocratic regimes in Bahrain and Saudi Arabia, which have been oppressing their people for decades. Press TV has also provided critical coverage of the extravagant costs of Britain's Royal Wedding at a time of great financial difficulty for ordinary Britons. The channel covered the 2011 unrest in Britain and the heavy-handed police crackdown, drawing the resentment of London's ruling establishment.

Wikileaks cables have revealed that London and Washington are exploring ways to construct a case to silence Press TV. And, Ofcom, the media arm of the Royal family, exhausted all efforts to put an end to Press TV's broadcasting in the UK. But it fails to grasp the reality of mass communication in the modern era and the impossibility of containing the flow of information. Press TV will do everything possible to make sure that its voice will definitely reach its audience in the UK.


For more information, please contact Press TV International on info@presstv.ir.










Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaban Bin Simba Ofisini kwake jijini Dar es salaam Januari 18, 2012. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,William Lukuvi.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Nkopi akifafanua jambo wakati wa mkutano mkuu wa madaktari nchini, Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kuhusu tamko lao la kuitaka Serikali kuwarejesha Hospitai ya Taifa ya Muhimbili, madakari wenzao walioko mafunzoni ambao wamehamishiwa hospitali za kawaida baada ya kuitisha mgomo wa kudai malipo yao
Mwanafunzi wa shule ya Msingi Luilo Ludewa akiwa amebeba majembe baada ya naibu waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri kuagiza warudi madarasani Jana asubuhi.
Mwalimu wa shule ya msingi Luilo kata ya Lifua wilaya ya Ludewa mwalimu Mgaya akipita katika eneo ambalo wanafunzi walikuwa wakilima na kuacha majembe na kukimbia kujificha
Wanafunzi wa shule ya Msingi Luilo Ludewa wakiwa wamejificha katika kichaka pamoja na walimu wao kumkwepa naibu waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri jana
safara wa naibu waziri wa tamisemi Aggrey Mwanri ukipita eneo ambalo wanafunzi walikuwa wakilima.Picha na Mdau Francis Godwin
---
BAADA ya naibu waziri ofisi ya waziri mkuu Tamisemi Aggrey Mwanri kuukataa mradi wa umwagiliajikatika kata ya Lifua wilayani Ludewa uliojengwa kwa zaidi ya shilingi milinio 500 bila kufanya kazi kutoka na kubomoka kabla ya muda na ule wa ukarabati wa nyumba ya mganga kata ya Lupangailiyokarabatiwa kwa kiasi cha shilingi milioni 7 ,mbunge wa jimbo la Ludewa acharuka mbele ya naibuwaziri amkataa mhandisi wa maji na mhadisi wa ujenzi ataka naibu waziri kuwapeleka jimboni Kwake ama jimbo la waziri mkuu Mizengo Pinda.
Mbunge Filikunjombe aliwakataa wahandisi hao wawili Christopher Nyandiga wa maji na mhandisi waujenzi Rashid Mtamila leo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa wakati wa majumuishoya ziara ya siku mbili ya naibu waziri huyo katika kutembelea miradi ya kimaendeleo katika wilaya hiyo ya Ludewa.
Mbunge Filikunjombe alimweleza naibu waziri huyo kuwa wilaya ya Ludewa imegeuzwa kuwa ni shamba la bibi kwa baadhi ya viongozi wasio waadilifu ambao wamekuwa wakitumia vibaya nafasi zao kwakuhujumu miradi ya kimaendeleo inayoibuliwa katika wilaya hiyo.
Alisema kuwa kila wakati amekuwa akiwaonya watumishi wa wilaya ya Ludewa kufanya kazi yao kwa uadilifu ila baadhi yao wameshindwa kabisa kuonyesha uaminifu katika utendaji wa kazi yao.
“Viongozi wenzangu na madiwani wangu wapo walionifuata kutaka niwatetee kwa uozo huu ila nasemaheri kulaumiwa kwa kusimamia ukweli na kupinga ufisadi unaofanyika katika wilaya ya Ludewa ila nipo tayari kuendelea kufanya kazi na viongozi waadilifu “
Alisema kuwa wahandisi hao wameendelea kuwa kikwazo kikubwa katika wilaya ya Ludewa na kuwamiradi mbali mbali inayosimamiwa katika wilaya hiyo imekuwa ni mibovu na haina sifa japo imetumiafedha nyingi zaidi .
Mapema asubuhi naibu waziri huyo alifanya ziara ya ghafla ambayo haikuwepo katika ratiba katika banio la mradi wa umwagiliaji wa Lifua ambalo umejengwa na kampuni ya Summer Communication kwakiasi cha zaidi ya shilingi milioni 357 toka mwaka 2009/2010 bila kufanya kazi .Kitoa taarifa ya mradihuo mbele ya naibu waziri Mhandisi wa maji wilaya ya Ludewa Nyandiga alisema kuwa awamu ya kwanza ilitumia kiasi cha shilingi milioni 357,262,990 na mradi huo kukabidhiwa kwa Halmashauri toka mwaka 2010 japo hautumiki kutokana na kuvujisha maji.
Wakati awamu ya pili mradi ulijengwa na kampuni ya Tan Direct Co.Ltd ya Dar es salaam kwa gharama ya shilingi milioni 227,613,136.15 kwa kazi ya kujenga mfereji wenye urefu wa mita 1725,usakafiaji wa eneo la kuingia na kutoka kwenye daraja hilo ,ujenzi wa vigawa maji vinne na ujenzi wa vianguko vya maji vinne na ujenzi wa kivusha maji kimoja na kuwa hadi sasa mkandarasi huyo amelipwa asilimia 64.9 ya fedha zote na kazi hiyo imefanyika kwa asilimia 73.2.
Akimhoji mkandarasi huyo naibu waziri huyo Mwanri alimtaka kueleza sababu ya kulipa mamilioni ya fedha katika mradi huo bila kufanya kazi na hauna maji katika kipindi hiki cha masika ,mhandisi huyo alikana kuwa yeye si msanifu wa mradi huo hivyo hawezi kujibia swali hilo.
Akitoa majumuisho yake na maombi ya mbunge Filikunjombe ya kutaka wahandisi hao kuondolewa katika wilaya hiyo ya Ludewa naibu waziri huyo alisema suala hilo linawezekana kwani pia kwa upandewake hajapendezewa na ufisadi mkubwa uliofanyika katika miradi hiyo.



Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekieli Maige alipokuwa akiwaeleza wafanyakazi wa Msitu wa Hifadhi Ruvu uliopo Kibaha, Mkoani Pwani nia ya Wizara kuanza kuzalisha nishati ya mkaa na kuni, hivi karibuni.
--
Na Tulizo Kilaga

WIZARA ya Maliasili na Utalii iko kwenye mchakato wakuangalia uwezekano wakutumia maeneo yake yalioko Kibaha mkoani Pwani kwa ajili ya uzalisha wa nishati ya kuni na mkaa.

Hatua hiyo inakuja kufuatia kukosekana kwa ufumbuzi wa tatizo la nishati ya kuni na mkaa ambao kwa miaka yote asilimia kubwa ya nishati hizo hasa mkaa hutumika jijini Dar es Salaam.

Katika ziara yake ya kutembelea misitu ya hifadhi iliyoko Mkoani Pwani hivi karibuni, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel Maige alisema kwa miaka yote asilimia karibia 50 ya nishati ya
kuni na mkaa unaozalishwa nchini unatumika jijini Dar es Salaam kutokanawakazi wake kushindwa kutumia nishati nyingine kama umeme na gesi.

“Hali ilivyo sasa ni lazima tukubari tutaendelea kutumia mkaa kwa miaka kadhaa ijayo,na ili kufanya hivyo ni lazima tujipange kuwa wazalishaji wa mkaa, Wizara sasa haioni haja yakusubiri
watu wachome mkaa na kuanza kukimbizana nao na badala yake imeamua kukabiliana na mahitaji ya nishati hiyo,” alisema Mhe. Maige.

Aliongeza kuwa kanuni ya uchumi zinasema kuwa jinsi unavyoongeza ugavi ndivyo unavyopunguza bei, na jinsi unavyopunguza bei ndivyo unavyowapunguzia hamu wazalishaji
wapya kuingia kwenye eneo hilo kwa sababu halitakuwa na faida. Hivyo wizara inaweka mikakati yakuzalisha mkaa.

“Wizara kwa kupitia Wakala wake wa Huduma za Misitu (TFS) inafikilia kuanzisha mashamba ya kuni ambapo itapanda miti inayokomaa kwa muda mfupi na baadaye kuchoma mkaa na
kufungua vituo vya kuuzia mkaa kwa bei nafuu kuliko mkaa wa wizi au mkaa unaotozwa ushuru mwingi kwenye maeneo yaiyoruhusiwa,” alisema Waziri.

Mhe. Maige alisema hatua hiyo itaiongezea kipato TFS na kuwapa changamoto wazalishaji wa nishati nyingine na kupunguza presha ya uvamizi wa misitu kwenye maeneo ambayo yamezuiwa.

Aliongeza kuwa utekelezaji wa mpango huo utahusisha sekta binafsi kwa kuwa sheria inaruhusu kuingia mkataba wa muda mrefu na watu wanaotaka kuendeleza misitu. Hivyo wawekezaji hao
watalazimika kupanda miti na kuuza huku ardhi ikibaki serikalini ili kuongeza uzalishaji.

Kwa upande wake, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu, Bi. Monica A. Kagya alisema wakati wa kuanzisha mashamba hayo watazingatia mahitaji ya wakazi wa maeneo husika
na kuchanganya aina ya miti kutokana na mahitaji ya wananchi, lakini dhumuni kuu litakuwa kupata kuni na mkaa.

Aliongeza kuwa, zoezi hilo litaanza kutekelezwa mara baada ya wataalamu wa misitu kukamilisha utafiti wa aina ya miti inayofaa kupandwa na kukomaa kwa muda mfupi huku ikizalisha mkaa mzito
unaopendwa na wengi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwamtumu Mahiza alisema atahakikisha vijana wanaotumia nguvu kazi zao kufanya uharibifu, wanashirikishwa kwa nguvu zote katika shughuli za upandaji miti inayokomaa kwa muda mfupi kuanzia msimu huu wa mvua ili kuweza kuzalisha nishati ya kuni na mkaa kwa wingi bila
kusababisha uharibifu wa mazingira.
Mkoa wa Pwani ni eneo linaloathilika zaidi na mahitaji ya mazao
ya misitu ya mkoa wa Dar es Salaam kutokana na ukaribu wa mikoa husika ambapo takwimu za mwaka 2010 zinaonyesha kuwa Tanzania hutumia magunia milioni 64 ya mkaa kwa mwaka ambapo
nusu ya hayo hutumika jijini Dar es Salaam.
--