Saturday 27 November 2010

http://www.youtube.com/watch?v=c35COXObeo8
Jumuiya ya Watanzania UK (TANZ-UK) inayoandaa shughuli za sherehe za Uhuru wa Tanzania, inakaribisha maombi ya Mtanzania/Watanzania ya kuandaa chakula cha jioni cha Kitanzania.

Sherehe za Uhuru kwa Watanzania waishio hapa Uingereza itafanyika Jumamosi, tarehe 11/12/10 katika ukumbi wa Stratford Old Town Hall, Stratford, London. Balozi, Mh. Peter Kalaghe atakuwa mgeni rasmi. Watanzania watapata fursa ya kumkaribisha UK Balozi na familia yake siku hiyo.

Sifa za mwombaji wa tenda:
>Awe Mtanzania na uzoefu wa kupika kwenye sherehe yenye zaidi ya watu 100
Tafadhali tuma maombi yako kabla ya tarehe 30 Nov. 2010.
NB: Maombi yatakayofika baada ya 30/11 hayatapokelewa.
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:
Nelly Fungo simu namba: 07951320600
au
nellyfungo@hotmail.com
Kwa taarifa zaidi ya shughulu hii tembelea tovuti ya Watanzania UK:
www.watanzaniauk.com/news
mobile no: 07424530228
email: tanzuk@ymail.com
website: www.watanzaniauk.com