Friday 15 July 2011

MAPENDEKEZO YA MABADILIKO YA MFUMO WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) –UK

Mchakato mzima wa kuanzishwa kwa chama cha mapinduzi UK, ulianzishwa kwa kuzingatia azma nzima ya chama cha mapinduzi kutaka kuwashirikisha wanachama wake katika maamuzi ya kukijenga chama na nchi, na pia kuleta demokrasia halisi ndani ya chama.
Tawi lilianzishwa rasmi mwaka ------ hapa UK na wanachama wake wakereketwa, na likaanza kushiriki kufanya kazi zake za uhamasishaji wa wanachama na kukijenga hapa UK.
Tawi limekuwa lilikua kwa kasi na limekuwa na wanachama wengi kuliko inavyopaswa kikatiba, na hivyo limekuwa vigumu kuendelea kuwa tawi kutokana na uwingi huu wa wanachama wake, pia kiuendeshaji na mawasiliano na makao makuu Dodoma Tanzania.
Vilevile kutokana na jiografia ya wanachama hawa wa nje ya nchi hasa ulaya na marekani na aina ya wanachama wa chama huku nje; kumeonekana kuwa kunauhitaji wa kuimarisha mawasiliano na uwakilishi wao ili kuleta tija ya mchango wa wanachama kwenye chama chao katika kukijenga chama na nchi yetu Tanzania.
Aidha kwa uhitaji huo, mapendekezo mbalimbali yametolewa kuboresha muundo wa chama huku nje ya nchi. Hi ikiwa na maana kuwa kurekebishika kwa mfumo au muundo huu kutatatua moja kwa moja tatizo la mawasiliano na itaongeza tija na ufanisi wa mawasiliano ya chama nje ya nchi na makao makuu.
Kama ambavyo imeelezwa hapo juu, mapendekezo yaliyotolewa yameangukia katika makundi mawili. Yaani tawi libadilike kimfumo kuwa Mkoa au Jumuiya kwa kuzingatia manufaa au uzuizi kama yalivyofafanuliwa kwa kina hapa chini;
Tawi kuwa mkoa
Manufaa yake:
Mkoa utatambulika rasmi na utakuwa na uwakilishi mpaka halmashauri kuu ya chama (nec)
Kwa sababu mkoa ni mfumo ambao tayari unafanya kazi ndani ya chama, basi itakuwa ni rahisi kutekeleza mfumo huu kiutendaji.
Mkoa halitahitaji kuweka mwongozo mpya wa kiutendaji, kwa sababu mfumo wa mkoa unafuata mtiririko wa ngazi za kiutendaji za chama.
Mkoa unaweza kuwa na jumuiya nyingine mbalimbali kama utakavyohitaji kuzianzisha

Uzuizi wake:
Kwa sababu mkoa unafuata mtirirko wa ngazi za kiutendaji za chama, basi mawasiliano yake lazima yapitie kwa katibu mkuu wa chama.
Kwa sababu unafuata mtirirko wa ngazi za kiutendaji za chama uwakilishi wake unaishia tuu kwenye halmashauri kuu ya chama (NEC)
Mkoa hauna ruzuku/kasma yake ya kuendesha shughuli zake kiutendaji unafuata utaratibu wa chama kiuhitaji, kwa sababu ni structure ya ndani ya chama.
Kwa sababu hizo hapo juu mkoa ni lazima kufuata mtiririko wa katiba ya CCM taifa kiutawala, na kiutendaji.
Kwa sababu CCM nje ya nchi iko katika mazingira tofauti kabisa na nyumbani inakuwa ni vigumu kuufuata mfumo wa kimkoa uliotengenezwa kwa ajili ya mazingira ya nyumbani.

Tawi kuwa jumuiya
Manufaa yake:
Kama jumuiya itakuwa na uhuru zaidi wa kuweza kuwa na katiba yake ya kujiendesha yenyewe kama jumuiya ya wanachama wa CCM nje ya nchi.
Jumuiya itatambulika rasmi kama moja ya jumuiya za CCM na itakuwa na uwakilishi ambao sio tu katika halmashauri kuu ya chama (NEC), bali pia katika kamati kuu ya chama.
Kwa sababu ya uhuru jumuiya itakaokuwa nao, sio lazima mawasiliano yake au uchangiaji wake ndani ya chama upitie kwa katibu mkuu wa chama, hii itapanua uwigo katika kuchangia mawazo na chochote chenye kuleta maendeleo kwa ufanisi zaidi.
Jumuiya inapokea ruzuku kutoka makao makuu ya chama kuendesha shughuli zake za jumuiya. Hivyo kwa jumuiya kupata ruzuku kutasaidia ufanisi zaidi wa juhudi zake katika kuazimia maendeleo.
Kwa sababu ya mrandano wa uhitaji walionao wanaCCM nje ya nchi jumuiya inakuwa ni nzuri zaidi katika kuhakikisha yale mahitaji na uwakilishi wake unafikishwa kwa wepesi chamani.

Uzuizi wake:
Kwa sababu jumuiya haifuati mtiririko wa ngazi za chama itahitaji kujitengenezea katiba yake itakayotoa mwongozo kwa jumuiya, na hili sio kazi rahisi sana lakini, inawezekana.
Kwa sababu tayari hii itakuwa ni jumuia, inaweza kuwa vigumu kuanzisha jumuiya jumuiya zingine ndani yake, kama zitahitajika. Kama jumuiya ya vijana, wanawake,wazazi nk.
Kwa sababu uwakilishi wake utahusisha mabara yote yaani ulaya,(Uingereza na ulaya kwa jumla), Marekani, bara hindi, mashariki ya kati, na mashariki ya mbali!; basi inaweza ikawa vigumu jinsi ya kupata viongozi na uwakilishi wao kwa ufanisi.

Baada ya kusoma uchanganifu wa kina ulioanisha faida na hasara ya tawi la CCM-UK kuwa Mkoa au Jumuiya; tafadhali toa maoni na mapendekezo kuwa unapendekeza tawi lifuate mfumo upi, kwa kujibu maswali yafuatayo kwa uwazi na kwa uhuru ukijua kwamba ni haki na wajibu wako kutoa mawazo yako.
MAONI, NA MAPENDEKEZO YAKO.
Je kutokana na maelezo ya kina hayo hapo juu, wewe kama mwanachama wa CCM UK unapendekeza tawi libadilike kimuundo na liwe vipi:
Tafathali weka X kwenye mfumo unaoutaka

Mkoa

Kwa nini umependekeza tawi liwe mkoa.




Jumuiya


Kwa nini umependekeza tawi liwe Jumuiya.











AHSANTENI SANA KWA USHIRIKIANO
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI NDANI NA NJE YA NCHI
CCM HOYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE