Sunday, 16 June 2013

Coventry Women Gala ya Tarehe-08/06/2013[Sehemu ya 2]Mgeni Alikuwa Mama Balozi JOYCE KALLAGE!!!


Waungwana;Tunaendelea na Matukio ya Coventry Women Gala...Mama Balozi Joyce Kallage na Da'Rose Kiondo..Wakifurahi Pamoja..ni Raha tuu..
Da'Agness akikaribisha Wageni na kujitambulisha.

Da'Halima akijitambulisha na kuwahakikishia watu Watashiba..

Hawa walisimamia Chakula na Kukaribisha Wageni.

Da'Stella akijitambulisha ..Yeye alikuwa msimamizi mkuu.

Da'Mija akijitambulisha..Yeye alisimamia Mitindo

Da'Rachel akijitambulisha..Yeye alisimamia Buruda, ndiye aliyepamba Ukumbi na Mc..
DJ Richie Dee..Yeye ndiyo aliyetuburudisha[Muziki]

Mama Balozi ;JOYCE KALLAGE;
Yeye alitupongeza na kutusisitiza kuendelea na masomo,Kusaidia watoto wengine wa kike Nyumbani wanaohitaji Kuendelea na Masomo lakini hawana uwezo.Kuungana  na kujitoa kwa Moyo na kufanya mambo mengi ya maendeleo.Pia alisisitiza sana tusijisahau Kufuata na kuendeleza mambo mema ya Kwetu..Hategemei mtoto wa mswahili asijue kiswahili ni aibu.Kama tumeshaliachia hili watoto wetu hawajui "KISWAHILI" Tufungue darasa la Kiswahili.
Aliongea Meengi.
Asante sana MAMA,Nasi tutafuata Ushauri wako.
[TEAM MAMA BALOZI]

Wanawake Oyeee!!!!Coventry Women Gala Oyeee!!!!!Waswahili Ughaibuni Juu!!!!!Wanawake na Maendeleo!!!!!
Amesema amefurahi kuona tumeweza kurudia tena!!

Hayo yote kwa furaha na unyenyekevu yalitoka kwa da'MARIAM KILUMANGA;Mwenyekiti wa;Tanzania Women's Association[TAWA UK.]
Alisisitiza Tusikate Tamaa na yupo pamoja nasi wakati wowote..Da'Mariam tulikuwa nae wakati uliopita.
Asante Saaaaana.
Dada/Mama;Hilda..Yeye ni Mfanyabiashara wa siku nyimgi,Amepitia changamoto nyingi sana.
Na sasa amesimama vilivyo..Ametufunza mambo mengi sana..alisema yeye si muongeaji sana..Mzuri sana kwenye Vitendo.

Asante Sana kwa Yote mama.


Dada;ROSE KIONDO,Kutoka Ubalozi wetu wa Tanzania hapa UK.

Da'ROSE KIONDO;Yeye alitusisitiza kujihusisha na Ubalozini kwani pale ni kwetu na tutambue hivyo..kwanini tunakuwa waoga na Nyumbani kwetu?Mtu hujivunia chake na kwako..kwa hapa tulipo Pale ndiyo Nyumbani,Wapo pale kwa sababu yetu pia.Aliongea Meengi yenye Faida kwetu.

Asante sana dada.

Alicheza kwanza..

Alitumia vilivyo uwanja...

Mc..mwenyewe hoii..usimchezee kabisa..Mada zake anazitunza vilivyo..

Ni-Aunty/Mama da'Fay..wewe utakavyo penda kumuita yeye hana shida..Yeye alitusisitiza zaidi,kutumia muda vizuri,kujiendeleza kielimu kwani haina mwisho..atakushangaa eti ukisema sina muda kwasababu nina watoto,mume,kazini,kazi za nyumbani..Ukiamua na kama wewe ni msomaji utasoma tuu..ni wewe utakavyojipanga..kila siku utasema muda huna mpaka lini?Tusipoteze muda kwenye mambo yasiyo na manufaa..hasa  tutumie hii MITANDAO vyema na si kutukanana na kuumizana..Tupendane..
Bila kusahau DIET..Na kutafuta mbinu ya kupunguza mwili..Aliongea meengi saana siwezi kumaliza yote hapa..


EPUKA UZEE USIOKUWA WAKO BIBI EEEEEHH.
.

Da'SUSAN

DA'SUSAN yeye aliongelea MADAWA YA KULEVYA..Utayajuaje,Watumiaji,kuepuka,uuzaji,Madhara yake na kuwalinda watoto wetu,Vijana,Jamii na nasisi wenyewe pia..Na mambo mengii yahusianayo na Madawa ya kulevya..

Asante sana.
Umeona hiyo beji niliyo jibandika hapo? Hawa wanatengeneza keki,beji na mengine meengi..ni wadada wanaojituma..ni AHLAMA NA KOIYA..Wape Kazi watoto wa Nyumbani..
Hongereni Sana

Da'TINNA..Yeye ni mwimbaji  mzuri sana sauti MUNGU amemjaalia..usisite kumpa kazi. Dada/Mtoto wa Nyumbani.ni burudani tosha sauti yake.

Mama Balozi,Wageni walipata Nafasi  ya kuona/kununua bidhaa mbalimbali kutoka kwa wanawake Wenzao...


Wewe unangoja nini?
Jitoe,Jitambulishe/Tambulisha kazi zako.Ujuzi wako..
Nategemea Kuwaona Wanawake wengi Shughuli ijayo..








kuona zaidi ingia hapa;








Mikakati/Majukumu..da'Halima na da'Rachel








Watu Wamependeza,Wamefurahi..Raha teleee Tabu za nini?



Watu wameshiba, na Wanakusikiliza,Kujifunza ...Inapendeza sana..

Mama Balozi,Da'Rose na Wageni..Ni furaha tupu na kucheza Pamoja......





Baaada ya kazi na kuhakikisha mambo yamekwenda sawa bin sawayaa tulicheza saana...






NIVicheko saaana..hapa da'Mariam alituchekesha saana..







Mapoziii na mama Balozi..[TEAM MAMA BALOZI]Hakuna mchezo baada ya kazi ni furaha tuu..



Shukrani Saaana na MUNGU awabari!!!!
Karibuni tena kwenye Coventry Women Gala Ijayo.. Mwezi wa TISA..,Wapi.Tarehe..Tuawafahamisha..

      Kwaniaba ya Team nzima ya Coventry Women Gala..
Tunawashukuru sana..
  Mama Mabalozi JOYCE KALLAGE,dada MARIAM KILUMANGA,DADA ROSE KIONDO,DADA HILDA,AUNTY FAY,WAGENI WETU WOTE..
WOTE WALIOSHIRIKI KWA NAMNA YOYOTE VILE..MUNGU AWABARI SANA. 

KAMA KUNA TULIPOKOSEA MTUSAMEHE SI NIA YETU.
PIA MNAWEZA KUTUSHAURI,MAONI NA KUTUELIMISHA KWA UPENDO.

TUNAWAPENDA SANA NA KUWATHAMINI WOTE.

Nikiripoti kutoka "Coventry Women Gala" ni mimi RACHEL-Siwa wa Swahili NA Waswahili-Mitindo Africa na Nga'mbo!!!