Tuesday, 19 February 2013TANZANIA HIGH COMMISSION 
 
Telephone: 020 7569 1470                                                                                                               3 Stratford Place    
Facsimile:  020 7495 8817                                                                                      London W1C 1AS              

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI, MHE. PROF. DK SOSPETER MUHONGO (MB), KUKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI UINGEREZA TAREHE 26/02/2013

Waziri wa Nishati na Madini wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof. Dk Sospeter Muhongo, anatarajia kufanya ziara ya kikazi nchini Uingereza kuanzia tarehe 25 hadi 28 Februari 2013.
Akiwa London Mhe. Waziri angependa kukutana na Watanzania waishio Uingereza kuzungumzia maendeleo ya sekta ya nishati na madini Tanzania na pia kubadilishana nao mawazo kuhusu maendeleo ya sekta hiyo.
Ubalozi wa Tanzania, London unapenda kuwakaribisha watanzania siku ya Jumanne tarehe 26, Februari 2013, Ubalozini saa 11 Jioni. Anuani ya Ubalozi ni 3 Stratford Place, W1C 1AS, London

Wote mnakaribishwa.