Mlezi wa chama cha wafanyakazi madereva Tanzania (TADWU), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akizungumza na madereva kabla ya kukabidhiwa rasimu ya maboresho ya maslahi ya madereva hao na cheti cha utambulisho wa chama hicho Dar es Salaam jana. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Abdallah Lubara na Mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Madereva Tanzania, Clement Masanja.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Abdallah Lubara (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, rasimu ya mkataba wa maslahi ya madereva waliyokuwa wakiidai serikali kwa muda mrefu Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Madereva Tanzania, Clement Masanja (kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda cheti cha utambulisho wa chama chao kipya kitakachoitwa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU) baada kuundwa rasmi ambacho kitazindulia Julai Mosi mwaka huu.
Naibu katibu mkuu wa chama hicho, Rashid Said (kulia) akizungumzia yaliyomo kwenye rasimu hiyo na maboresho ya maslahi yao.
DC Makonda akisalimiana na madereva baada ya kumaliza kwa mkutano huo.
Madereva wakiwa wamesimama wakisubiri kusalimiana na mlezi wao DC Paul Makonda.
Ni usikivu kwa mlezi wao wakati akihutubia.
Mkutano ukiendelea.
Hapa ni furaha tupu kwa madereva hao.
Madereva wakiwa kwenye mkutano huo.
Madereva wakishangilia hutuba ya mlezi wao Paul Makonda.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea
Na Dotto Mwaibale
CHAMA cha Madereva nchini nchini kimemkabidhi mlezi wao Mkuu wa Wlaya ya Kinondoni Paul Makonda rasimu ya mkataba uliobeba maboresha ya maslahi waliokuwa wanaidai kutoka kwa wamiliki pamoja na Serikali.
Katika hatua nyingine madereva hao Julai Mosi mwaka huu wanatarajiwa kuzindua chama chao ambacho kitaitwa Chama cha Madereva Wafanyakazi Tanzania (TADWU).
Hatua ya kutengeneza rasmu hiyo hiyo imekuja baada ya kikao walichokaa Juni 21 mwaka huu ambapo lengo lilikuwa ni kuwashinikiza waajiri kuwapa mikataba ya kudumu wakiwa kazini ikiwa ni pamoja na likizo za uzazi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu katibu mkuu wa chama hicho, Rashid Said alisema rasimu ya mkataba huo imebeba maboresho ya maslahi yao waliyokuwa wanadai.
Alisema madai hayo ni pamoja na bima ya maisha , mazishi yenye staha, muda wa kazi kisheria, matibabu, na nauli ya kwenda kazini.
"Leo tuna chama cha wafanyakazi madereva Tanzania , pia tumepewa mkataba hivyo nawatangazia madereva wote kuwa tumepata chombo cha kuzungumzia tofauti na ilivyokuwa awali.
Kwa sasa imebaki kujadili na serikali kuhusu kuboreshwa kwa mishahara hivyo napenda kuwatangazia madereva kuwa tumepata mikataba tuliyohitaji miaka mingi,"alisema.
Katibu huyo aliongeza kuwa chama hicho hakitasita kumchulia hatua za kisheria mmiliki atakayekiuka sheria hizo na kuongeza hakitasitakumpeleka kwenye vyombo vya sheria kama walivyokuwa wanawafanyia mwanzoni.
Akikabidhiwa mkataba huo kwa chama hicho, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alisema mahali walipofikia madereva hao kwa sasa ni jambo la kuleta maendele makubwa.
Alisema watanzania wanatakiwa kutambua kuwa madai hayo si kwa ajili ya madereva peke yao bali ni kwa ajili ya taifa zima na kwamba kutatuliwa kwa changamoto hiyo kutapunguza ajali zinazoendelea kutokea nchini.
Makonda alisema asilimia kubwa ya madereva wamekuwa wakipata ajali kutokana na kuchoka hivyo wanaposinzia usahau kuwa wanaendesha vyombo vya moto hivyo kusababisha ajali.
Katika hatua nyingine Makonda alisema kuwa asilimia 80 ya waandishi wa habari hawana mikataba ya kudumu na kwamba ni changamoto hivyo aliwataka kwenda kuonana nae ili kupata ushauri wa namna ya kuwawezesha kuhakikisha wanapewa mikataba ya ajira na waajiri wao. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)