Sunday 22 January 2012

Johnnie Carson, Assistant Secretary of State for the Bureau of African Affairs; Ret. General Colin Powell, former U.S. Secretary of State; Susan R. Rice, U.S. Permanent Representative to the United Nations; and Ambassador R. Barrie Walkley inaugurating the new U.S. Embassy in Juba, South Sudan on Independence Day.
Secretary Clinton watches a skit at the Center for Research and Action for Peace in Abidjan, Cote d'Ivoire, Tuesday, Jan. 17, 2012.
AP Image / Jan 17, 2012
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia eneo la uwanja wa mao unaotarajiwa kuengwa upya baada ya taratibu kukamilika. kushoto yake ni Waziri Ofisi yake Mohd Aboud Mohd.
--
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amefanya ziara fupi ya kukagua Uwanja wa Michezo wa Mao ambao Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko katika mipango ya kutaka kuujenga upya Uwanja huo.Balozi Seif alikagua Ramani ya eneo la uwanja huo akiwa na Kamati Maalum iliyoundwa ya kuandaa michoro ya uwanja huo.

Miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja na Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohd Aboud Mohd, Waziri wa Habari Abdillahi Jihad Hassan, Waziri Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdull habib Fereji,Waziri wa Mawasiliano na Miundo mbinu Hamad Masoud, Waziri asiye na Wizara Maalum Machano Othman Said na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Dr. Ali Mwinyikai.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema uwamuzi wa Serikali ya kuimarisha Uwanja wa Mao ni kujenga mazingira mazuri ya kusherehekea vizuri zaidi sherehe za Mapinduzi.

Alisema uwanja wa Amani hivi sasa haukidhi mahitaji ya sherehe hizo kutokana na ufinyu wa eneo pamoja na kuepusha hitilafu za uwanja kutokana na gwaride la Vikosi vya Ulinzi ambalo ndio chachu ya sherehe hizo.

“ Kwa kweli bila ya gwaride hakuna sherehe. Na hili ndilo linalowapa nafasi zaidi wananchi kufurahia sherehe hizo” Alisisitiza Balozi Seif.

Wajumbe wa Kamati hiyo walipata fursa ya kujadiliana michoro ya ramani hiyo wakisisitiza kuwepukwa kwa nyumba zilizo karibu na uwanja huo wakati ujenzi utakapowadia.
Uwanja wa Mao ni miongoni mwa Viwanja Vitatu vinavyotegemewa na Wanamichezo kuhudumia michezo kikitanguliwa na kile cha Amani Unguja na Gombani Kisiwani Pemba.

Balozi Seif akionyesha uso wa matumaini ya kuboresha uwanja wa mao kushoto yake akiwa na katibu mkuu habari Dr. Ali Mwinyikai. Kulia ya balozi ni waziri wa miundo mbinu Hamad Masoud Mwenyekiti Wa Baraza La Michezo Zanzibar Sherry Khamis Na Waziri Ofisi Ya Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mohd Aboud Mohd.