Sunday, 28 June 2015


Kwenye kilichosikika jana June 25 2015 toka ndani ya Kikao cha Bunge Dodoma ilikuwepo pia ishu ya Mbunge Martha Mlata kuanzisha mjadala kuhusu amri ya Mahakama kwamba Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi Sugu akabidhiwe mtoto wake ambae amezaa na Faiza Ally kutokana na Mbunge huyo kuonekana kutoridhwishwa na malezi ya mtoto akiwa kwenye mikono ya mama yake.

Ombi likapokelewa kwenye meza ya Naibu Spika leo June 26 2015 >>>”Nimepokea ombi maalum la kuwasilisha maombi binafsi kutoka kwa Mbunge Joseph Mbilinyi kwa hiyo namruhusu” >>> Naibu Spika Job Ndugai.

“Asante sana Naibu Spika, naomba nitoe maelezo binafsi jana tarehe 25 June 2015, Mbunge Martha Mlata alidai kuwa kuna Mbunge wa CHADEMA amempora mwanamke mmoja mtoto mdogo wa miaka miwili na amempora wakati Mbunge huyo amekuwa hatoi matunzo kwa mama yake… Mlata aliwataka Wabunge wote wanawake kuungana kukemea kitendo alichodai kimefanywa na Mbunge huyo”



“Hakutaja jina la Mbunge aliyemhusisha na madai yake ila alidai kuwa ni msanii mwenzake… hata hivyo alitaja jina la mwanamke anayedaiwa kunyang’anywa mtoto kuwa ni Faiza. Mbunge aliyelengwa na mashambulizi ni mimi Joseph Osmond Mbilinyi, mimi ndiye baba wa mtoto Sasha Desderia Mbilinyi anaedaiwa kuporwa kwa mama yake, na Faiza aliyetajwa ni Faiza Abdallah Ally ambaye ni mzazi mwenzangu na mama mzazi wa Sasha Desderia“

“Watu wazima hawapendelei kuzungumzia mambo binafsi hadharani… Nadhani sitakosea kusema hata Mheshimiwa Martha mwenyewe asingependa kuzungumzia matatizo yaliyopelekea ndoa yake kuvunjika“


“Mimi ni mmoja wa watu wazima wenye akili timamu ndio maana sijazungumzia hadharani kuhusu uhusiano wangu na mzazi mwenzangu Faiza Ally na mtoto wetu Sasha… Sasha ameishi na mama yake tangu alipozaliwa mwaka 2012, katika kipindi chote nimempelekea mama yake laki tano kila mwezi, nimemlipia ada ya shule Milioni 3 kila mwaka.. Mlata kama angekuwa anataka kujua angeniuliza ningempatia taarifa hizi kabla hajarusha tuhuma nzito“

Sugu 10“Mwanamke anayedaiwa kuwa mnyonge anajulikana katika kumbi za starehe nchi nzima, picha zake zilisambazwa katika Mitandao ya Kijamii na kuleta fedheha kubwa kwa watu wanaojali maadili ya mavazi, picha zake nyingine akiwa amevaa diapers zilisambaa mitandaoni na Martha Mlata angeweza kupata ukweli wa mambo haya kabla hajarusha tuhuma mbele ya Bunge“

Sugu 7“Nilienda Mahakama ya Mwanzo Manzese, niliwasilisha ushahidi kwamba mzazi mwenzangu asingeweza kumlea mtoto.. Mahakama ilimwita akajitetea, June 23 Mahakama iliridhika na ushahidi wangu, ikaamua mtoto akabidhiwe kwangu ili nimlee. Kilichodaiwa kuwa ni uporaji wa mtoto kiukweli ni amri ya Mahakama, Mlata hakuwahi kuonekana Mahakamani, nina mashaka hata kama anamfahamu mtoto mwenyewe au mama anayemwita mwanamke mnyonge“

“Mashauri haya hayakupaswa kuwekwa hadharani kama alivyofanya Martha Mlata… Nimesikitishwa na Martha Mlata kuzungumza mambo binafsi. Pamoja na Mahakama kunipa haki, mtoto bado yuko kwa mama yake kwa sababu mimi ni mstaarabu… nimetoa nafasi ili Majadiliano ya kifamilia yafanyike… Naomba mjadala huu usiendelee zaidi ya hapa” >>>Mbunge Joseph Mbilinyi.